Tutailipa ACACIA, Ila tuing'oe CCM kwanza

Waulize watawala walioweka sheria kuwa kampuni ya kigeni ikiwekeza Tanzania mzawa anatakiwa kumiliki hisa zisizopungua 30%. Baada ya hapo uliza wenye hisa hizo kwenye makampuni ya kigeni ni akina nani? Asilimia kubwa si wafanyabishara tuliowazoea (fedha walitoa wapi)?. Ndipo ujue waliamua kugawana rasilimali zetu. Kwanini 30% isiwe ya serikali. Ni lazima tujikwamue kutoka hapa tulipo, lakini nguvu kubwa na matumaini yetu tusitegemee wanasiasa.
Kwa maisha yalivyo huku vijijini usingetarajia deni kubwa la taifa kutokana na miradi kama barabara za rami, fly over, train na wala sio kilimo cha kisasa au maji safi. Usafirishaji bila cha kusafirisha, tunaishia kuletewa kila kitu kama matahila (mavazi, chakula, mafuta, tooth pick, mitumba,dawa, dola n.k). Tungeanza na kilimo tupate vya kusafirisha, baadae tujenge matrain na ma fly over.
Ukombozi wa maisha bora (kuachana na umaskini wa kutupwa) ndio tunaoutaka na sio ngonjera za amani na utulivu.
Kwa hali ya uchumi ilivyo tayari tumetulia kwa njaa na shida.
Wanajamvi tunahitaji majibu sahihi ya kujikwamua na si sanaa. Watz wanakiu ya maendeleo, hawahitaji utani kama wa yule jamaa aliyesema ataleta "Maisha bora kwa kila mtanzania" Leo katawala miaka 10 na sasa amestaafu muulize maisha aliyotuletea. Viongozi wawe makini na kauli za tamaa bila kuwa na uwezo ya kuzitimiza kwa vitendo. Na siku hizi nazisikia kauli kama hizo kwa staili mpya!

I saliute you all comrades.
 
Mikataba ipi inawabeba, we umeiona? Au umesikia story kutoka kwa mtu ambaye hawezi kuthibitisha. Mikataba haiwabebi kutoa data za uongo, hamna mkataba wa namna hiyo dunia nzima, na hili swala litapelekea mikataba yote kubadilishwa subiri uone.
Mkuu usipaniki. Kwani tulikuwa hatuoni wabunge wakipitisha sheria bungeni? Unaukumbuka ule muswaada wa gesi na mafuta uliopitishwa 2015 siku ile usiku wapinzani wakatoka nje? Huo ndio mfano wa mikataba ya kimangungo inavyopitishwa na wazee wa ndiooooooooooo. Nimekupa mfano rahisi ili uelewe.

CCM OUTTTTTTTTTTTTTTT
 
Wewe una uhakika ACACIA watashinda hiyo kesi? Na je umeiona hiyo mikataba? Kufungua kesi mapema ni lazima maana wameguswa sehemu ya maisha yao.lakini cha pili hiyo CCM tutaitoa kwa namna ipi? Ya kuchukua makapi yanayotemwa huko CCM halafu sisi tunayapokea na kuyapatia bendera kugombea kwetu? Hapo ni sawasawa na kutoa CCM A kuja CCM B,,yaani mtu ahamie Chadema leo na kesho apewe kugombea uraisi tena bila utaratibu maalumu? Bado una ndoto ya kwamba tutaitoa ccm? Na haohao pia walikwepo wakati hiyo mikataba ya unyonyaji inapitishwa ioa walinyamaza kimya,wametukwamisha kwenye katiba mpya,ila kukatwa tu uraisi wakakimbilia huku we bado unaamini watatusaidia kuitoa Ccm?amka mkuu,wanasiasa wasikupelekeshe
Msihamishe magoli. Huyu anayejifanya kupigana sasa hakuwa pamoja na hao mabwana zako unaowataja? Yeye alifanya nini miaka yote hiyo 20 bungeni. Tukubali kama taifa kuna mahali tumekosea tukae chini tujisahihishe siyo kuleta lawama za kijinga ambazo hazina msaada kwa hali tuliyonayo sasa.
 
Wewe una uhakika ACACIA watashinda hiyo kesi? Na je umeiona hiyo mikataba? Kufungua kesi mapema ni lazima maana wameguswa sehemu ya maisha yao.lakini cha pili hiyo CCM tutaitoa kwa namna ipi? Ya kuchukua makapi yanayotemwa huko CCM halafu sisi tunayapokea na kuyapatia bendera kugombea kwetu? Hapo ni sawasawa na kutoa CCM A kuja CCM B,,yaani mtu ahamie Chadema leo na kesho apewe kugombea uraisi tena bila utaratibu maalumu? Bado una ndoto ya kwamba tutaitoa ccm? Na haohao pia walikwepo wakati hiyo mikataba ya unyonyaji inapitishwa ioa walinyamaza kimya,wametukwamisha kwenye katiba mpya,ila kukatwa tu uraisi wakakimbilia huku we bado unaamini watatusaidia kuitoa Ccm?amka mkuu,wanasiasa wasikupelekeshe
Hapa lengo ni kupata mpinzani atakaye leta chachu za maandeleo ya taifa letu,na siku zote mpinzani mzuri ni yule anayekujua nje na ndani. Maana yangu ni hivi hakuna mpinzani mzuri na atakaye tela changamoto za kimaendeleo kama CCM, hiki chama kinabidi kisivunjike bali inabidi kiwe chama cha kipinzani hapo ndipo tutaona umuhimu wa CCM kama ifuatavyo

1.Kwanza viongozi wa ccm wataacha kuwa wanafiki. Kwa mantiki hiyo watu wenye elimu zao ambao watakua ni wabunge 2020 wataishauli vizuri serikali teule. Lakin kwa sasa hawafanyi hivyo kwa sababu hawana uhuru wa kufanya hivyo. Hiki chama kina maprof na watu wenye phd kibao lakin kwa sasa wanazidi wa Lisu kutokana kufanya kazi kinafiki na kiuoga bila na kusababisha kushindwa kutoa ushauri nzuri kwa serikali yetu.

