Tutadhibiti wafanyabiashara CCM-Nape | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutadhibiti wafanyabiashara CCM-Nape

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 3, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na Juddy Ngonyani,Sumbawanga

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kimeangalia upya njia ya kuwadhibiti wafanyabiashara wanaojiunga na chama hicho na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho

  Akizungumuza katika mkutano wa chama hicho wenye lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu nini maana chama hicho kujivua gamba mkoani Rukwa jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Bw. Nape Nnauye alisema kuwa uamuzi huo unatokana wafanyabishara hao kutumia uwezo walio nao kuendekeza vitendo vya rushwa ilikijipatia uongozi.

  Alisema kuwa hiyo ni hatua moja wapo ya chama kujisafisha, huku akibainisha njia zitakazotumika kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho.

  Bw. Nnauye alisema kuwa ilifika mahali waanachi wakapoteza imani na chama pamoja na viongozi wake jambo lililofanya chama hicho kurekebisha mambo mengi ikiwemo kutokomeza vitendo vya rushwa ama kwa wagombea na waachama ili kukirudisha chama katika mstari unaotakiwa.

  Awali Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini Bw. Aeshy Hillary pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Rukwa Bw. Hipolitus Matete waliipongeza hatua iliyochukuliwa na Halmashauri Kuu Taifa ya kuwaondoa wabadhilifu na wale wasio na maadili mema ndani ya chama hicho.

  Hata hivyo Bw. Hillary alitumia nafasi hiyo pia kutoa msaada wa baiskeli kumi kwa baadhi ya walemavu washio katika manispaa hiyo.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nape matatizo sio wafanya biashara matatizo ni Katiba ya Chama Chemu kijinufaisha ndani kwa ndani MAFIASO

  Nchi nyingi duniani zina wafanyabiashara wakiziongoza na wametenganisha vizuri kabisa biashara na Siasa--- Mfano Waziri Mkuu wa Italy
  Amerika Members of Congress wengi ni wafanyha biashara na wanajua kutenganisha biashara na Siasa
  Hapo kwa jirani zetu wakenya the same thing

  What is needed to be done is a stronger Constitions to safagauard it people... CCM melala kweli
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  May be macho yangu yanaona makengeza hapa
  ni wabadhirifu gani wameondolewa kwenye chama au ile kutamka tuu ndio wameondolewa
   
 4. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Picha za mkutano huo ziko wapi?????????? Au aliongea na watoto wa shule??????????
   
Loading...