Tusipoteze muda hata sekunde 5

The Certified

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
910
773
Usipotezee/Tusipotezee muda kujadili mfumo uliopo sasa hivi katika nchi hii MUBASHARA.....

Kwa kufanya hivyo moja tunajitafutia magonjwa ya akili. magonjwa ya hisia. magonjwa ya viungo na mengine mengi kabisa ukitaka kufanya mambo yako hapa duniani kwa amani fanya vitu vifuatavyo
1. Jitambue ulikuja hapa duniani kufanya nini na sio kusikiliza nani kasema nini

2.Ukishajua wewe ni nani fanya kile ulichojua kimekuleta hapa duniani kwa upande mmoja naweza sema kuna watu wamezaliwa kusaidia jamii na wengine wamezaliwa kuumiza jamii moja kwa moja na hili halipingiki ukitaka kuamini hili kasome kisa Cha HIROSHIMA NA NAGASAKI JAPAN au kwa walio saidia dunia kasome Kuhusu Taicoon Billgate na Wanaolandana nae..................

Nileje kwenye mada yangu sasa kwa hapa nchini umasikini tunautaka sisi wenyewe maana kila kinachoanzishwa au kinachokuwa na sindano za kuchoma akili zetu tunataka kukijua na kukifatilia kinaga ubaga hadi mwisho ila hapo tunasahau kuwa kwenye kilo 50 za mchele nyumbani haziwezi kuwa 50 milele ni kwamba zinashuka na kupotea.

Sasa ule muda tunafanya mahesabu ya nchi yetu tunasahau kufanya mahesabu ya hisia na fikra zetu bila kusahau hatua tulizopo na kutafta hatua za wengine kuzijadili na kuzifata na tunasahau kuwa hizo hatua tunazozifata za wengine hatujui itachukua umbali na muda gani kwenye maisha yako (hata yangu pia)

najua ni ngumu kabisa kuzuia hii hali ila tukiamua tunaweza na tukajikuta tunakwenda mbali sana kifikra na kusaidia jamii ila hata kwa wale wanaoumiza jamii pia hawakosekani nani ngumu kuwakwepa hata Yesu naona aliwakimbia kwa mambo yao...

sasa basi tusipotezee muda kujadili mambo ya hii nchi na kusahau nchi ya ndani ya mwili na nje ya familia yako kwani yanayotokea hayana mwisho na sio mapya ila katika dunia hii ila sisi tunafanya marudio tu au tunapita barabara iliyopitwa na taifa la enzi au karne ya 4 au 10 sasa basi kwa kujalibu kukemea haya yanayotokea duniani kwa mdomo au maandishi hata vitendo mimi naona haina mashiko kabisa kwa dunia au nchi ya sasa maana masikio yako uhamishoni na hata kama yatarudi basi hayata toa nafasi kupokea DB kutoka chanzo chochote.............

naomba nilegeze kidogo Uzi iko hivi kwa nchi hii au kizazi hiki kina fumbo kubwa sana ambacho mwenye CODE Za ku_unlock nahisi ni Mwenyezi Mungu tu yani usijichoshe kumpigia ngoma KONOKONO ukizani atakata mauno alikadhalika kwa nchi hii ya Vilaza (nimekoti kutoka kwa mtu sio maneno yangu) huwa natafuta maana ya neno hilo ila sipati kama utaweza nisaidie..........

kwa hiyo nchi hii na waliomo na wanaoongoza huwezi ongea kitu kikafanya au kukubaliwa ila kinachoweza kubaliwa au kusikilizwa na kufanyiwa kazi ni pale utakapo sema tu kwa akili yako kuwa nataka kwenda sehemu na utafanya ila sio uisemee hii nchii kuwa iko hivi iendee hivi my friend hakuna kitu kama hicho kwa sasa labda miracle itokee .
sasa nafunga kwa kusema tusipotezee muda kuikosoa na kuipinga serikali hii ila wewe ndio utapingwa na kupigwa maana hamna namna nyingine kama unakataa tumeona hela ikienda chooni na kutupwa kwenye shimo la kinyeshi tusipotezee muda kukosoa madudu ya watu tupotezee muda kukosoa madudu yetu kwanza



The Charmie..........Think out of the Box
 
Back
Top Bottom