Bila huruma ya CCM hakuna mpinzani atakayeingia Bungeni

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,709
Ndugu zangu watanzania,

Kwa Sasa watanzania hawana Imani kabisa na upinzani na wapinzani,hawawaamini wapinzani kwa kuwa wameona ni watu waliokosa msimamo, vigeu geu,njaa Kali, hawawaamini kwa kuwa wanaona wapinzani Ni watu unaoweza kuwapigia Kura Leo na kesho wakakimbia.

Hakuna mwananchi mwenye Akili Timamu anayeweza kuhatarisha maisha yake au kuwa Tayari kupigwa mabomu au kupata kilema Cha mguu au kuvunjwa mkono kwa kumpigania mpinzani awe mbunge wakati anajuwa kesho atakimbiwa na kuachwa bila msaada wowote,anajuwa hakuna mpinzani anayepigania maslahi ya wananchi zaidi ya Tumbo lake,anajuwa kitu pekee Cha kumwamini mpinzani na ambacho hawezi kukataa au kugeuka Ni juu ya jinsia yake tu.

Watanzania wamejifunza kuwa wapinzani Ni watu pale wanapotafuta ubunge na udiwani tu lakini wakishapita wanageuka kuwa na Dunia Yao,ndio maana siyo ajabu akina Lema na viongozi wengine wa chadema walikuja na kuwatukana watanzania kuwa Ni maskini na wanaofanya kazi zilizolaaniwa,wakasahau kuwa Ni hao hao ndio waliowafikisha hapo walipo fika na kufahamika, wanapoteza kumbukumbu kuwa Ni hao ndio waliowapa heshima na kuwaheshimisha maana wengine walichangiwa kwa kila kitu mpaka kuwa viongozi lakini mwisho wa siku walipovimbiwa viinua mgongo vyao wakaja kuwatapikia watanzania matusi ya udhalilishaji.

Watanzania wametambua kuwa Ni CCM pekee yenye uwezo wa kiuongozi,Ni CCM pekee yenye uchungu na maisha yao,Ni CCM pekee yenye kubeba ajenda ,Sera na ilani yenye kugusa maisha Yao,Ni CCM pekee yenye uwezo wa kusimamia Rasilimali za Taifa letu kwa maslahi ya watanzania wote,ndio sababu ya Kuendelea kuiamini,kuiunga mkono,kuitetea,kuipigania na kuipigia kura kila uchaguzi,ndio sababu ya kuipa ushindi katika kila ngazi ,ndio sababu ya kutomkubalia yeyote atakaye taka Kuchezea amani ya Taifa letu Wala kuwashawishi na kushawishika kuipinga serikali ya CCM.

Ni jukumu la CCM kulinda heshima hii iliyopewa na watanzania kwa Kuendelea kuchapa kazi kwa uadilifu,uzalendo na kugusa maisha ya watu, kuwasikiliza watu,kuwa karibu nao,kutatua kero zao,kutoa majibu kwa wakati,kuwalinda dhidi ya wanyonyaji,kutumia Rasilimali zetu kuwapatia huduma Bora na stahiki watanzania,kuja na ilani itakayoendana na wakati na mahitaji ya wakati pamoja na kuja na wagombea wenye kujua Mahitaji ya watanzania, kero na changamoto zao, wazalendo na wachapakazi, waadilifu,wenye historia nzuri kiutendaji,waaminifu na wasema kweli ,wenye kuzungumza lugha za watu juu ya Mahitaji Yao,wenye kuwa karibu na watu ,wenye kujuwa cheo Ni dhamana na ni kwa ajili ya watu pamoja na kujuwa kuwa uongozi Ni utumishi kwa watu.

Ni lazima CCM ilindwe kwa nguvu zote kwa jasho ,machozi na Damu ili iendeleee Kusalia madarakani maana Hawa wengine watalipasua Taifa letu,kwa kuwa hawana Uzalendo na Taifa letu Wala uchungu na maisha ya watanzania Ndio maana Ni kawaida kusikia makauli ya ajabu ajabu kutoka katika vinywa vya viongozi wa upinzani kwa kuwa wao na familia zao wanajuwa wataweza kwenda marekani na ulaya kutanua maisha na kuwaacha watanzania wakiteseka ,Ndio maana watanzania hatupo tayari kuruhusu Hilo kutokea hapa nchini kwa kuwapa Kura na madaraka upinzani na kuisaliti CCM iliyotufikisha hapa kwa kututumikia kwa upendo uzalendo na unyenyekevu mkubwa na uliotukuka ,CCM haitaachia madaraka na hiyo ndio kauli ya mamillioni ya watanzania wazalendo wa Taifa letu.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Ndugu zangu watanzania,

Kwa Sasa watanzania hawana Imani kabisa na upinzani na wapinzani,hawawaamini wapinzani kwa kuwa wameona ni watu waliokosa msimamo...
He Ukisoma au kupitia dondoo za Ripoti ya CAG ambayo Rais wako alipatwa na mshangao hadi kutamka Neno "STUPID" ni Nani walengwa? Kwani ni wapinzani ndio wametafuna hiyo pesa?

CCM ni mamluki, Wezi, wala Rushwa na waharibifu.

Hatuwezi kuwa na Shule mbovu na vyoo hakuna etintynasubiri Msaada.

Huku walioiga hata pesa za Halmashauri.

KATIBA iitiahe Haki na Tume huru Uchaguzi ufanyike Kwa haki hayo uje ubadilishe somo la huu Uzi wako wa kijinga.
 
Sio wapinzani tu, hata waliopo CCM wapo kwa ajili ya matumbo yao. Hakuna mwanasiasa yeyote ambaye yupo eti kwa ajili ya maslahi ya wananchi.

Wazalendo wengi siasa hawazijui. Waliopo kwenye siasa ni wababaishaji.
Viongozi wa CCm wapo kwa ajili ya kuwapigania na kuwatetea watanzania
 
He Ukisoma au kupitia dondoo za Ripoti ya CAG ambayo Rais wako alipatwa na mshangao hadi kutamka Neno "STUPID" ni Nani walengwa? Kwani ni wapinzani ndio wametafuna hiyo pesa....
Wachache wanaokwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma na viapo vyao watakutana na mkono wa Sheria ambapo kwa hakika watajuta kwa matendo yao ya kirafi na kibinafsi, katika hili Rais wetu Hana Subira
 
Kweli sasa nimeamini kuwa UJINGA NI KIPAJI kama vile mpira na Ronaldo, riadha na Nyambui au Bayi, Comedi na Kingwendu na hivyo Lucas mwashambwa na ujinga.
Utaniwia radhi lakini hicho ndio kipaji chako ulichojaliwa na wengi hawana kabisa.
Hoja hujibiwa kwa hoja,hivi kwa mtusi ya akina Lema,lissu,heche n.k ni Nani wakuwapigia kura Upinzani!
 
Back
Top Bottom