Tusione aibu kwa mambo haya 4

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
⏩NGUO ZA ZAMANI, Kwa sababu mavazi/nguo zilizochakaa hazitafsiri vipaji vyetu na undani wetu wapo wanaovaa vibaya lakini kwenye maisha yao wana kila kitu cha thamani, mafanikio hayapimwi kwa muonekano.

⏩MARAFIKI WA HALI YA CHINI, kwa sababu hakuna hadhi ya kujifaharisha kuwa na rafiki tajiri, msomi wa masters n.k wakati hatujafikia level zao, tuwafurahie tulio nao huenda hawa masikini ndio watu muhimu katika maisha yetu, jinsi tunavyoishi ndivyo tutakavyopata marafiki tunaoendana nao.

⏩WAZAZI WALIOZEEKA, kwa sababu ivyo ulivyo leo ni wao walifanikisha kwa namna nyingi sana, tujivunie wazazi wetu haijalishi hawana kitu eti wapo kijijini wanalima wamezeeka tunaona aibu ata kumpeleka marafiki/wachumba tunaowapata kumtambulisha kwa wazazi.

⏩MAISHA YA HALI YA CHINI, kwa sababu mafanikio yanakuja kama tukiishi katika maisha yetu ya uhalisia tusijaribu kuigiza(pretend) wengine tuishi jinsi maisha yalivyotupangia huku tukiendelea kutatua changamoto zinazo tukabili tutaona mafanikio yanakuja tu.

TUSIONE AIBU.
 
Back
Top Bottom