Na Juddy Ngonyani,Sumbawanga
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kimeangalia upya njia ya kuwadhibiti wafanyabiashara wanaojiunga na chama hicho na kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi ndani ya chama hicho
Akizungumuza katika mkutano wa chama hicho wenye lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu nini maana chama hicho kujivua gamba mkoani Rukwa jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Bw. Nape Nnauye alisema kuwa uamuzi huo unatokana wafanyabishara hao kutumia uwezo walio nao kuendekeza vitendo vya rushwa ilikijipatia uongozi.
Alisema kuwa hiyo ni hatua moja wapo ya chama kujisafisha, huku akibainisha njia zitakazotumika kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho.
Bw. Nnauye alisema kuwa ilifika mahali waanachi wakapoteza imani na chama pamoja na viongozi wake jambo lililofanya chama hicho kurekebisha mambo mengi ikiwemo kutokomeza vitendo vya rushwa ama kwa wagombea na waachama ili kukirudisha chama katika mstari unaotakiwa.
Awali Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini Bw. Aeshy Hillary pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Rukwa Bw. Hipolitus Matete waliipongeza hatua iliyochukuliwa na Halmashauri Kuu Taifa ya kuwaondoa wabadhilifu na wale wasio na maadili mema ndani ya chama hicho.
Hata hivyo Bw. Hillary alitumia nafasi hiyo pia kutoa msaada wa baiskeli kumi kwa baadhi ya walemavu washio katika manispaa hiyo.