Tutaendelea kuona tunaibiwa madini hadi tutakapotaka kuelewa biashara yao

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Wakati tunajisifu tunaumeme mwingi Migodi Mingi inatumia mabillion kujihudumia kwa umeme wao binafsi.
-Leo kama tungewapelekea umeme wa uhakika enzi hizo leo wenda wangeisha rudisha gharama zao za uwekejazi na tungefaidi hiyo Kodi tunayosema hawalipi...

Tungejua tutakuwa na mashaka ya uendeshaji wa migodi, tungekubali na sisi kuwekeza mitaji kama taifa angalau asilimia 40 au 50
-hapo na sisi tungekuwa wamiliki na hakuna ambacho wangefanya tusikijue.

Uwekezaji ktk migodi ni uwekejazi wa matrillion inachukua muda mrefu kurudisha mtaji wao ila siku wakilipa kodi ni Sawa ya makodi ya Makampuni lukuki na zaidi ni mabillion ya kodi. Kwa kujua Hilo kabla hatujalaumu ilikuwa ni jukumu letu kufuatilia hatua kwa hatua na leo Tungejua professionally walipata au wanapata faida ili tufurahie mabillion ya kodi zetu yaani cooperate income tax.

Kwa sababu tuliamua kuwaachia wenyewe hiyo kazi wakulaumiwa ni sisi.

Mwaka 1998 tulipaswa kujua kodi ya faida kwa migodi inalipwa kwa muda mrefu lkn ikilipwa ni nyingi mnoo. Tungewekeza kuwahudumia watu wa migodi vifaa, vipuli, nguo za kazi na vifaa vya usalama PPE. Kwao hizi wanatumia mabillioni kuagiza nje ya nchi sisi Tungewekeza hapo na kuweka sera ya kuwataka wafanye local purchasing nchi ingeona faida kubwa ya migodi. KWANZA tungepata soko la viwanda vya ndani, Kemikali ajira, na kukuza uzalishaji huku tukiwapunguzia gharama za uendeshaji faida yake wanarudisha mtaji wao mapema na sisi tunafaidika na kodi yetu mapema.

Note
Pamoja na kutolipa kodi kubwa ya faida
Wanatulipa vikodi vidogovidogo kama
1:Mrabaha 4%
2:Service levy kwenye almashauri migodi ilipo
3:wanawekeza kwenye vimiradi vya kijamii (cooperate social responsibility) tunawaona kwenye TV matangazo yao.
4:Wanaenda mbali hadi kujisifu kwa kodi wanazolipa wafanyakazi wao PAYE kwa sababu Bila uwepo wao zisingepatikana.
5:Kodi wwnazokatwa wakinunua vitu vyao nje ya nchi...
Na vikodi vingine vidogovidogo


Rais akapata wakati mgumu kusimamia na kufuatilia vitu ambayo Misingi ilipaswa kuwekwa mwaka 1998. Sisi wananchi tunaombea juhudi hizi ziwe na miisho mizuri kwa taifa na iishie kuwavutia wawekezaji wengi zaidi.

mitale na midimu
Tuuelewe utajiri wetu ili tuuchote kimaridadi
 
Back
Top Bottom