Tutafute projects zisizokuwa za gharama kubwa

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Hello wana JF,

Mie naona kila kijiji kupewa million 50 kwa ajili ya maendeleo na serikali was not realistic na serikali iko embarassed by it.....

Sasa tutafute ideas za project ambazo kila kijiji kitafanya kwa budget ndogo kutoka serikalini??? Labda serikali ina uwezo wa milioni 20 badala ya 50 can we work on this small budget?

Nimeleta wana JF tushirikishane kipi kifanyike kilete maendeleo vijiini.

Thank you,

Becky.
 
Mi nilipenda kama angalau kila kijiji kingepewa trekta. Gharama za uendeshaji wanakijiji wangejigharamia. Hili lingesaidia hata ktk hili wanalohubiri la 'viwanda'.

Mkuu nimependa wazo la trekta,ngoja tuone wengine wanasema nini...
 
Naona wakopesha pesa mnapiga kampeni tusipewe hiyo pesa. Mi nasema hivi, serikali itupe pesa yetu tukopeshane (ahadi ni deni)!
 
Mi nilipenda kama angalau kila kijiji kingepewa trekta. Gharama za uendeshaji wanakijiji wangejigharamia. Hili lingesaidia hata ktk hili wanalohubiri la 'viwanda'.

Wazo zuri sana, trekta, mbolea na Mtaalamu wa kuwafundisha irrigation system na mwingine kuwatafutia soko lenye uhakika wa kuuza bidhaa zao ndani au hata la nje ya nchi. Hata serikali inaweza kununua au mazao yao na baadaye kuyauza kwa watu binafsi.

Iwe kazi ya serikali yetu kutafuta masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi. Kwa kifupi kuwafundisha wakulima wetu kulima kwa kisasa vijiji vyote Tanzania.
 
Vijiji vinatofautiana kulingana na mazingira, nadhani si kila kijiji kinahitaji trekta, kwa vile vyenye mahitaji ya trekta, huu ni mradi mzuri ukisimamiwa vyema. Pia, huwa nawaza yale maji ambayo hutiririka ktk vipindi vya mvua nyingi, hupotelea tu kusikojulikana, kila kijiji chenye nafasi, kingejengewa bwawa la kuyahifadhi haya maji, yatumike kwa ufugaji wa samaki na kilimo cha bustani za mbogamboga ktk msimu wa kiangazi.
 
Wazo zuri sana, trekta, mbolea na Mtaalamu wa kuwafundisha irrigation system na mwingine kuwatafutia soko lenye uhakika wa kuuza bidhaa zao ndani au hata la nje ya nchi. Hata serikali inaweza kununua au mazao yao na baadaye kuyauza kwa watu binafsi.

Iwe kazi ya serikali yetu kutafuta masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi. Kwa kifupi kuwafundisha wakulima wetu kulima kwa kisasa vijiji vyote Tanzania.
Shukrani mkuu kwa indepth analysis
 
Hayo ya tractor wengi yaliwashinda mengine ni scrap mpaka sasa
Mwanzo wanayapokea lakini baada ya kuharika kidogo na uuzaji wa matairi unaanza.
Nafikiri bora tungeweza hata kuwapa Maji salama kila kijiji
Kuhakikisha kina mama hawatembea maili nyingi kutafuta maji
 
Shukrani mkuu kwa indepth analysis

Mkuu kila binadamu lazima ale chakula na tuna ardhi yenye rutuba ya kutosha. 80% ya watu wetu ni wakulima, we have got tremendous assets we should use it well. Tunaweza kulisha Africa nzima na nusu ya Bara la Asia.

Yaani tuwe na watu wetu au mabalozi wetu kwenye nchi kama China, India, Russia, USA, EU, Australia, Nigeria, South Africa etc kutafuta masoko kwa bidhaa zetu na kuwaalika wawekezaji walete tractors zao, mbolea na irrigation systems kwa bei nafuu. Tunaweza kununua kwa wingi halafu tukalipa kwa miaka kadhaa kama 5 mitano hivi. Inabidi tujipange vizuri.
 
Hayo ya tractor wengi yaliwashinda mengine ni scrap mpaka sasa
Mwanzo wanayapokea lakini baada ya kuharika kidogo na uuzaji wa matairi unaanza.
Nafikiri bora tungeweza hata kuwapa Maji salama kila kijiji
Kuhakikisha kina mama hawatembea maili nyingi kutafuta maji
Walishindwa usimamizi, sasa itabidi usimamizi imara uwepo. Kushindwa kwao isiwe sababu ya kulizika jambo hilo.
 
Hayo ya tractor wengi yaliwashinda mengine ni scrap mpaka sasa
Mwanzo wanayapokea lakini baada ya kuharika kidogo na uuzaji wa matairi unaanza.
Nafikiri bora tungeweza hata kuwapa Maji salama kila kijiji
Kuhakikisha kina mama hawatembea maili nyingi kutafuta maji
Kila jambo linawezekana kama kutakuwa na usimamizi mzuri na kuwekwa onyo ikitokea mmeharibu afu kukawa hakuna matengenezo hatua za kisheria zihusike
 
Hayo ya tractor wengi yaliwashinda mengine ni scrap mpaka sasa
Mwanzo wanayapokea lakini baada ya kuharika kidogo na uuzaji wa matairi unaanza.
Nafikiri bora tungeweza hata kuwapa Maji salama kila kijiji
Kuhakikisha kina mama hawatembea maili nyingi kutafuta maji

Tukiyanunua contract ni yao repair ni juu yao kama miaka mitano hivi. Pia kuwafundisha vijana wetu jinsi ya kurepair hizo tractors.
 
Mkuu kila binadamu lazima ale chakula na tuna ardhi yenye rutuba ya kutosha. 80% ya watu wetu ni wakulima, we have got tremendous assets we should use it well. Tunaweza kulisha Africa nzima na nusu ya Bara la Asia.

Yaani tuwe na watu wetu au mabalozi wetu kwenye nchi kama China, India, Russia, USA, EU, Australia, Nigeria, South Africa etc kutafuta masoko kwa bidhaa zetu na kuwaalika wawekezaji walete tractors zao, mbolea na irrigation kwa bei nafuu. Tunaweza kununua kwa wingi halafu tukalipa kwa miaka kadhaa kama 5 mitano hivi. Inabidi tujipange vizuri.
Kura za heshima . hii ndiyo italeta tija kuboost uchumi wetu kwa kufanya export nying na italeta pia tia kuja kwenye uhalisia wa mapinduzi ya viwanda maana malighafi zitakuwepo na nguvu kazi ipo pia
 
Back
Top Bottom