Elections 2010 Tusisubiri 2015; Tuanze sasa

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Nimekuwa nikifuatilia maoni ya wanaCHADEMA, humu Jf na hata mitaani, na wengi wanalaani kushindwa uchaguzi wa mwaka huu na kusema tusubiri 2015, CCM itaanguka.

Ninachotaka kuwaasa ndugu zangu, tukisubiri 2015 bila kujipanga vyema, tutakuja kuumbuka hata zaidi ya mwaka huu. Sote tunajua kuwa pamoja na kazi kubwa tuliyoifanya mwaka huu, lakini tumeishia kuibiwa kizembe mno. Ni sawa na mkulima aliyejituma sana kulima, alipovuna akaweka mazao yake stoo asifunge mlango, then akapita kibaka akachukua kiulaini, sasa mkulima analalamika.

Kusemma kweli naweza sema kuwa mwaka huu tulijiandaa kushindwa, sio kushinda. Naweza kutoa mfano wa jimbo nililopo; kwanza hadi wiki 1 kabla ya uchaguzi, hatukuwa na mawakala katika vituo vyote. Tunaenda kwenye kupiga kura, zaidi ya 25% ya vituo hatukuwa na mawakala. nilijaribu kutembelea vituo kadhaa wakati wa zoezi la kupiga kura, nikagundua kuwa mawakala walikuwa wamelkaa mita kadhaa kutoka kwa anayehakiki majina ya wanaopiga kura; wakala hana karatasi wala orodha ya waliotakiwa kupiga kura pale. Hali kadhalika, katika vituo vingi nilona mpangilio ni kuwa tokea mtu angeweza kupewa karatasi ya kupigia kura, akapiga na kuweka kwenye box, akiwa amemgeuzia wakala mgongo wakati wote,kwa maana kwamba hata angekuwa anapiga kura zaidi ya moja asingeonwa.

Jioni ilipofika, zoezi lakuhesabu kura lilipoingia ndio lilikuwa kichekesho. Kwanza, bila sababu za maana masanduku yalikuwa yanahamishwa kutoka kituo kimoja hadi kingine kabla hayajahesabiwa, eti kwenda sehemu zenye taa! Hakuna wakala aliyekuwa anahoji. Baada ya zoezi lakuhesabu mawakala walikuwa wanatia saini kwenye karatasi za matokeo ambayo yalikuwa yameandikwa loosely kiasi kwamba nakala waliyokuwa wanapewa baadhi ya mawakala ilikuwa haionyeshi chochote, na hakuna aliyegoma kupokea! Mbaya zaidi ni kuwa mawakala baada ya kuhesabu kura katika vituo vingi walitimua zao home, wakiacha mabox ya kura na wasimamizi wa vituo wakisubiri magari ya halmashauri yaje kupitia.

Mawakala wengi waliondoka na nakala za matokeo walizopewa kwenda nazo makwao, hivyo kumfanya mgombea ubunge na wasaidizi wake wategemee zile zilizokuwa zinatoka kwa wasimamizi peke yake wakati wa kujumlisha. Cha kusikitisha zaidi ni kuwa kwa vile vituoa ambavyo CHADEMA haikuwa na mawakala na walitegemea wa CUF, hawakupewa nakala za matokeo kutoka vituoni (hadi leo)

Katika mazingira kama hayo jamani wanaCHADEMA, tunaweza kweli kuilaumu CCM kwa kutuibia? Na hapa nilipo ni mjini, ambapo pamoja na mapungufu yote hayo Dr Slaa aliibuka na zaidi ya 35% ya kura zilizotangazwa na NEC! Ni katika eneo ambalo CHADEMA tulifanikiwa kuwa na wagombea udiwani kweye zaidi ya 60% ya kata zake. Imagine kuwa yapo majimbo mengi ambayo kwanza ni remote, pili hatukuwa na wagombea ubunge na hata kwingine walikuweko lakini wagombea udiwani hawakuweko.

Kwa maoni yangu naamini hata hizi 26% CCM wametuachia, nadhani hawakuamua tu kuzipunguza, wangeweza kuzipunguza sana tu bila ya yeyote kuwapinga kwa ushahidi.

Mi nadhani huu ndio wakati wa CHADEMA kujipanga. CHADEMA wamepata kura (kwa mujibu wa NEC) zaidi ya mil 2. Hii ina maana kuwa kulikuwa na wapiga kura zaidi ya mil 2 ambao wanaiunga mkono CHADEMA. Hivi kweli kutoka kwa hawa watu wote tutashindwa kupata watu 52,000 kuwa mawakala katika vituo vya kupigia kura. Mi naamini wapo watanzania wengi sana ambao wapo tayari kujitolea kwa hiari yao wenyewe, kulinda kura zao, na naamini tunaweza kujipanga na kuwa na mawakala zaidi ya hata watano katika kila kitu (kwa kutumia vyama vingine), kuwa na waratibu zaidi ya hata 10 katika kila jimbo watakaokuwa wanafuatilia kwa karibu zoezi la kupiga kura na baadae watakaoshirikiana kupata jumla ya kura na kuwa na matokeo ya jumla moja kwa moja kutoka vituoni, kabla ya kusubiri kwenda kwa mkurugenzi.

