Tutafakari baadhi ya mada za "Je, tutafika?" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutafakari baadhi ya mada za "Je, tutafika?"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Jun 20, 2009.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Mimi ni mmojawapo wa wapenzi wa kipindi kinachorushwa na Channel 10 kila Jumanne: Je, tutafika? Kipindi hiki huwa kina mada nzuri ingawa mara nyingi ‘animator' anakiharibu, hasa anapozungumza zaidi kuliko wachangia mada. Anakera sana kwa hili na nadhani halijui hilo!

  Pamoja na hoja nzuri zinazojadiliwa na kipindi hiki, linapokuwa ni swala linalohusu dini, ‘animator' wenyewe anakuwa na ‘bias' fulani, ambayo nimeona ni vizuri niiweke wazi. Kati ya mijadala inayohusu mambo ya dini nilishasikiliza miwili.

  Wa kwanza ulihusu MAHAKAMA YA KADHI na wa pili kijitabu kilichoandaliwa na Chirstian Professionals of Tanzania (CPT) na kupitishwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kuhusu MPANGO WA KICHUNGAJI KUELEKEA UCHAGUZI UJAO.

  Katika mijadala yote miwili niliona kuwa ingawa ‘animator' anaonekana akipinga udini lakini yeye mwenyewe ndiye aliyejaa huo udini. Katika mada ya kwanza yeye mwenyewe alionyesha upande aliokuwa akiuunga mkono na hivyo alijaribu kuweka ‘leading questions' kwa wachangiaji ili wachangie kile alichotaka kuhitimisha na kilichohusu: kwa nini maaskofu wanapinga Mahakama ya Kadhi ambayo ni haki ya Waislamu? Kwa uelewa wangu hakuna anayepinga Mahakama ya Kadhi kama itaanzishwa nje ya Katiba kwa vile "Nchi haina dini na mambo yanayohusu imani ni watu wenyewe".

  Katika mada ya pili, alikuwa na ‘tactics' zilizile na ilionekana wazi kuwa anachochea udini zaidi badala ya kuelemisha umma wa Watanzania kuhusu mada yenyewe.

  Mfano, katika mada zote mbili ‘selection' ya wachangiaji haikuonyesha kuwa na uwiano mzuri. Aliwachagua watu wa dini fulani wengi zaidi na wenye uelewa wa dini yao kuliko wale aliowachagua wa dini ya pili na pengine alichagua wale alioona wanamwelekeo anaoutaka.

  Kwa mada ya pili pia alifanya hivyohivyo. Dini moja aliwachagua watu 3 wenye uelewa mzuri wa dini yao na nyingine wawili (mmoja mchungaji Lusekelo) na kati ya hao wawili, mmoja hata hakujua kitu gani cha kuchangia. Na hivyo, baada ya mada yenyewe, hitimisho lilielekea upande mmoja aliotaka huyo ‘animator' umma wa Watanzania ujue ndiyo Maaskofu wa Kanisa Katoliki wana udini na wanahatarisha amani ya nchi yetu kwa kujiingiza kwenye siasa.

  Yaani waraka wao unaowataka watu watumie vizuri haki ya kuchagua viongozi waadilifu na wenye uchungu na nchi yao bila kujali dini, itikadi ya chama au kabila la mtu, yeye anaona hiyo siyo kazi ya madhehebu ya dini. Wachangiaji wote siku hiyo (Jumanne, June 16, 2009) walikuwa na mtazamo huo na ndivyo ‘animator' wa kipindi alivyotaka Watanzania waelewe.

  Lakini mimi huwa najiuliza kama huyu ‘animator' ana nia ya kuelemisha jamii na hana udini, kwa nini huwa hawaaliki, mfano, padri au askofu fulani wa dhehebu husika ili nao waeleze upande wao na kuacha wasikilizaji waamue kulingana na jinsi walivyosikia maelezo yenyewe kuliko yeye kujifanya ndiye anayewaalimua?

  Yeye kama ‘seasoned journalist' nilitegemea awe mtu ‘open' na asiye na udini lakini kwa mada hizo mbili na pia baada ya kusoma ‘articles' zake alizoandika kuhusu hizo mada, niligundua kuwa ana ajenda ya siri na ni mtu aliyejaa udini kuliko anavyonekana anaupinga.

  Katika mada ya pili alisisitiza zaidi kwa nini Kanisa linajiingiza kwenye siasa na kusema kufanya hivyo ni kuhatarisha amani ya nchi. Wachangiaji wengine nao pia walikuwa na maoni hayohayo.

  Of course, inategemea yeye anafahamu nini katika ‘kuchanganya dini na siasa'. Binafsi naamini kuwa mwumini mzuri wa dini atakuwa mwanasiasa mzuri pia na mwanasiasa mzuri akiingia kwenye dini atakuwa mwumini mzuri vilevile. Dini au siasa havimuharibu mtu bali mtu ndiye anayeharibu dini au siasa.