2.Hiki chama cha kipinza tarajiwa kinajua ni wapi waliteleza na wajua madudu yote walio liletea taifa hili mpaka sasa kuliko chama chochote cha kipinzani wanavyo dhani wanajua madudu ya ccm. Kwa hiyo wakiwa wapinzani watakipa mikimiki chama tawala(chadema) zaidi tunavyo ona lisu anavyo fanya kwa sasa kwa sababu wana akina lisu wanafikia mia hivi huko ccm lakin wameamua kua mazezeta wa muda ili kurifurahisha tumbo. Lakin wakiwa wapinzani bungeni watafanya kila njia kuikosoa serikali ya chama tawala wakitumia uzoefu wao ambao walikua hawautumii ipasavyo ili waweze kurejea magogoni 2025 na hapo ndio utamuona mpinzani harisi kwa maendeleo ya taifa letu.
 
Zungusha mikono Sasa!!mabadiliko .....lowasa .....lowasa mabadiliko!!!
 
Hivi aliyewaambia ACACIA watashinda kesi ni nani? Mbona watanzania hamjiamini, kesi kufunguliwa London au sehemu nyingine yoyote ile duniani haimaanishi Tanzania lazima ishindwe.
Alafu kesi yenyewe ni ya kuomba kuruhusu third party kufanya uchunguzi hata sio kuomba fidia. Watu mnaogopa sana companies za nje, ACACIA wana pesa ndiyo ila a $1 billion dollar company kwa hii age sio scary at all.
Hapa hoja ni Kuking'oa Chama Cha Majambazi madarakani kwa namna yoyote wacha kujivua ufahamu
 
mwendelezo wa siasa za matukio. hili jambo magufuli kaamua kulifanya, kama hamuwez kumuunga mkono, mwacheni atekereze hadi mwisho. acheni kudandia mambo na kutake advantage kisiasa. watz wa sasa wanajitambua, tunataka kiongoz bora na sio chama. kama tatizo ni chama, mbona waliosaini mikataba sasa wapo chadema? akina sumaye, lowasa nk.
 
Huyu mtu kaliingizia taifa hasara na anaendelea kufanya hivyo kwa mihemuko ya kick
 
Uing'oe CCM uweke nani? Kwani nani hajui CCM iko CHADEMA? Sema tuikatae CHADEMA kwa kuwa imepokea majizi yaliyokataliwa CCM. CCM kwa sasa ni safi wala haihojiki tena mkuu.
 
Kuing'oa mara ngapi
Mku si unaina wanazidi kukimbizwa mijini.
 
hapa itabidi raisi iweke uchama pembeni wanasheria watakaopelekwa wawe type ya kina lisu maana tunaweza lizwa kama yule jamaa wa gazeti alivyotuliza
 
Historia imetusogeza katika ukingo wa haki. Mahali ambapo tunapaswa kutoa haki kwa wenye haki, na kupokea haki tunayostahili.
Ikiwa nguvu itahitajika ni sawa, maana historia itakuwa imetusogeza kwenye ukingo wa machafuko na hatuwezi kukwepa!

CCM imetuletea majanga yasiyomithilika.Ndio iliyopitisha sheria za uwekezaji kimuhemuhe. Ndio waliosign mikataba na wazungu kwa siri.
Na kama rasilimali zetu zimeibiwa basi CCM ni mshiriki namba moja kwenye huo wizi.

Tutamlipa Acacia, sio kwasababu ni halali, ila ni haki yake kisheria.
Na CCM hatuwezi kuwaacha hivi hivi hivi, itageuka ni mazoea.Tutamtendea kama mwizi anavyotendewa.
1. Tuitoe madarakani kabla ya kuidhinisha shilingi yoyote kumlipa Acacia.
2. Wahusika wakuu, Mzee Mkapa & co. Tuwafanyie mahakama ya wazi pale uwanja wa taifa.
TUWAHUKUMU WATU KUTOKANA NA MATENDO YAO.

Ndugu zangu, nyakati kama hizi ni adimu sana katika historia.
Ni nyakati za kipekee na zisizofananishwa na nyingine kwa vijana kuonyesha uwepo na uhai wao katika taifa. Vijana lazima waache alama ya kizazi chao katika historia.

Tumekusanya matatizo mengi kama taifa na hii ni fursa ya kuyatatua.
Nyakati kama hizi zinahitaji maamuzi magumu, roho na mioyo iliyo tayari ambayo hutokea mara chache sana katika historia. Lakini zinapotokea huleta mafanikio makubwa sana kutoka katika uwezo wa juu kabisa wa mtu!

CCM OUT!
Utakuwa umevimbiwa ili tumpe nani sasa
 
Hakuna jipya kwenye maelezo yako
Tuing'oe CCM halafu tumuweke nani?
 
Tukikuchunguza we mwenyewe utakuta familia yako inapaswa kukushitaki hadhalani na kukukimbiza usirudi tena
 
Back
Top Bottom