Tutakukumbuka daima Mzee RK…

Tutakukumbuka daima Mzee RK…

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
Siku na tarehe kama ya leo mwaka 2008 majira ya saa 2:30 asubuhi ndio siku ambayo baba yetu mpendwa mzee RK ulipoiaga dunia ukiwa na umri wa miaka 76. Ilikuwa ni Ijumaa ya terehe 4/1/2008 ndiyo siku ambayo baba yetu mpendwa alipoiaga dunia baada ya kuugua kansa ya koo kwa takriban mwaka mmoja.

Ulikuwa ni msiba mkubwa sana kwetu kutokana na juhudi zako za kutulea ukiwa peke yako baada ya kifo cha mama yetu hapo mnamo tarehe 1/8/1982 akikuachia jukumu la kulea watoto 8, watatu wa kike na watano wa kiume. Ingawa kaka zangu 3 na dada zangu 2 walishakuwa wakubwa kwa umri na kimo, ni mimi na wadogo zangu wawili, mmoja wa kike na wa mwisho wa kiume ndio tulioachwa na mama tukiwa na umri wa chini ya miaka 11.

Tunakumbuka kauli yako baada ya kifo cha mama yetu kwamba hutaoa mke mwingine mpaka hapo utakapotulea na kuwa watu wazima na kujitegemea na hiyo ilitokana na hofu yako ya malezi ya mama wa kambo kutokana na imani kwamba malezi ya mama wa kambo yana walakini. Sina uhakika sana na jambo hilo lakini huo ulikuwa ndio uamuzi wako.

Kwa juhudi zako na kwa kusaidiana na kaka na dada zangu ulimudu kutulea mimi na wadogo zangu hadi tukafikia umri wa kujitegemea. Ni mapenzi yako na malezi yako mahiri ndiyo yaliyoifanya familia yako ya watoto 7 tuliobaki, kushikamana hadi leo bila kusambaratika, baada ya dada yetu mkubwa na mlezi wetu aliyechukua jukumu la mama kufariki hapo mnamo tarehe 5/5/1994 kwa kifafa cha mimba.

Tumejifunza mengi sana kwako, lakini lililo muhimu sana kwetu ni kutusisitiza kujiamini na kujitegemea kwa kila kitu. Nakumbuka msemo wako kwamba mtegemea cha ndugu hufa masikini, msemo huu ndio ulikuwa kama kauli mbiu yako ya kutuchagiza kila mtu kujitegemea bila kutegemea msaada kutoka kwa ndugu.

Leo hii imetimia miaka mitano tangu ututoke, na tunakukumbuka sana kwa hekima na busara zako. Ulikuwa mcheshi na mwenye furaha wakati wote na hata pale ulipokuwa umezongwa na jambo, bado tabasamu lako lilikuwa halikuishi usoni pako, ilikuwa ni vigumu kwetu kujua ni wakati gani ulikuwa na huzuni, ulikuwa ni mwerevu wa kubadili jambo lililokukera na kuliweka katika mzaha na hivyo kutokukuumiza kihisia. Lakini hata hivyo, hukusita kuonyesha hasira zako pale ilipobidi.

Tumeendelea kufuata nyayo zako na hivi sasa familia yetu imezidi kushikamana na kuwa imara, na wote tunatamani kama ungekuwepo leo hii na kushuhudia kile ulichokipanda maana sasa ndio tunaona matunda ya malezi yako. Tumejijengea heshima mbele ya jamii sio kwa sababu ya mali wala fedha, bali kwa sababu ya hekima na busara ulizotuachia kama moja ya nguzo muhimu katika maisha.

Tunaomba Mwenye enzi Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi, amina.
 
Mungu amrehemu Mzee RK katika makao yake ya milele,amen.Dah pole sana Mtambuzi katika kipindi kama hiki unapomkumbuka baba yetu mzee RK
 
Mkuu huyu RK ninani??....>>>>Pole sana mkuu mungu aendelee kuwapa nguvu na kuwa na mshikamano huo mliokuwa nao namwisho mungu aendelee kumuondolea adhabu ya umauti mpaka hapo siku ya kiyama!ili mkakutane tena kujenga familia moja!Amen
 
Mungu aendelee kumlaza mahali pema peponi baba yetu mpendwa.

Mzee mwenzangu Mtambuzi jitahidi kumuenzi mzee wetu kwa kuiga na kutenda yale mema aliyoyafanya.

Pamoja sana.

Pamoja sana mkuu.
Naamini hata wana JF wamenufaika na urithi alioniachia Mzee RK.
 
Hongera kwa malezi mazuri ambayo ni urithi mkubwa toka kwa baba yenu mpendwa. Mungu ampe pumziko la amani. Amina!
 
Daima Baba mpo nae ndani ya nafsi zenu kutokana na yale mema aliyo walisisha. Tumuenzi kwa kutii yale aliyo tuagiza kuyatenda katikamaisha yetu yote ya hapa Dunian
 
Pole sana Mtambuzi na familia kwa ujumla....

Kumpoteza mzazi ndiyo loss kubwa anayoweza kuipata binadamu hapa duniani...

Raha ya milele umpe ee bwana, na mwanga wa milele umwangazie mzee RK,

Apumzike kwa amani....AMEN!!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu Mtambuzi kazi ya Mungu haina makosa ni yeye alituumba na ni yeye pekee mwenye mamlaka ya kutuchukua kadri apendavyo.Pamoja sana katika kumbukumbu ya Mzee RK.

Swali la kichokozi baada ya wewe na wadogo zako kufikisha umri wa kujitegemea Mzee RK alibahatika kumpata mwenza wa kumliwaza.
 
Pole sana mkuu Mtambuzi kazi ya Mungu haina makosa ni yeye alituumba na ni yeye pekee mwenye mamlaka ya kutuchukua kadri apendavyo.Pamoja sana katika kumbukumbu ya Mzee RK.

Swali la kichokozi baada ya wewe na wadogo zako kufikisha umri wa kujitegemea Mzee RK alibahatika kumpata mwenza wa kumliwaza.

Samahani hilo sikuliweka kwa sababu binafsi, lakini kwa kuwa umeuliza nitakujibu.
Alimpata mtu mzima mwenzie na walidumu kwa miaka sita hivi lakini the choice he made didn't work out the way he thought it would....
 
Swali lingine dogo Mzee RK anatoka upareni maana Kilimanjaro kubwa mzee kuanzia Hai,Machame,Huru,Old Moshi,Marangu,Mamba,Mwika,Kilema,Rombo,Same....

Hapana ni RK wa Mkoani Kilimanjaro
 
Swali lingine dogo Mzee RK anatoka upareni maana Kilimanjaro kubwa mzee kuanzia Hai,Machame,Huru,Old Moshi,Marangu,Mamba,Mwika,Kilema,Rombo,Same....

Upareni mkuu wilaya ya Same.........
 
Rest In Peace mzee wetu RK.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom