Tutahakikisha tunawaua ndani ya wiki moja

Tutahakikisha tunawaua ndani ya wiki moja

Mimi naamini hawa wanaoua polisi sio majambazi maana majambazi nia yao ni kuiba watajirike. Wala si magaidi maana magaidi wasingelenga kuua polisi tu. Mimi nadhani ni walipa visasi wenye uzoefu sana katika mambo ya vita. Kama ndivyo, kwa namna polisi wanavyoshughulikia jambo hili, hao wauaji, wataendelea kupeta na kuzidi kuua. Haiwezekani wauaji wenye weledi mkubwa hivyo kivita wawe na maficho yao mahali pamoja na waendelee kukaa hapo baada ya kufanya tukio baya. Mimi naamini kwa asilimia kubwa kwamba hata kama waliouawa na polisi ni majambazi lakini sio wale waliowaua askari wale wanane.
 
Habari ya Pasaka wana jamvi wa jf.
Baada ya salam nina machache yananipa mashaka juu ya weledi kiutendaji wa jeshi latu la polisi.

Kwanza nalaani vitendo vya mauaji ya askari wetu kwa namna yoyote tukio hili si la kuungwa mkono.

Aidha napenda kutoa mashaka niliyonayo juu ya utendaji wa jeshi letu hasa ikitokea jeshi hili linapo vamiwa na kuuwawa kwa askari wake na hatua wanazozichukua.

Ikumbukwe hili si tukio la kwanza, na kwa taarifa tunazozipata huko pwani si kwa mchezo maana kkosi cha kupambana na ugaidi kiliwahi kwenda, lakin kazi ni ngumu na roho mkononi.

Lakini nimestushwa na kauli ya kamishna Marijan kua washawaua watano kati yao na watahakikisha wanao km idadi ya askari waliouwa au zaidi.

Najiuliza je polisi kusema watawaua ni kuchukua sheria mkononi? Je hao watakaouliwa tuna uthibitisho gani kua ndio wahusika? Kwann polisi wasiseme tutawatia nguvuni na sheria ifate mkondo wake? Ikiwa watauawawa tu serikali itajuaje mzizi wa kundi hili? Na km njia ni kuwaua kwann mpaka leo bado wapo na wanasunbua?

Mimi hua napatwa na mashaka na jeshi letu pale linapotaka kucheza sinema kujivika uhusika wa stering kua lazma lishinde na liwaoneshe watu kua limeshinda.

Ikiwa hii ndio dhana basi upo uwezekano mkubwa sana wa wahusika wa matukio hawapatikani km inavyodaiwa.

Kilipovamiwa kituo cha staki shari. Jeshi siku ya pili likituonesha silaha zilizo ibiwa.

Tukio hili pia baadhubya silaha zikizoibiwa znadaiwa kuonekana. Sikatai inawezekana. Lakini nina mashaka kua jeshi letu linataka kuwaaminisha umma kua wale majambazi si lolote si chichote tumewaua na silaha zetu zimerudi. Jeshi limetangaza vita, nadhan hapa ni mahala pa kupaangalia sana, isije watu wasio na hatia wakatolewa kafara kwa mazingira waliokuwepo, maana hata kama mtu atauwawa na polisi kwa kuhisiwa atajumuishwa ktk ujambazi hakuna namna.

Nafahamu ktk mapambano majambazi hufa, lakini kwa mazingira ya tukii hili, inaingia akikini watu wafanye tukio kubwa km hili na wabaki walipo wasubiri dola wakati wanajua dola ni kubwa na hawazezi kushindana nayo? Kwann tusiletewe watu hawa tuwaone mahakamani wakihukumiwa kwa makosa yao?

Namalizia kwa kusema nina mashaka na utendaji wa jeshi letu sababu linachotaka kufanya ni kiwaonesha wananchi kua limewaua wahusika wakt hilo sio lengo.
Kwann jeshi letu halijawahi kukubali kua walioondoka na silaha hawajapatikana? Sijui km nimejieleza nikaeleweka lakini mashaka yangu isije tukawatoa kafara wasio na hatia kujipa credit kua tumewashinda halafu tukikaa tena kidogo tukio lingine linakuja. Sidhani kwa ukubwa wa tukio hili na lile la staki shari mtu aje kuniaminisha kua hawa watu ni wakawaida. They got skills in that field sasa kirahisi tu eti wameuawawa napata shida hapo.

Mwisho. Namuomba Mungu isitoke roho ya mtu asie na hatia akaacha majonzi kwa familia na ndugu. Akawa miongoni mwa waliodhulumiwa nafsi, jeshi letu kuweni waadilifu ktk hili hata km mnauchungu basi toeni roho za waalifubwa kweli, msimkute mtu anajikatia mkaa porini mnamimina risasi mnamuweka ktk orodha. Mungu ipusha najua haya mambo yapo jamani usiombe yakukute upoteze ndugu asie na hatia uchungu ni mkubwa sana.

Mwisho TULAANI MAUAJI YA ASKARI, UTEKAJI, UVAMIZI WA STUDIO ZA HABARI NA MZIKI. NA UNYANYASAJI WA AINA YOYOTE KWA MTANZANIA YEYOTE. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Mbona nilisikiliza ile hotuba mwanzo mwisho sijasikia iyo kauli.

Ungeambatanisha hako ka clip ili tusikie
 
Siku baba yako akipigwa risasi na majambazi kisha akafa ndo utakuja kujua kwa nini hawa Jamaa wanahisira kiasi hicho.
Unajua mwananchi anatoa hoja kama hii kama mtu mwenye hakili timamu vile, wakati kibaka akimpora sim tu ye ndo wakwaza kusogeza taili. Labda nikuulize kitu mtoa mada, mkilikamata jambazi mtaani kwenu hamtalichima moto? Acheni siasa kwenye watu kama hawa majambazi, anga zao hawanaga huruma kabisa yani:
 
Ndio maana hii kituhaitaisha. Polisi wanaenda ua hovyo halafu wanatuaminisha kuwa ndiyo yale majambazi. Cha ajabu wao wanakimbilia kuua tu kwa nini? Tujue kwamba wanawaua ili wasiseme tunachotakiwa kusikia? Kuna kitu polisi wanajua wanatuficha?????
Je na wewe unakijua hicho kitu?
 
Mtoa mada ni mjinga na huwezi kutufanya sote humu mapunguani. Narudia tena wewe ni mjinga. Hoja yako haina maana yoyote maana pembe uloegemea inaonekana kabisaa huwapendi polisi na uko upande wa hao majambazi, narudia tena wewe ni mjinga. Wewe ni nani uifundishe polisi kazi yake. Mkishavikwa vi beji vyenu msituni vya sjui redi brigedi na kupiga vi pushapu vitatu mnajiona mnafahamu saana mambo ya kiusalama. Tueleze basi mjinga wewe yalipo hayo majambazi maana yaonesha wewe ni mmoja wao, huwezi sema jeshi linafanya usanii mjinga wewe watu hawalali usiku kucha kwa ajili ya usalama wako. Unafikiri Marekani hawakujua mambo ya sheria dhidi ya Osama? Ngoja niishie hapa nisipate ban
 
