nilishalizungumzia hili katika thread nyingine some days ago. Ccm inashirikiana na nec (tume ya uchaguzi, lakini pengine hao wanaopita na kukusanya details hawajui kitu gani hasa kinafanyika baada ya wao kuwasilisha ngazi za juu orodha zenye details za wanachama wao.
Nasikiavyo hawa wanaokusanya details hizo huliupwa kati ya 50,000 hadi 100,000 kufuatana na wingi wa majina yanayowasilishwa.
Baadaye hayo majina – na mengine kutoka kila kituo cha uandikishaji (nchi nzima - na hasa sehemu za miji zinazosadikiwa kuwa na wapinzani wengi) hupelekwa nec.
Hizo orodha za majina ya wapiga kura ya wana-ccm yakifika kule makao makuu ya nec, zinatafutwa orodha za majina ya wapiga kura kutoka vituo hivyo na kinachofanyika ni kuyaondoa, (au kuyahamishia kwenda kwenye orodha za majina ya vituo vingine vya mbali), majina yote yale mengine (ambao siyo ya wana-ccm).
Matokeo ya uharamia huu unaofanywa na nec hauwi wa 100 per cent, lakini kwa kiasi kikubwa majina ya wale siyo wana-ccm yanavurugwa, kwa kuondolewa kabisa au kuhamishiwa katika orodha za vituo vingine.
Ndiyo maana kule jimbo la temeke mwaka 2005 majina ya wapiga kura zaidi ya laki moja hayakuonekana katika orodha, wengi wao wakiwa wa vyama vya upinzani na hivyo kushindwa kupiga kura.
In fact mtindo huu wa kuwa-defranchise wapinzani ulianza kutumika hasa 2005, na umeigwa kutoka zimbabwe, ethiopia (katika uchaguzi wao wa 2005 na mwaka huu pia) na kenya (wakati wa moi 1992 na 1997).
Na ndiyo maana ccm haitaki kata kata kuwa na nec huru, au pia kutomuondoa chairman wake, l makame ambaye anazeekea pale – kwani anaridhia hujuma hizo chafu. Nashangaa kwa nini vyama vikuu vya upinzani hawasusii uchaguzi – bila ya wawakilishi wao kuwamo ktk nec.
Haya ninayowaambieni ni kweli kabisa, chunguzeni sana kwa nini ccm inakazania kufanya hivyo.