Tutazame historia inatufundisha nini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutazame historia inatufundisha nini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LGMJAMII, Jan 6, 2011.

 1. L

  LGMJAMII Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nazani Kama Hatuna macho ya kuona au kama Hatuna masikio ya kusikia, Basi Tutazame Historia, Tuone Historia inatukumbusha nini?

  Daima Tukiangalia Historia tutaona kwamba UDHALIMU au NGUVU au UBABE au UONEVU dhidi ya Jamii inayokandamizwa huwa ina mwisho. Tuliona Hitler, Musolin, Poland na Ushoshalisti wao na pengine pia, walikuja lakini Mwishowe Nguvu ya Umma ya Wanyonge Walikuja kushinda au kupata nafasi ya Kutulia dhidi ya uonevu au ukandamizaji waliokuwa wanatendewa.

  Nazani ningependa kuwakumbusha watu wachache, Wenye kupenda kuwakandamiza Watanzania, au kuwaonea au kwa makusudi kupitisha mikataba ya kujirikimbizia mali huku wakijua kuwa wanawapa Mzigo watanzania- Kuwa wasisahau Mwisho wa hayo yote yapo, na mwisho huwa mbaya sana na aibu.

  ALUTA CONTINUA, Tanzania Itasonga na Siku moja Watanzania watakuja kuonja Raha na Matunda Ya nchi yao.
   
 2. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,269
  Likes Received: 2,047
  Trophy Points: 280
  Tanzania itasonga mbele lakini CHADEAMA kamwe haiwezi kusonga kwani watanzania hatupendi fujo kamwe!
   
 3. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ndio ushabiki wa kijinga! Hata kama wewe ni CCM unapaswa kufikiri vizuri sio CHADEMA wanaoleta vurugu bali ni CCM. Walipewa kibali cha maandamano na mkutano wa hadhara na RPC Andengenye lakini dakika za mwisho IGP akazuia maandamano kwamba kungekuwa na vurugu. CHADEMA wakaandamana kwa amani kuelekea mkutanoni, lakini POLISI wakaleta vurugu na kuua! Kumbuka pia kutokana na sheria ya vyama vingi ya 1992, maandamano ni haki ya kila chama na polisi wanapaswa kupewa tu taarifa masaa 48 kabla ya maandamano. Sasa kama polisi walikuwa na uwezo wa kutumia nguvu zote zile dhidi ya maandamano ya amani walishindwaje kutoa ulinzi kwa CHADEMA? CCM wanajipa umeya kama Arusha na sehemu nyingine walizopata madiwani wachache wanavuruga uchaguzi kama vile Mwanza, Hai na Moshi mjini. Sasa katika mazingira hayo ni nani anayeleta vurugu CHADEMA au CCM? Kalagabaho kumbuka pia kuwa dola haiwezi kuizidi ngumu ya umma, ipo siku CCM yako na dola yenu itashindwa tu!!
   
Loading...