  Mtu mwenye imani nzuri ya dini au mtu mwadilifu lazima atafanya pia siasa yenye uadilifu. Madhehebu ya dini, mfano, yanachangia katika maendeleo ya nchi – ikiwa ni pamoja na siasa (kuhamasisha waumini wao wachague viongozi/wanasiasa waadilifu), huduma za jamii – elimu, afya, etc.

  Ukisema madhehebu ya dini yajiondowe kwenye siasa – yaani yajiondoe kwenye maendeleo ambayo ni siasa, elimu, afya, etc una maana kuwa unataka kuwafuga baadhi ya watu/Watanzania kutokuwa Watanzania halisi. Siasa ya Tanzania ni ya watu wote – wawe wachungaji, mashehe, mapadri au maaskofu au watu wa dini nyingine. Kwa maana hii, siasa na dini zinapaswa zifanye kazi moja ya kukamilishana. Ni kama anayekwea ngazi anashika pande zote mbili kwa wakati mmoja – yaani imani yake inaleta changamoto mwenye siasa na siasa inasaidia imani yake kukua vizuri kwa kuinjengea mazingira ya uhuru wa kutosha wa kuamini na kuabudu. Kufanya hivyo siyo sawa na kuchanganya dini na siasa bali ni kuwajibika kwa imani/mwumini au kiongozi wa dini.

  Kitu kinachokatazwa kufanyika katika madhehebu ya dini ni kuwa na viongozi wa kiroho wanaoshabikia chama kimoja dhidi ya kingine kwa sababu kufanya hivyo kutaleta msukosuko kati ya waumini na wananchi kwa ujumla kwa vile katika dini fulani kuna waumini wa vyama mbalimbali.

  Na dini au dhehebu likishabikia chama kimoja, hapo inakuwa si sahihi. Kwa vyovyote vile kutakuwa na mwingiliano wa kimasilahi na vurugu. Lakini kusema usichanganye dini na siasa – kwa maana ya kusema usichangie kuboresha sisasa ya nchi – yaani maendeleo ya nchi, hapo naona ni kitu kisichoeleweka kabisa.

  Dini zinapaswa kukamilisha sehemu ambazo serikali inashindwa au inafanya kwa kulegalega. Kwa sababu huwezi kusema mchungaji, padri, shehe au askofu achangie maendeleo ya nchi na kumkataza asichangie kuboresha siasa ya nchi yake. Kufanya hivyo ni kumfuga. Sijui ‘huyu seasoned journalist' anaelewa nini kuhusu siasa na wanasiasa.

  Kwa vile kila anayezaliwa ni mwanasiasa, inawezekanaje tuwe na baadhi ya watu wasioruhusiwa kuchangia kuboresha siasa/maendeleo ya nchi yetu au hoja ni kwa vile Kanisa linahamasisha waumini na wananchi kwa ujumla kuhusu kutumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki katika mambo yote yanayohusu maendeleo ya nchi na maendeleo yao wenyewe?

  ‘Civic education' katika Kanisa katoliki haikuanza leo au jana. Ni kitu cha miaka na miaka na ‘animator' wa "Je tutafika?" anaona ‘civic education' haipaswi kufanyika kanisani. Kanisa Katoliki linaamini kuwa imani lazima inonekane katika matendo. Na kuwa na mchakato wa kuwapa waumini uelewa mzuri kuhusu haki zao za msingi sidhani kama ni kazi ya serikali tu. Hii ni kazi ya kila mtu, kila dhehebu la dini na taasisi mbalimbali.
   
  Last edited: Jun 20, 2009
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Maelezo yako pia yamejaa, udini wa upande mmoja.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Aahh yule mzee ni mdini sana na kama ukikaa chini kumsikiliza haukuchukui muda kujua hilo. Hata hivyo ukweli ni kuwa ukitaka kuchagua watu wenye busara wachague wakati wanapojadili mambo ya dini..hapo utapata scale halisi ya uelewa na upeo wa mtu..lol
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jun 20, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Yule mzee Makwaia wa Kuhenga alifanya niache kuangalia kipindi hicho kwa sababu ya jinsi anavyoendesha. Anajaribu sana kutengeneza 'public opinion' kwa kuchagua wale anaoona hawaelewi mambo au wako upande wake. Siku moja alikifanya kipindi hicho kuwa 'live' alianza kupata wachangiaji walioanza kumpinga kuhusu serikali ya awamu ya kwanza. Alidai kwamba taasisi za dini za kiislamu pekee ndio zilizotaifishwa lakini kuna mtu alipiga simu kumpa mifano ya taasisi za dini ya kikristo zilizotaifishwa. Kuanzia wakati huo hakufanya kipindi hicho kuwa 'live' tena! Kama kuna mtu ana simu au email yake aitoe hapa ili tumjulishe mapungufu yake pls!
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jun 20, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama kuna mtu ana email au simu ya 'Patamu hapo!' Makwaia wa Kuhenga atupatie pls!
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ndio hapo jamaa wanapo guswa sipo!
   
Loading...