Tutailipa ACACIA, Ila tuing'oe CCM kwanza

Tutailipa ACACIA, Ila tuing'oe CCM kwanza

Hakuna jipya kwenye maelezo yako
Tuing'oe CCM halafu tumuweke nani?
Kwenye biblia kitabu cha Mwanzo wakati Adam na Eva wamekula tunda la mti wa katika,Mungu alitoa adhabu kwa kila mmoja aliyehusika, yani mpaka shetani alipewa adhabu!

Kisha Mungu akawafukuza Adam na Eva kwenye Bustani na akamuweka malaika mwenye upanga wa moto kuulinda ule mti wa katikati.

Sasa basi, sio Mkapa wala CCM wala yeyote aliyeshiriki ataachwa. Kila mmoja apewe adhabu inayomstahili halafu tuwafukuze pale ikulu.
 
Kuongea mbali na vitendo mbali,tukiwa fukuza ccm ikulu tumuweke nani?
 
Hivi aliyewaambia ACACIA watashinda kesi ni nani? Mbona watanzania hamjiamini, kesi kufunguliwa London au sehemu nyingine yoyote ile duniani haimaanishi Tanzania lazima ishindwe.
Alafu kesi yenyewe ni ya kuomba kuruhusu third party kufanya uchunguzi hata sio kuomba fidia. Watu mnaogopa sana companies za nje, ACACIA wana pesa ndiyo ila a $1 billion dollar company kwa hii age sio scary at all.
Hebu fikiria siku ambayopo uchunguzi huru ukafanyika alafu ikaonekana huu uchunguzi wa kwanza wa mruma ni sawa na project ya research propasal ya saint joseph kwamba haukuwa na vigezi kozi kwingine ni assumption zao tu katika kufanya ukadiriaji. What will be next na huku hisa zao zinashuka katika soko.
 
Mikataba ipi inawabeba, we umeiona? Au umesikia story kutoka kwa mtu ambaye hawezi kuthibitisha. Mikataba haiwabebi kutoa data za uongo, hamna mkataba wa namna hiyo dunia nzima, na hili swala litapelekea mikataba yote kubadilishwa subiri uone.
Ina maana tulisign Mikataba bila kujua kiwango cha madini katika udongo/miamba yetu??? Kma tulifanya tafiti kabla na kugundua zipo kiasi kadhaa na kuithaminisha kiwango cha fedha kinachoendana na mkataba kosa ni la nani?
 
Umeongea kitu cha msingi sana, yani research zote zilizowahi kufanywa kabla zinalingana lingana ila hakuna hata moja inayoreconsile na findings za tume ya prof Mruma.

Yani hizi findings za tume ya prof Mruma ni entirely new revelation!
 
Basi hapo kuna mawili, labda tume ya Prof. Mruma inadanganya kwa sababu zake binafsi labda ufinyu wa vifaa na muda pia (Siku 21 nadhani kama sikosei).

Au feasibility study report iliongopa kwa sababu zake pia ( rushwa ilipita au uharaka na weledi wa mambo haya).
 
Historia imetusogeza katika ukingo wa haki. Mahali ambapo tunapaswa kutoa haki kwa wenye haki, na kupokea haki tunayostahili.
Ikiwa nguvu itahitajika ni sawa, maana historia itakuwa imetusogeza kwenye ukingo wa machafuko na hatuwezi kukwepa!

CCM imetuletea majanga yasiyomithilika.Ndio iliyopitisha sheria za uwekezaji kimuhemuhe. Ndio waliosign mikataba na wazungu kwa siri.
Na kama rasilimali zetu zimeibiwa basi CCM ni mshiriki namba moja kwenye huo wizi.

Tutamlipa Acacia, sio kwasababu ni halali, ila ni haki yake kisheria.
Na CCM hatuwezi kuwaacha hivi hivi hivi, itageuka ni mazoea.Tutamtendea kama mwizi anavyotendewa.
1. Tuitoe madarakani kabla ya kuidhinisha shilingi yoyote kumlipa Acacia.
2. Wahusika wakuu, Mzee Mkapa & co. Tuwafanyie mahakama ya wazi pale uwanja wa taifa.
TUWAHUKUMU WATU KUTOKANA NA MATENDO YAO.

Ndugu zangu, nyakati kama hizi ni adimu sana katika historia.
Ni nyakati za kipekee na zisizofananishwa na nyingine kwa vijana kuonyesha uwepo na uhai wao katika taifa. Vijana lazima waache alama ya kizazi chao katika historia.

