Tusitegemee kulala na mashetani na kuamka na malaika

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Ndugu wanaJF Bunge ndilo hilo leo lime vunjwa na kuashiria kuanza kwa kampeni rasmi. Kwa muda wa miezi michache serikali itaongozwa na watendaji wake wa kuajiriwa kwa maana wengi wa viongozi wa kuchagulia aidha wata kuwa bize na kampeni. Kwanzia muda huu mengi yata semwa na ahadi nyingi zita tolewa. 2010 ime wajia ramsi.

Natumai wengi wetu tulioweza tumesha jiandikisha na kujianda kupiga kura mnano Oktoba. Kura moja pekee yake inaweza asi badilishe chochote lakini kwa pamoja kura zetu zina nguvu sana. Kwa maana kura zetu hazita zungumza kwa binafsi yetu bali ita zungumza kwa niaba ya Watanzania kama kikundi chenye umoja na kutafuta maendeleo ya wote.

Nawa sihi Watanzania wote wasi poteze haki zao za kupiga kura. Najua wengi wata kuwa wame kata tamaa na wengine kuchoshwa. Lakini siku zote maishani yule anayeshinda ni yule anaye tafuta nguvu wakati pumzi ime muisha ili kumalizia kazi. Safari bado ni ndefu lakini ushindi una hitaji uvumilivu na staha.

Kama kuna kitu kimoja nita kacho wasihi wananchi ni kwama wasiuze kura zao. Wapigie kura watu ambao kweli wanadhani kazi na dhamana ya kuwaongoza wataiweza. Kuna tabia ya kuto kupiga kura au kumpigia kura yoyote wengi wetu tuki dhani siasa haituathiri maisha yetu ya kila siku. Kosa kubwa sana. Tusi tegemee kulala na mashetani na tuamke na malaika. Miaka mitano ni michache lakini ni muda wa kutosha kwa mambo mengi makubwa yanayo athiri mustakabali wa taifa kutokea kama tulivyo ona kwenye miaka mitano ya kwanza ya awamu ya nne.

Ndugu zangu Watanzania tume piga kelele kwa miaka mitano na tumeandika na kuanika malalamishi mengi ndani ya muda huu. Tumeongea mpaka wengine pumzi zime tuisha. Tumeandika mpaka wengine mikono imechoka. Tume jadiliana na kugombana lakini sasa muda wa kuongea umeisha na ni wakati wa vitendo. Oktoba ina wajua,, Ndugu wanaJF, ndugu Watanzania ni muda wa kuwa mabadiliko ambayo tume kuwa tuki lilia muda wote huu. Ni muda wa kuona kama kweli yote tuliyo kuwa tukiya sema tulimaanisha au tulisema tu kuridhisha kadamnani. Ndugu wananchi 2010 ime wada rasmi. Asubuhi ime kucha na wale mashetani bado leo hii ni mashetani wale wale wa 2005. Tusi tegemee miaka mitano mingine ita wabadilisha.
 
good message that either may fall on dead ears,or on ears of ignorant voter,

ila shime watanzania wakati wa mabadiliko ni sasa,ni vigumu kumtoa JK lakini ni rahisi kutengeneza bunge litakaloishake CCM na JK kwa kuchagua wabunge wengi wa upinzani,wote tunafahamu ni namna gani wabunge wa CCM kwa kutumia wingi wao wamekwamisha au kuharibu mambo mengi ya msingi nchini ,mwetu,wakati wa kulalamika umeisha sasa wakati wa kuact umefika
 
Umenena Mwanafalsafa lakini jee Watanzania wapo tayari kukubali mabadiliko?
 
Back
Top Bottom