Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,479
- 40,120
Wengi wetu tumekulia katika nyumba ambazo wazazi wote wawili walidumu katika mahusiano ya ndoa daima dumu. Ingawa kulikuwepo na vijistereotype behaviors kati ya mmoja wa wazazi hasa upande wa baba kuwa na mwelekeo wa mahusiano nje ya mama zetu. Lakini ndoa zilidumu daima.Tumeshuhudia mara nyingine kama si mara nyingi mama zetu wakiwa inferior mbele za baba zetu lakini ndoa zilidumu,Familia nyingi ziilikuwa na steps sons and daughters lacuna nod zilidumu
Mara nyingi kama si zote ndugu wa upande wa baba walijitahidi kutawala nyumba za wazazi wetu hasa kumkandamiza mama zetu lakini ndoa zilidumu.Nyingi za harusi za wazazi wetu hazikuwa za mbwembwe na classic kama zilivyo leo, ndoa zilifungwa kanisani kisha watu walitembea kwa miguu kurudi home huku kukiandaliwa ubeche (punje) nyumbani na kumbi zilikuwa ni makuti yaliyozungushiwa uani na kila mtu alialikwa kusheherekea muunganiko huo.
Maajabu ya leo ni kuwa mambo yamebadilika, Wakati wazazi wetu walichangiwa pesa na zawadi za kuanza maisha, sisi tunachangiwa mamilion ya kuteketeza one eve night ya reception. Kipindi hiki michango ya harusi imekuwa ni balaa, tunachangishwa mihela ambayo matumizi yake in a day ni tofauti kabisa na fedha ichangwayo. Sherehe karibuni zote zinafanyikia ukumbini na si nyumbani tena, waalikwa ni maalum tena ulinzi ni mkali.
Kumekuwa na figisu figisu kwenye tasnia ya ndo yenyewe. Kwani inaonekana kadiri harusi inavyokuwa na gharama na mbwembwe nyingi ndivyo inavyokuwa determined kukaa kwa muda mfupi kwani wanandoa wa siku hizi kuachana na kutalikiana ni kama ilivyo rahisi kuhamisha mtoto shule.
Nini kimejiri? Nini kinasababisha wanandoa wasisikilizane ama kuheshimiana ndani ya ndoa? Nini kimesababisha usaliti kufikia kiwango cha juu katika ndoa za leo kuliko zamani? Siku hizi mtu aliye ndani ya ndoa anaweza kuokota kabinti akakasomesha hadi kufikia viwango vya juu huku akikamiliki kama mke wake na akampangishia nyumba/ chumba bila wasiwasi. Siku hizi akina mama ndo wanaongoza kuchomoza na viserengeti boyz tena kwa fashion wanatambiana mitaani.
Nini kimepungua wakuu?
Kuna link gani imekosekana hapo kati hadi kufikia taasisi ya ndoa kuparanganyika siku hizi?
Tusake majibu, tuokoe ndoa zetu