Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,630
- 11,096
Kwanza kabisa kwanini hautumii mitandao ya kijamii? Ilikuwa hivyo toka mwanzo au ulifuta baada ya kutumia?
Socia media zimekuwa sehemu mpya ya maisha ya binadamu kuendana na kasi na mabadiliko ya Teknolojia ila lengo kuu la mitandao ya kijamii limepotea ghafla baada ya teknolojia hii kupokewa kwa mikono miwili Duniani kote. Social media imekuwa biashara kubwa Duniani, kuanzia kwa makampuni na wafanyabishara, lakini kila teknolojia ina faida zake na hasara zake... ila kwa social media zimedhihirisha hasara ni nyingi zaidi kwa watumiaji.
Kwanini niliamua kufuta social media?
Kabla sijafika hapo, mwaka 2013 ndiyo nilijiunga na mtandao wa kijamii Facebook ambao ndiyo ulikuwa chachu ya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya mawasiliano na uwasilisaji taarifa. Hii ndiyo ilikuwa peak era ya social media... no bullsh!t, ukifungua tu Facebook unakutana na picha, machapisho na akaunti za ndugu, marafiki na watu unaowajua.
2015, nikajiunga na Instagram, vivyo-hivyo kama ilivyo kwa Facebook ukawa mtandao mzuri sana kukutana na marafiki pamoja na mastaa kutoka fani mbalimbali, ulipendwa zaidi kutokana na mfumo mpya wa kupakia picha, kuwa na following/followers, na celebrities kupewa blue ticks hivyo kuongeza usalama na uaminifu kati ya mastaa na mashabiki zao.
2016, nikajiunga Twitter. Mtandao uliokuwa ukitumiwa zaidi na viongozi wa kiserikali Duniani. Twitter ilikuwa tofauti zaidi na mitandao mingine, ukilenga zaidi text-based content. Ulikuwa ni mtandao ambao una community ya watu wa profession mbalimbali.
Baadaye nikajiunga na Musical.ly ambayo baadae walibadilisha jina na kuwa TikTok. Mtandao ambao ndiyo umebadilisha kabisa dhumuni kuu la mitandao ya kijamii kupitia short-form video contect. Mwanzo Musical.ly ilikuwa ni mtandao ambao watu wanapakia video wakifuatisha lyrics za nyimbo, pamoja na kufanya duet na wasanii/watumiaji wengine. TikTok ilipobadilisha jina la Musical.ly ikaunganisha na taarifa za watumiaji wote kwenda TikTok.
TikTok ndiyo ulikuwa mtandao wa kwanza kuufuta, mwaka 2021. Ukafuatiwa na Snapchat...
Fast forward 2025... Kwanini nimefuta social media?
1. Uraibu.
Hii tutakubaliana wote, algorithm zimekuwa designed kuwafanya watu wawe glued kwenye simu zao. Walianza kwa kuweka likes, comments, notifications ila hazikufanikiwa... hapa ndiyo TikTok alipokuja kufanya mapinduzi kwa kuleta wazo la short-form video content na wakafaulu, wapinzani wao nao wakafuata... Meta walishatambulisha IGTV ambayo ni product iliyofeli kwasababu watumiaji wengi wanataka kuona video fupifupi tu zitakazowafurahisha, chekesha, au kuwashangaza. Ndiyo wakafuata kwa kuleta Reels, YouTube wakaweka Shorts. Yote hii ni kuhakikisha watumiaji wengi wanakuwa active kwenye platform zao, watu wengi maana yake kuna biashara nyingi zitafanyika. Hatari zaidi mpaka watoto wadogo sasa hivi wananunuliwa tablets ambazo matokeo yake ni uraibu na watoto kujitenga tofauti na zamani watoto waikuwa wakijumuika katika michezo na vitu mbalimbali.
2. Kupoteza muda & umakini.
Kwa wastani Duniani watu wa umri kati ya miaka 18-24 wanatumia social media zaidi ya masaa 4 kwa siku. Ukichukua mtu mmoja-mmoja mpaka masaa 8 au zaidi kwa siku. Muda na umakini unapotea kwasababu ya ku-scroll tu.
3. Hatari kwa Afya ya Akili.
Depression, comparison, cyberbullying. Mtandao kama Instagram usipokaa vizuri basi utajihisi kwenye safari ya maisha wewe upo mwisho kabisa. Social media sasa hivi imekuwa highlight reel, picha kali, location kali, kila mtu ana pesa na maisha mazuri. Unaweza kuhisi unakuwa motivated kuona your peers wana-flex lakini s kweli, utabaki kwenye loop ya kuwa inspired badala ya ku-"get your hands dirty". Tuliotumia social media ile era ya 2010s tunajua jinsi ilivyokuwa... watu walikuwa wana-post kitu chochote, Facebook ndiyo ushahidi ulipo kwa zile picha za zamani, social media ilikuwa kwa lengo moja tu kukutana na marafiki.
4. Mitazomo hasi na isyojenga.
Kuanzia siasa, michezo, burudani. Social media imekuwa kijiwe cha kila mwenye simu... kila mtu anaweza kutoa mawazo yake mpaka wajinga, unaweza kutoa mawazo chanya au kupakia chapisho lolote akaja mtu kukutukana au kuandika chochote anachoona kwake yeye ni sawa.
5. Habari na taarifa za uongo.
Usipokuwa makini ni rahisi kuuchosha na kuujaza ujinga ubongo wako kutokana na vitu vya uongo vinavyochapishwa kila siku.
Zipo sababu nyingi lakini kwangu hizo ndiyo zimepelekea nikakaa mbali na mitandao ya kijamii.
Lengo la social media limepotea siku nyingi, siyo sehemu salama tena kwa mtumiaji wa kawaida, labda wafanyabishara, mashirika na watu maarufu.
Mfano: Meta, Instagram waliona haitoshi kukawa na reels tu, wakaleta suggested posts ili tu wakulazimishe uone trending posts/reels kwenye timeline yako. Ukienda X (Twitter) imekuwa uwanja wa cyberbullyingi, watu wanaona ni sifa kuuvua utu wa mtu au kutukana ilimradi tu wapate impressions ili wapate bahasha kutoka kwa Elon Musk kupitia X Payouts.
Nina mengi ya kuandika ila haya yanatosha... wapo watakaouliza kwanini natumia JamiiForums, sitawajibu maana jibu lipo wazi, ni kama ambavyo bado bado natumia Reddit na YouTube.