Tutafakari kauli hii ya Mbowe

Tutafakari kauli hii ya Mbowe

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
10,310
Reaction score
6,546
Heri ya jumapili wanabodi.

Jana katika shughuli ya kumuaga ndugu Alphonse Mawazo, Ndugu Mbowe alinukuliwa akisema " Tutampeleka Kamanda Mkumbo mahakamani ili ajue gharama ya kumuweka Mwanza Ndugu Lowasa kwa siku 8 ni shilingi ngapi"

Mwisho wa kunukuu:

Nionavyo:
Kumpeleka mahakamani Mkumbo ni kwa ajili ya kupindisha haki ya kiutu ikiwamo ya kuchelewesha mazishi ya ndugu mawazo au ni kwa ajili ya lowasa kukaa mwanza kusubiria mazishi?

Mbona naona kama Lowassa anafanywa mungu mtu? Ilhali haki ilikua haijatendeka kwa mawazo?.......ishu ni Lowasa au Mawazo?

Michango hasi na chanya inakaribishwa..
 
Lowasa akachunge ng'ombe hana tena ishu katika habari.
 
Mpiga dili huyo. Mzee anatafuta njia ya kurudisha loss ya kusaka urais. Na hao wengine Wanamtafuna mzee wa watu mpaka akifilisika anapigwa out kama Dr Slaa.
 
Mpiga dili huyo. Mzee anatafuta njia ya kurudisha loss ya kusaka urais. Na hao wengine Wanamtafuna mzee wa watu mpaka akifilisika anapigwa out kama Dr Slaa.

Kwa hiyo kauli ya Mbowe ilijikita zaidi kutafuta hela za lowasa kuliko kumjali marehemu?
 
Anataka kutuhadaa watanzania kwa malengo yake binafis kila mtu anahaki mbele ya sheria kama kila mtu anachofikilia kuwa ni vyema ruksa
 
Na wewe mpeleke Mbowe mahakamani kwa kile unachokilalamikia.
 
Lowasa na Sumaye wanahudumiwa na serikali kwa asilimia kubwa. Uwepo wao kule kwa muda mrefu ni matumizi mengine ya pesa za uma ambayo yangeweza kuepukwa! Ikumbukwe kwamba kwenda kuaga mwili wa kiongozi wa chama chao ni justifiable!
Tunahitaji viongozi wa taasisi za uma wanaotumia common sense. Elimu tu bila common sense ndiyo imefikisha taifa hapa tulipo!
 
Hivi mnaosema Mbowe anataka anataka kumshtaki RPC kama 'dili' mna akili kweli? Mawazo angekuwa rafiki yako halafu ukapigwa mabomu ya machozi ukiwa kwenye maombolezo ya kifo chake ungesema hayo? Kwa vile polisi walizuia mazishi kwa karibu wiki mbili ungekuwa msibani ungeondoka au ungesubiri mazishi? Kama umesubiri mazishi kwa muda wote huo kwa nini usidai gharama zako ilhali mahakama imeshahukumu kwamba amri ya RPC ilikuwa batili?
 
Kwan haujui kwamba edo ni mtaji
 
Me nawashangaa sana UKAWA wanatapatapa sana mpka kutumia misiba kama sehemu ya kujichukulia ujiko! Kwahiyo haiwaumu jamaa kufa ila inawauma Lowasa kukaa mwanza siku 8???
 
Wanamhadaa tu mzee.mbona alikwenda shinyanga kuwaangalia waliooololewa toka shimoni na huko atalipia nani
 
Soma tena habari uielewae siyo lawasa Bali ni garama za kuendelea kuweka mwilo Wa marehu ktk hospoli ya bugando
 
Hiyo ni kauli ya mwanasiasa na imetolewa kisiasa sasa wewe unataka nini? Unafikri kama kamanda Mkumbo angetenda haki Lowassa angepoteza muda wote huo hapo Mwanza?
 
Back
Top Bottom