Tatizo ni pale tutakapoamini kuwa wapo watu waliopo kwa ajili ya kufanya hizi organisation. Ki ukweli ndugu zangu, hakuna mtu wa kufanya haya. Sio Slaa, wala Mnyika wa Zito wala Mbowe. Ni sisi wenyewe. Kuna kila umuhimu wa kila mmoja wetu kujisikia yupo responsible na kuhakikisha mambo yanakuwa sawa katika eneo lake alilopo, kama sio jimbo basi hata katika kata yake. Mi nadhani makao makuu wanatakiwa tu kuagiza ongozi za wilaya, ziandae mipango mikakati thabiti ya kila jimbo, ikionyesha mipanglio ya nini kitafanyika kusuka na kuimarisha mitandao ya ushindi katika kila jimbo na kila kata.

Tunafahamu kuwa katika baadhi ya maeneo CHADEMA haina uongozi kabisa au ina uongozi dhaifu (baadhi ya wilaya, hata mikoa). Kwa yale maeneo ambayo hamna uongozi kabisa inaweza kuwa rahisi kwa watu kujitolea na kuwasiliana na makao makuu. Ugumu kidigo upo yale maeneo ambayo yana uongozi dhaifu. Hapa busara inatakiwa itumike sana kwa sababu hatua zozote inabidi zichukuliwe chini au kwa kushirikisha na uongozi uliopo. Sometimes baadhi ya viongozi wanakuwa wazito kiutendaji na ukiwaandama sana wanahisi kuwa unataka kuwanyang'anya madaraka yao. Kwenyemaeneo kama hayo tuwe makini...
 
Mkuu,

Nakuunga mkono mada yako. Kuna wana-CHADEMA wenzetu wanaendekeza ushabiki kana kwamba wao wanaipenda CHADEMA kuliko wengine. Ni hao ambao tukimwaga point za kukosoa ili ijirekebishe ama hawachangii na hata wakichangia basi wanalainisha ukali kama ambavyo wenzetu CCM wamezoea.

Chama kinatakiwa kikosolewe hadharani ili kesho kisirudie uzembe unaotajwa. Na tunavyokosoa sasa hivi tuna nafasi ya miaka mitano kurekebisha kasoro zile.

Kumbuka tunazoziona humu ni ndogo na wao chamani wanazijua kubwa.

Hatuwezi kuwazuia wana-CCM wasiingie humu JF eti wataona asoro zetu na kuzitumia. Kama tunatoa kasoro zetu na kina SLAA wanaziangalia tu bila kuzishughulikia basi CHADEMA si mama kama Nyerere alivyosema CCM si mama.

Hakuna mwana-CCM aliyeikosoa CCM hadharani kuliko Nyerere. Sasa wewe una ukereketwa gani wa CCM kumzidi Nyerere aliyetoka jasho kuianzisha wakati wewe kazi yako ni kukimbiza bendera na kupayuka sera alizozijenga.

CHADEMA mmetuangusha. S lazima wote tukate kadi zenu lakini tulijenga matumaini kupita kiasi wakti kumbe wenyewe ndani mnajua uwezo wenu.

Kama kuna mwaka chama cha upinzani kilipata moral support basi ni mwaka huu. Kila mbinu ya uchakachuaji ilikuwa hainong'onwi. Hata mtoto akiisikia utaona imesambaa kwenye SMS na mwisho inatua kwenye JF na forum zingine.

Zote hizo tisa. Kumi ni pale CHADEMA ilipoweka mawakala na ikashindwa kuwatangazia wanachi kura ilizopata vituoni. Kura zimehesabiwa mwisho saa 06:00 usiku kazi ikabaki kujumlisha matokeo ya vituo jimboni. Hapa, hata CCM wanakiri uzembe wa Tume kutumia siku zaidi ya tatu kujumlisha matokeo.

Uzembe wa kujumlisha wa Tume ndiyo uzembe uliopo CHADEMA sasa hivi. Hadi sasa CHADEMA wanasubiri nini kutoa matokeo yao waliyopata kituo kwa kituo. Kama hawajatoa hadi leo basi aheri ya uzembe wa Tume kuliko uzembe wa CHADEMA ambayo hadi sasa imeshindwa kujumlisha kura za majimbo yote na kuna watu humu JF eti wanasubiri hadi leo Dr. SLAA shujaa wao awasomee.

Dr. SLAA ni shujaa nakubali lakini ushujaa gani wa kusbiri hadi sasa wakati kopi za matokeo alipelekewa na mawakala wake sik ileile.