Tumekusanya matatizo mengi kama taifa na hii ni fursa ya kuyatatua.
Nyakati kama hizi zinahitaji maamuzi magumu, roho na mioyo iliyo tayari ambayo hutokea mara chache sana katika historia. Lakini zinapotokea huleta mafanikio makubwa sana kutoka katika uwezo wa juu kabisa wa mtu!

CCM OUT!

Nakubaliana na wewe 100% na Kwa waliotayari kufanya kama walivyo Fanya Korea kusini kumuondoa raid madarakani,naomba waniunge mkono tuanzishe movement ya kuiondoa ccm na magufuli wao maana ili ni janga kwetu
 
Lea kweri tushachoka sana mafisadi ni mengi Mno wamefanya. Ipumzike tu 2020.atuna jinsi.
 
Tuipuzishe CCM.Iende ikajiathmini kwanza.Miaka 50 inatosha.
 
Uing'oe CCM uweke nani? Kwani nani hajui CCM iko CHADEMA? Sema tuikatae CHADEMA kwa kuwa imepokea majizi yaliyokataliwa CCM. CCM kwa sasa ni safi wala haihojiki tena mkuu.
CCM haiwezi kukubali kuwa imeiba ng'ombe hata siku moja.
Mkijitahidi sana mnasema mmeiba kamba ila Mwisho wake kulikuwa na ng'ombe.
 
Historia imetusogeza katika ukingo wa haki. Mahali ambapo tunapaswa kutoa haki kwa wenye haki, na kupokea haki tunayostahili.
Ikiwa nguvu itahitajika ni sawa, maana historia itakuwa imetusogeza kwenye ukingo wa machafuko na hatuwezi kukwepa!

CCM imetuletea majanga yasiyomithilika.Ndio iliyopitisha sheria za uwekezaji kimuhemuhe. Ndio waliosign mikataba na wazungu kwa siri.
Na kama rasilimali zetu zimeibiwa basi CCM ni mshiriki namba moja kwenye huo wizi.

Tutamlipa Acacia, sio kwasababu ni halali, ila ni haki yake kisheria.
Na CCM hatuwezi kuwaacha hivi hivi hivi, itageuka ni mazoea.Tutamtendea kama mwizi anavyotendewa.
1. Tuitoe madarakani kabla ya kuidhinisha shilingi yoyote kumlipa Acacia.
2. Wahusika wakuu, Mzee Mkapa & co. Tuwafanyie mahakama ya wazi pale uwanja wa taifa.
TUWAHUKUMU WATU KUTOKANA NA MATENDO YAO.

Ndugu zangu, nyakati kama hizi ni adimu sana katika historia.
Ni nyakati za kipekee na zisizofananishwa na nyingine kwa vijana kuonyesha uwepo na uhai wao katika taifa. Vijana lazima waache alama ya kizazi chao katika historia.

Tumekusanya matatizo mengi kama taifa na hii ni fursa ya kuyatatua.
Nyakati kama hizi zinahitaji maamuzi magumu, roho na mioyo iliyo tayari ambayo hutokea mara chache sana katika historia. Lakini zinapotokea huleta mafanikio makubwa sana kutoka katika uwezo wa juu kabisa wa mtu!

CCM OUT!
Naomba ufafanuzi wako mkuu. Kwani mmiliki wa kampuni za kigeni yeye akivunja masharti ya mkataba huwa hashitakiwi?
 
Naomba ufafanuzi wako mkuu. Kwani mmiliki wa kampuni za kigeni yeye akivunja masharti ya mkataba huwa hashitakiwi?
Anashtakiwa kufuatana na taratibu tulizokubaliana !

Next?
 
Mikataba inawabeba ndio maana mpaka sasa serikali hawagusu hiyo mikataba.
Hiyo mikataba wewe unaifahamu? Mbona mnasema mikataba imewekwa siri sasa umejuaje contents zilizopo kwenye hiyo mikataba wakati mnasema imefanywa siri?
 
COLLECTIVE IMBECILITY
-------------------||-------------------

What Tanzanians mistake?

Parenting goals and plans. We imparted selfish mentalities and ignorance of commonalities.

Partisanship and discrimination based on selfish reasons are the results of non-nationalistic and non- rationalistic parenting.

We imparted to hate and kill ourselves rather than tender, love and care of ourselves.

Social, economic and cultural development won't be there without intellectual mature.

Let's all learn to accept our weaknesses and acknowledge strengths of others.
Sijakuelewa,

Tufanye lugha rahisi!
CCM ni mwizi au sio mwizi?
 
Nilikuwa namuangalia Mbowe akiongea Baraza Kuu la Chadema.

