Tutarajie nini baada ya kauli hii?

Stopper3

JF-Expert Member
Sep 1, 2019
625
1,030
Baada ya mijadala mitandaoni, hii ni kauli ya Mbwana Samatta. Je, tutarajie mabadiliko yoyote kutoka kwa Captain, au ataendelea kupuyanga?

Je, kwa Tweet yake hii ni kweli amegundua alikuwa hajitumi?

IMG_20191121_080829_848.jpeg
 
Binafsi nimeelewa maelezo ya Nahodha wa Taifa Stars. Ila ningependa nimkumbushe tu mdogo wangu kwamba Soka ni mchezo wa HISIA! Hisia hizi zinakuwa za mchanganyiko, zipo za furaha/mapenzi na zipo za huzuni/chuki pia. Bahati mbaya sana Soka la kileo limepitia mbadiliko mengi ikiwemo ya Kiteknolojia. Watanzania wanakupenda na wanakufatilia sana hapa nyumbani.

Matokeo yake wanafatilia Ligi ya Ubelgiji na Mashindano mengine unayocheza, kifupi wanaujua uwezo wako. Pia wanafatilia na Ligi mbalimbali Duniani na Mashindano tofauti tofauti kwahiyo uwezo wao wa uelewa wa mambo haya umeongezeka sana ingawa kwa viwango vianvyopishana kutokana na Taaluma zao. Soka kiasili linachezwa eneo la wazi na kila mmoja ana uwezo wa kuona kinachofanyika wakati mchezo unachezwa na kujua nani kapatia na nani Kakosea kama ambavyo wachezaji pia mnajua nani leo Kazingua na nani alikuwa poa, hata wewe mwenyewe unajua siku unapopatia na unapozingua pia.

HISIA ndizo zinafanya mashabiki wajichore picha yako na kuandika jina lako MBWANA SAMATTA kwenye miili yao na Mabango wanayoyashikilia kwa dakika 90 za mchezo. Kuwalipa hawa watu kwa kuonyesha HISIA za furaha/mapenzi kwako na Taifa Unapaswa KUJITUMA SANA kuliko unavyofanya sasa. Watanzania wanapenda kuona kinachotoea Genk kitokee na Taifa Stars. Wao wanasema sio lazima ufunge ila UFIE timu tu PERIOD! Wanajua kila mmoja ana uwezo na majukumu yake kiwanjani lakini wanasema mipira kwako inapotea kirahisi sana na ikipotea UNATEMBEA au muda mwingine UNACHEKA wenzio wanaendelea kupambana kutafuta mipira unayopoteza.

Binafsi nimesikia na kusoma tetezi mbalimbali kutoka kwa watu mbalimbali pia, ila niwashauri kwamba wamuache Samatta ajitetee mwenyewe kiwanjani mpira ni mchezo wa wazi mno na Watanzania wanaupenda na kufatilia sana, mara nyingine mnajivunjia heshima kutetea Upuuzi usio na Tija. Hakuna anayemchukia Mbwana Samatta miongoni kwa wapenda soka na wanampenda na kumsifia akifanya vizuri kwahiyo akikosea wanamwambia pia na wala huku sio Kumkosea Heshima bali ni kumkumbusha majukumu makubwa na matarajio anayobeba mabegani mwake. Watanzania si wajinga!


Mwandishi: Jemedari Said Kazumari

FB_IMG_1574317791018.jpg
 
Tulitaka awe kipa yeye, beki yeye, mkabaji yeye, mfungaji yeye? Hapana, ndio maana ikaitwa Team!
Nyie watetezi mwenyewe kakubali kukosolewa mbona kila siku watu wanalalamika huku naniliu hapendi kukosolewa ila haohao mnalalamika kila sikumnapinga mtu kukosolewa,Samatta yeye nani asikosolewe? Tuache ushamba mpira hauchezwi chumbani
 
Baada ya mijadala mitandaoni, hii ni kauli ya Mbwana Samatta. Je, tutarajie mabadiliko yoyote kutoka kwa Captain, au ataendelea kupuyanga?

Je, kwa Tweet yake hii ni kweli amegundua alikuwa hajitumi?

Najiuliza kwani huyu Bwana Mbwana alikuwa anachezea timu nzima na watu walihitaji kiwango cha timu au cha Mbwana? bado sielewi elewi kuna redio moja imemshambulia sana jana nkashindwa kuelewa watu huwa wanafikiri vipi.

Mbwana amekuwa na kiwango cha Mesi? kusema tuiite Taifa stars kuwa na uwezo wa kuwa timu mbili kwa mara moja yani Taifa stars yenyewe na Mbwana akiwa timu ya pili binafsi kwa uelewa wangu mdogo sidhani kama Mbwana amefikia level hiyo.
 
Champion boy

Kichape Genk, huku Bongo wakikuzingua staafu tu waachie timu yao kichwaa cha mwenda wazimu kama vipi hata uraia unabadili tu.

Haina kufeli
Ndomaana ikaitwa kichwa cha mwendawazimu sababu kila mtu ana mamlaka ya kuongea na kufanya maamuzi
 
Nyie watetezi mwenyewe kakubali kukosolewa mbona kila siku watu wanalalamika huku naniliu hapendi kukosolewa ila haohao mnalalamika kila sikumnapinga mtu kukosolewa,Samatta yeye nani asikosolewe? Tuache ushamba mpira hauchezwi chumbani
mbona umemshkia bango sana samatta vp mzee kwani ameua au alikuchania mikeka? uwe muelewa siyo mechi mbili tatu tu unalalamika kama umenyimwa mshahara
 
Comment yako haieleweki mkuu, hebu iandike upya.
Hizo ndo akili za wabongo kumfukuza stars wameona haitoshi wanataka wamfukuzishe na Genk badala yake aende Nchimbi, akihamia newcastle watamuandama tena.. wabongo bila kuwaletea ugumu watakuburuza sana
 
Back
Top Bottom