OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 669
Baada ya kuisoma kwa uzuri tafiti iliyofanywa na wataalamu wa mafuta na gesi Afika, Polus, A na Tycholiz, W nimekuja na review ya kile ambaco kipo kwenye kazi waliyoifanya mwaka 2019 ikiaangazia uwanja wa madini na gesi asilia nchini Tanzania huku wakionesha namna ambayo nchi inapoteza mbali na kuwa na rasilimali nyingi huku wenyewe wakiwa wameona si vyema kutumia msamiati 'Laana ya rasilimali'
Gesi asilia iligundulika nchini Tanzania mwaka 1974 na kampuni ya AGIP na uchimbaji wake ulianza rasmi mwaka 2004 ambapo Benki ya Dunia ilikadiria kuwa gesi asilia itaifaidisha Tanzania na kuwaondoa wati milioni 11 kutoka katika wimbi la umasikini mkubwa. WAkati huo madini yalikuwa yakiendelea kuchimbwa nchini na hakuna faida ya moja kwa moja iliyokuwa inaonekana kwa wananchi juu ya uchimbaji wa madini hayo.
Wasomi waliaoandika kazi hii ya David Versus Goliath: Tanzania's effeorts to stand up to foreign gas corporations hawakuweza kuweka kisa alichowahi kuandika Kamara Kusupa kuhusu Bulyankulu na visa vingine vya wananchi waliokaribu na migodi ambao walinyanyaswa na kupelekea vifo vya watu kadhaa, kama ambavyo mwaka huu kampuni moja ya uchimbaji ililazimika kuwalipa wahanga wa matukio ya kinyanyasaji
JINSI TANZANIA INAVYOLIWA
Imebainika ya kwamba katika makampuni 1700 ya uchimbaji madini na gesi asilia ni 25% tu ndio wanalipa kodi. Hata Royalties zinazolipwa ni ndogo mno ambazo ni 2.3% ya makusanyo yote ya kodi hiyo ni kwa kipindi cha 1998 hadi 2011. Kibiashara ni kawaida kwa watu kusema hawapati faida lakini wasomi hawa wameonesha kampuni tatu kubwa ambazo mmetoka kuingia nazo mkataba zilipata faida ya USB 37.2 Bilioni mwaka 2017 ambapo wakati huo makusanyo ya kodi ya Tanzania kwa ujumla yalikuwa USD bilioni 7.3. Andiko hili linaonesha ubovu wa mikataba iliyokuwepo ambapo ilifanya Tanzania ipoteza kiwango kikubwa cha fedha kama mapato
Kutokana na arguments zilizokuwepo, watu wengi huwa na lawama kwa vyombo hivyo vya nje kutokana na ukubwa wake na ni kweli ni vikubwa kwa kuwa Mitaji ya kampuni kubwa tatu ni mara 16 ya GDP ya Tanzania, hata hivyo watafiti wanasema tatizo lipo ndani ya nchi na sio nguvu ya nje ya kampuni hizo
MZIZI WA FITNA
Leo tunashuhudia mtanange kati ya Waziri wa Nishati January Makamba na Mkurugenzi wa TPDC kuhusu kiwango cha mafuta kilichopo nchini. Japo hii haikuwa sehemu ya hoja za hao wanazuoni lakini wameweka wazi kwamba kutoa wataalamu wa nishati kutoka Wizara ya Nishati kuwapeleka TPDC kuna walakini kwa kuwa TPDC ni mdogo kwa Wizara ya Nishati ambapo inaweka ulazima wa wao kuripoti wizarani na kushindwa kuchukua maamuzi ya kitaalamu yasiyoathiriwa na siasa
Suala lingine ni kuwa na uwezo finyu wa ku-negotiate kwenye mikataba ya madini, ambapo katika hili watafiti hao wamemtaja Magufuli kuwa alijitahidi kuangalia mikataba na ile iliyokuwa na viashiria vya unyonyaji vilifutiwa leseni na kufanya uchangiaji wa mapato kutoka kwenye madini kwa GDP kupanda
Watu wengi walioko madarakani wana woga, kwenye kutoa taarifa, hali inayokuwa changamoto, i.e wanazuoni wameonesha kuwa walipata shida kukutana na wataalamu kutoka Benki Kuu ya Tanzania kwa kuwa hawakutaka kuonge nao wakati wa tafiti yao
Aidha watu wamewaambia watafit kuwa 'Kukalia ofisi ya umma ni njia fupi ya kupata utajiri' bila shaka hii ni akili iliyo kwa wengi ambapo ubadhirifu umekuwa kwa vichwa vya watumishi wa umma badala ya kuweka maslahi mapana ya taifa. Hoja zao zimeandikwa vizuri na wachumi wa maendeleo Smith and Michael Todaro (2014)
NJIA SAHIHI
Njia ambayo watafiti wameshauri katika kazi yao ni kuongeza uwezo wa kupambana na rushwa, kwa kitu ambacho watafiti wamekiita 'Magufuli Effect' kwa kuongeza uwajibikaji na kupitia upya mikataba ya madini na gesi. Aidha tumeona hivi karibuni masuala mengi yaliyoanzishwa na Magufuli kuhusu madini yakikiukwa ikiwemo kuruhusu usafirishaji wa makinikia ambapo Waziri Mkuu alisema nchi inakuwa imeshapata stahiki yake ambayo kimsingi ni dhahania kwa kuwa haujui kiwango cha madini yaliyoko ili kupata kodi stahiki
Hoja zilizoko kwenye kazi hii ni hoja nzito ambazo zinaendana visuri na hoja za Action Aid kwenye kuzidisha wigo wa kupaa kodi bila kuongeza tozo, ushuru nk wakati vipo fedha nyingi ambazo tunaziacha bila kuchukua stahiki, recently ration ya Tax to GDP haizidi 14 ambapo ukusanyaji kodi ukiwa mzuri hasa kwenye sekta ya madini na gesi hesabu za Action Aid zimeonesha Tax to GDP ratio itapanda hadi kufikia 50% ambapo hatutakuwa tena na haja ya kuomba mikopo kutoka nje
Ni muhimu kuzalisha wataalamu wa kutosha wakuitazama vyema mikataba ili kujua namna bora ya kufaidika kutoka kwenye mikataba hiyo
Kaz iliyokuwa Reveiwed ni Polus, A., & Tycholiz, W. (2019). David versus Goliath: Tanzania’s Efforts to Stand Up to Foreign Gas Corporations. Africa Spectrum, 54(1), 61-72.
Signed
OEDIPUS