Alipokuwa anaongelea mapungufu ya mambo ya madini kuanzia mwaka '97-'00,Waheshimiwa wawili Sumaye na Lowasa ambao walikuwa kwenye Mkutano huo walikuwa wanaangaliana.

Nadhani kama kuna mtu anayeijua mikataba vizuri ni hawa watu wawili ambao walishanusa hadhi ya Kuwa Makatibu wa Baraza la Mawaziri ambalo Mawaziri huapa kwenye kiapo maneno haya ...."sitatoa siri za Baraza la Mawaziri "....

Picha imekaa vizuri hii.
 
Mikataba ipi inawabeba, we umeiona? Au umesikia story kutoka kwa mtu ambaye hawezi kuthibitisha. Mikataba haiwabebi kutoa data za uongo, hamna mkataba wa namna hiyo dunia nzima, na hili swala litapelekea mikataba yote kubadilishwa subiri uone.
Unajua watu tunazungumzia issue moja lakini kwa style tofauti ya uandishi. Mmoja anatoka nyuma kuja mbele mwingine anaanzia siku ya kwanza kuendelea. Sikiliza; mikataba inasema (Kamanda Lissu anayo nakala ya mmoja wa mikataba hiyo. Lissu aliwahi kushitakiwa kwa uchochezi huko nyuma) eneo la mgodi na madini ni Mali ya mwekezaji. Ndiyo maana mwekezaji anaweza kumzuia hata RC kuingia hadi mwenye Mali aridhie. Serikali haki yake ni 4% ya mauzo. Maana yake kwa kuwa ule mchanga ni sehemu ya madini bado ni mali ya mwekezaji. Tulichotakiwa kufanya ni kusubiri ili tupate hiyo 4%. Mikataba inasema kwa upande wa serikali, kutakuwa na TMAA. Miaka yote hiyo TMAA wapo ndani ya kila mgodi. Serikali ya CCM leo wanadai kuonewa wapi? Watu hamuelewi CCM ni hivi Mimi na wengine inatuuma sana kuibiwa madini rasilimali zetu. Hilo limepigiwa kelele sana huko nyuma mpaka Lissu ameshitakiwa kwa uchochezi kesi imeenda karibu miaka 5, alikuwa anadai k.n.y. sisi watanzania. Nikwambie ndugu yangu katika serikali hii na hata zilizopita hakuna wasichokijua. Juzi mb. Kafumu kaongea, alokuwa kamishina wa madini. Hakuna asiyejua. Ndiyo maana akina LISSU na wengine walipodai mikataba iwe huru serikali ilikataa. CCM walikaa kimyaa. Wabunge wa CCM walikaa kimyaaa. Tena walikuwa wakiwazomea Lissu, Mnyika na wengine kule bungeni. Leo kuna watu humu ndani, kwenye radio, kwenye TV mnapiga kelele na kushangilia kwa lipi geni? Si tangu utawala wa Mkapa na Buzwagi @ Karamagi akina Lissu waliyasema hayo? Walisema mikataba hiyo ina shiiida lakini si serikali na CCM mlikataa? OK what next. Mwanasheria Lissu, Mnyika, na akina Kafulila wanasema; kwa kuwa wawekezaji wanafanya kazi hizo kisheria (mikataba) inabidi utaratibu wa kisheria ufuatwe. Huwezi mtu mmekubaliana madini na mchanga Mali yake halafu wewe unamzuia kuendelea na Mali yake. Inauma lakini ndiyo ukweli ana haki ya kukushitaki. Lisu alisema kabla ya hatua ile ilochukuliwa na Mhe. Rais kwanza tungefuata hatua walizochukua wenzetu waloibiwa kama sisi @ Bolivia. Ukisema hivi unaambiwa eti Lisu anawapenda wawekezaji !! Lakini haya si mliyataka wenyewe mkapiga makofi bungeni, leo kulikoni !!!?
 
kitu ambacho bado sijafahamu ni kwamba tumeibiwa kiasi gani?

maana kimkataba tulipaswa kulipwa 4percent of the value. hivyo kama wali under estimate kwa billion 885 tumepunjwa around 45billion plus may be a penalt. sasa ukizidisha mara miaka 18 hata haifiki trillion moja.

lakini hasara tutakayokuja kuifidia itazidi trillion moja kama tukishindwa kesi huko mbeleni. Kwa niini serikali ya Magufuli isiwaite kwanza uongozi wa kampuni husika ipande opinion yao na hata kuwaruhusu kufanya their independent analysis hata kupitia maabara zile zile walizofanyia serikali kuona je wamefikia same conclussion?
 
Back
Top Bottom