Siku baba yako akipigwa risasi na majambazi kisha akafa ndo utakuja kujua kwa nini hawa Jamaa wanahisira kiasi hicho.
Unajua mwananchi anatoa hoja kama hii kama mtu mwenye hakili timamu vile, wakati kibaka akimpora sim tu ye ndo wakwaza kusogeza taili. Labda nikuulize kitu mtoa mada, mkilikamata jambazi mtaani kwenu hamtalichima moto? Acheni siasa kwenye watu kama hawa majambazi, anga zao hawanaga huruma kabisa yani:
Mkuu nashkuru maana umegusa katika mambo ninayoishi, mwaka jana nilinusuru kuuwawa kwa kijana mwenye umri wa miaka 17 4m three.alikua na wenzie waliiba simu na akatiwa nguvuni ikikua usiku km saa 5. Nilikuta anachezea kichapo watu wanaandaa mafuta wamchome. Moyo wangu haukukubali niliingia, watu wa mtaani wananifahamu na wananiheshimu pia, wapo walio thubutu hata kunipiga mm rungu za mikono ili nimuache lakin nilijua nawaambia wote nawajua na huyu kijana akifa wote mtawajibika.

Watu walikua wananilaumu na kuniambia nina huruma na vibaka. Lakin mm sikujali nilihakikisha naokoa maisha yake. Kwa hshima nikionayo mtaani ilibidi watu waogope. Nikamchukua yule kijana huku watu wanapiga magongo mpaka kwao nikawaona wazazi wake, nikawaambia nampeleka kituoni ila hakikisheni wwnzake wanarudisha simu.

Nilimfikisha kituoni na kuandika maelezo, na aliebiwa akatoa maelezo. Yule kijana alikua ananiambua "mjomba uhai wako upo mikononi mwako nisaidie" nikamwambia acha wizi. Leo ikikua siku yako lakin shukuru Mungu. Alipoingua celo aliniamia huku analia kua mjomba mungu akulipe nakushukuru sana.

Nimekupa hadithi hii ya kweli ili ufahamu tu kua kuna vitu sisi wengine tunaviishi. Imagine huyu kijana angepoteza uhai kwa simu?

Kuhusu mauaji ya polisi, sote tunakemea, ila tunaomba polisi wasiwatoe watu wasio na atia muhanga. Ijitahidi kuhakikisha wanaouwawa ni wahusika na si vinginevyo.
 
Kiufupi wenzio wamelewa damu wewe unahisia hivi ila uko chumbani kwako
 
Kweli maamuzi siyo sahihi sana lkn na sisi tuache kujichukulia sheria mkonini za kuwaua askar wakati si ndo wenye matatzo me c dhan km ackar anaweza kukutia nguvun km huna hatia
wameua askari wetu kusiwe na huruma. hawana adabu
 
Mkuu alipendekeza kuwa polisi waanze utaratibu wa kwenda na majambazi wanayoyakamata ili yakaonyeshe maficho yao silaha zilipo. Nadhani nilimwelewa vizuri ila sijui kama hao nao walimwelewa!
 
Polisi hawatikiwi kuvunja sheria sababu wao ndiimo wasimiaji wa sheria isivunjwe, ilitakiwa wakamate waliovunja sheria na si lutangaza kuwaua kana kwamba washahuku. Maana ya mahakama ni kuthibitisha anaetuhumiwa ni kweli ndie ametenda kosa sasa hao wanauliwa nani kathibitisha ni wahusika na kwannn waamue kiwaua wanaficha nn? Hata wakiwaua watakua wamearudisha wenzao waliokufa? Mkuu kuna utofauti kati ya askari na mhalifu hivyo haitakiwi askaei nae afanye km alivuofanya mhalifu ni kinyume cha sheria.
Sio awamu hiii
 
Tatizo wanaouwawa ndio wahusika? Mtu afanye tukio kubwa halafu akae hapo hapo awasubiri mje kumuua?

Mkuu;
Kule kwetu kwa kinyamwezi cha kwetu wanasema; The dead stay dumb. Yaani maiti hasemi. Hivyo, hawataweza (Hao maiti) kusema kuwa wameonewa au walitendwa vilivyo stahiki kwao.
Maombi nitakayoomba kwa Kamishna, Chonde chonde baba, tego la panya lisije ingia hata wasokuwemo. Pia, kama ni jambazi kweli, lionesheni jamani tulijue. Mbona Polisi wetu mliwaonesha??
 
Back
Top Bottom