Ndoa za mikataba zinahitajika sasa..3 years, 5 years , 20 years or forever till death.
Ndoa ni mkataba, ila wa kudumu (maisha), hizo nyingine 3,5 nk ni uzinzi tu wa kawaida ambao upo katika maisha yetu ya kila siku ambao tukiutenda tunapaswa kutubu na kuomba msamaha mbele ya Mungu. Kumbe basi kwa kufanya hivyo hatuwezi kuita hiyo kitu kuwa ni ndoa takatifu eti kwa miaka say 10, then what next.
Ndio maana ikaandikwa katika kitabu kitakatifu (Biblia), alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe, pia Ndoa na iheshimiwe na watu wote.
Kwa ndoa za Kiislamu najua ni tofauti, huko talaka zipo hata kama ukiingia leo, ukajisikia kutoka kesho yake, sharti tu ufuate taratibu zao then unatoka na kuwa huru kuanza maisha mapya.
Lakini ni ukweli usiopingika kuwa hata kama kungelikuwa na hiyo opportunity ya kufunga ndoa za mikataba say 5 year, kuna wengine wangelazikamika kuongeza mikataba yao several times na mwisho wa siku wanakufa pamoja, maana muda unaweza kuisha, lakini ukimwangalia mwenzako kwa jinsi ambavyo mmekwisha zoeana, mnavyoendana, mnavyoridhishana kwenye kila idara, nk, unajiuliza utoke uende wapi tena?