Tusiotumia pombe njoni tupeane pole

Duniani kuna vilevi vitatu:
  1. Kilevi cha kunywa (e.g. Serengeti Lite😛)
  2. Kilevi cha Kuvuta (Bangi,Unga)
  3. Kilevi cha Kuingiza😀
Wengi wasiotumia kilevi cha 1, wako sana kwenye kilevi cha 3. Wanapiga kilevi cha 3 usiku kucha! Kwahiyo hamna haja ya kujisikia vibaya, sio kosa lenu kuwa kilevi cheni hakifanyiwi matangazo kwenye TV na Redio!
 
Kumbe! Basi sawa ngoja nibakie kuwa mnywa juisi na soda tu.
 
Ndicho kinachonikumba mara kwa mara japo taendelea kuwa hivihivi. Nimepoteza kapani kubwa na kutengwa na marafiki.
 
....msio kunywa pombe wengi wenu ni wanafki,wapenda majungu,viherehere na waoga wa maisha pia.
....sio wote though-we take many then we generalize to draw the conclusion.
Aisee sio kweli ndugu, mimi nilifuata lifestyle ya baba na mama japo dada zangu baadhi wanakunywa tungi (wawili)
 
.....halafu wanapenda sana masengenyo hao wanaojifanya hawanywi pombe-...ni hovyo kabisa.
IGWE usituhukumu katika level hiyo, wengi wetu tusiokunywa tuliamua kuwa hivi kwa kuiga wazazi wetu pia na ugumu wa maisha. Mimi kilichonifanya ni kuiga baba na mama na ugumu wa maisha
 
Usitulee nyuki, duh na ni kweli kabisa siwezi kukaa meza moja na asiyekunywa pombe
 
Dah...Pombe bana🙂🙂
Kazi kubwa ya pombe mwilini ni kutia uchizi..
Unapokunywa pombe...kimelea cha pombe(Ethanol) huingia kwenye damu na huenda kupenya katikati ya seli za ubongo na kukata/kuharibu mawasiliano na sehemu nyingine za mwili..ndiyo maana mlevi huwa anashindwa kujidhibiti...kujiona yeye ndiyo bora kuliuko binadam mwingine..kuongea/kucheka kwa sauti ya juu...kutukana...kupigana...kulia bila sababu....kuwa mzembe kwa kutovaa viatu.....na majuto yote huja baada ya pombe kuisha...na hiyo ndiyo huwa salama yake...kwani unywaji wa pombe uliokithiri huishia kwenye koma au kifo....Uamuzi ni wako.😀😀😀😀😀
 
Wakizidi kukucheka wachepukie wake zao tena kipindi wapo tungi,wataacha kukucheka na wanaweza wacha na pombe yeynyewe kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…