Baba Adele
JF-Expert Member
- Mar 21, 2017
- 208
- 229
Habari ya Pasaka wana jamvi wa jf.
Baada ya salam nina machache yananipa mashaka juu ya weledi kiutendaji wa jeshi latu la polisi.
Kwanza nalaani vitendo vya mauaji ya askari wetu kwa namna yoyote tukio hili si la kuungwa mkono.
Aidha napenda kutoa mashaka niliyonayo juu ya utendaji wa jeshi letu hasa ikitokea jeshi hili linapo vamiwa na kuuwawa kwa askari wake na hatua wanazozichukua.
Ikumbukwe hili si tukio la kwanza, na kwa taarifa tunazozipata huko pwani si kwa mchezo maana kkosi cha kupambana na ugaidi kiliwahi kwenda, lakin kazi ni ngumu na roho mkononi.
Lakini nimestushwa na kauli ya kamishna Marijan kua washawaua watano kati yao na watahakikisha wanao km idadi ya askari waliouwa au zaidi.
Najiuliza je polisi kusema watawaua ni kuchukua sheria mkononi? Je hao watakaouliwa tuna uthibitisho gani kua ndio wahusika? Kwann polisi wasiseme tutawatia nguvuni na sheria ifate mkondo wake? Ikiwa watauawawa tu serikali itajuaje mzizi wa kundi hili? Na km njia ni kuwaua kwann mpaka leo bado wapo na wanasunbua?
Mimi hua napatwa na mashaka na jeshi letu pale linapotaka kucheza sinema kujivika uhusika wa stering kua lazma lishinde na liwaoneshe watu kua limeshinda.
Ikiwa hii ndio dhana basi upo uwezekano mkubwa sana wa wahusika wa matukio hawapatikani km inavyodaiwa.
Kilipovamiwa kituo cha staki shari. Jeshi siku ya pili likituonesha silaha zilizo ibiwa.
Tukio hili pia baadhubya silaha zikizoibiwa znadaiwa kuonekana. Sikatai inawezekana. Lakini nina mashaka kua jeshi letu linataka kuwaaminisha umma kua wale majambazi si lolote si chichote tumewaua na silaha zetu zimerudi. Jeshi limetangaza vita, nadhan hapa ni mahala pa kupaangalia sana, isije watu wasio na hatia wakatolewa kafara kwa mazingira waliokuwepo, maana hata kama mtu atauwawa na polisi kwa kuhisiwa atajumuishwa ktk ujambazi hakuna namna.
Nafahamu ktk mapambano majambazi hufa, lakini kwa mazingira ya tukii hili, inaingia akikini watu wafanye tukio kubwa km hili na wabaki walipo wasubiri dola wakati wanajua dola ni kubwa na hawazezi kushindana nayo? Kwann tusiletewe watu hawa tuwaone mahakamani wakihukumiwa kwa makosa yao?
Namalizia kwa kusema nina mashaka na utendaji wa jeshi letu sababu linachotaka kufanya ni kiwaonesha wananchi kua limewaua wahusika wakt hilo sio lengo.
Kwann jeshi letu halijawahi kukubali kua walioondoka na silaha hawajapatikana? Sijui km nimejieleza nikaeleweka lakini mashaka yangu isije tukawatoa kafara wasio na hatia kujipa credit kua tumewashinda halafu tukikaa tena kidogo tukio lingine linakuja. Sidhani kwa ukubwa wa tukio hili na lile la staki shari mtu aje kuniaminisha kua hawa watu ni wakawaida. They got skills in that field sasa kirahisi tu eti wameuawawa napata shida hapo.
Mwisho. Namuomba Mungu isitoke roho ya mtu asie na hatia akaacha majonzi kwa familia na ndugu. Akawa miongoni mwa waliodhulumiwa nafsi, jeshi letu kuweni waadilifu ktk hili hata km mnauchungu basi toeni roho za waalifubwa kweli, msimkute mtu anajikatia mkaa porini mnamimina risasi mnamuweka ktk orodha. Mungu ipusha najua haya mambo yapo jamani usiombe yakukute upoteze ndugu asie na hatia uchungu ni mkubwa sana.
Mwisho TULAANI MAUAJI YA ASKARI, UTEKAJI, UVAMIZI WA STUDIO ZA HABARI NA MZIKI. NA UNYANYASAJI WA AINA YOYOTE KWA MTANZANIA YEYOTE. MUNGU IBARIKI TANZANIA.