Kuna mwenzetu humu alilaumu campaign team itubu kwa watanzania kwa nini haikuona mambo kama kuhesabbu kura kituo kwa kituo ni big deal na kuiacha Tume ihesabu yenyewe. Mwenzetu alikuwa sahihi.

Naamini ndani ya CHADEMA wapo watakaoliona hili na wanaohusika wasipochukua wajibu wa kuomba radhi basi yaliyosambaratisha NCCR pale Tanga ndiyo yatakayoisambaratisha CHADEMA.

Siombi yatokee lakini ukiutafakari ukweli sishangai yakitokea.

Wana-CHADEMA tuwe wavumilivu na tukubali kukosolewa. Mwana-CCM akitukosoa tuichukue hoja yake na tuifanyie kazi. Mbona humuhumu tunaikosoa CCM kulicho taasisi yoyote humu duniani.

Je, tusipojenga utamaduni wa kukosoana je tungeshika dola nani angetukoso. Tulilfanya kwenye uchaguzi huu ni kosa ambalo halitaondoa mioyoni mwetu.

CCM wamechakachua na hata wangetaka kutupa asilimia 10 wangeweza. Kwani nini nasema hivyo. TUmewaacha wao na tume yao ndiyo wawe maprofessa wa kujumlisha kura za vituoni.

TUmeshindwa kutumia gazeti letu la TANZANIA DAIMA au hata MWANAHALISI kupeleka correct data zionwe na wananchi halafu paleale walinganisha na kinachotangazwa na Tume.

Leo humu JF watu na akili zao wanasubiri data zitakasotamkwa na Dr. SLAA. Hivi ni nani alisema kumpenda Dr. SLAA ni kufunga nadhiri ya kuamini kila anachotamka.

Hivi hata DR. SLAA akitamka data sahihi sasa hivi inasaidia nini. Kusubiri haya kama wenzetu wanavyodhani ni kuweka shaka kuhusu uelewa wetu au exposure yetu ya mambo ya dunia hii.

Angalia hata tunavyochangia humu JF. NI ushabiki, kejeli, wakati mwingine matusi.

Sina uelewa wa sheria na hivyo napekua thread za humu kuhusu suala la TUme huru. Wanaochangia hilo karibu wote wanajikita kuichukia Tume, kuiponda, kuidhihaki, kuitukana na kuipa majina mbalimbali ya chuki.

Ni haki yao lakini hata mimi nichukia kama wao. lakini ni nani ambaye hadi sasa ameshatusaidi walau njia moja ya kuondokana na Tume hii. Je, sheria inaruhusu? Je, mtu apande mahaamani kama Mtikila alivyofanya kwa wagombea-huru?

Haya ndiyo wataalau watusaidie na tuyashughulikie ili kabla ya 2015 tuwe tumeshapata TUme mpya iliyo huru. Tukiendelea kuitukana basi hata Tume itaendelea kugonga glass ya wine wakishangilia matusi yetu kwani hakuna serikali au taasisi ilyoondolewa kwa matus, dharau au kejeli.

Tafakari.
 
Ni kweli mkubwa. Huo ni ukweli mtupu. Tusipojisahihisha tutaishia kulalamika na kutukana tu. Inasikitisha mada nzuri kama hii hakuna wachangiaji. Tuendelee kuelimishana.
 
Nikupeteje,

CHADEMA Hawajashindwa kutoa matokeo ya kituo kwa kituo. Ni matokeo hayo ndiyo yaliyofanya uongozi wa CHADEMA kuimabia NEC uwozo walioufanya. Kinachofanya wasitangaze matokeo hadi wakati huu ni kutokana na maongezi yaliyokuwa yakifanyika baina ya wadau mbalimbali na viongozi wa CHADEMA. Kwa mfano viongozi wa dini waliingilia kati kwa kuogopa kuwa matokeo hayo yakitolewa hadhalani yanayweza kuchochea hasira miongoni mwa wanachi na kusababisha kuvunjika kwa aman. Bado uongozi wa CHADEMA unatafakari maombi hayo na iwapo itaonekana hayana umuhimu basi matokeo ya uchaguzi yatatolewa hadharani wakati wowote
 
Hii thread hapo juu mmetoa analysis ya kufa mtu huu ni ukweli mtupu kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji, kimya cha Dr. Wa ulweli mie binafsi kimenikera sana hata akiongea na kutoa data sijui lini haitasaidia na anaweza kuonekana kichekesho...
 
Umeongea mambo ya msingi sana na kama Chadema wakianza sasa kufanyia kazi mikakati walioainisha kwenye website yao basi matatizo haya ya kweli yatakuwa yameshughulikiwa kwa sehemu kubwa. CHADEMA ndio tumaini la watanzania, msitusaliti.
 
Back
Top Bottom