Tusimuliane: Umetoka wapi na career yako?

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Nimekumbuka mbali. Tusichekane.

Nikiwa na umri mdogo, nilikuwa nasikiliza sana vipindi vya redio kabla ya ujio wa televisheni na mapinduzi yake. Huko nikadevelep interest na media lakini zaidi nikavutiwa na kuwa DJ.

Mbele mbele kidogo, interest ikabadilika. Nikaongeza na kusoma sana magazeti, hivyo nikawa mtu wa redio na magazeti. TV haikuwahi kuniteka sana hata ilipokuja.

Nikaachana na kupenda U-DJ nikahamia kutamani kuwa Mwandishi kwa sababu nilikuwa nikisoma sana makala na kufuatilia habari zote.

Siku hazigandi, masomoni kuelekea Chuo Kikuu machaguo yakaongezeka kiasi cha kunivuruga kidogo. Nikawa mtumiaji sana wa internet ambako nikakutana na vitu vingi sana sana. Ilifikia hatua nikawa sijui kipi naweza kufanya kwa sababu sikupataga nafasi ya kupractise chochote kati ya vile ambavyo niliona vinanivutia.

Nikajikagua, kwenye uchaguzi wa kozi nikajikuta nimeangukia Masscom with Public Relations. Huko nikaelewa vizuri ni kitu gani naweza kufanya na ndicho nafanya mpaka sasa.

Stadi nzuri za kuwasiliana na kushawishi zimenipa nafasi ya kufanya kazi kwa ubora na utofauti kila ninapokuwepo. Zaidi ya yote nafurahia kufanya hivyo. Nachukulia ni kipaji na taaluma.

Wewe una kipaji gani? Unakitumia?
 
Me kipaji changu bado sijakijua naona kimejificha naishi kwa kuunga unga ila kuna siku nitaamua tu kufurahi nitanunua bange nyingi nitavuta sana hapo kipaji changu kitaonekana alafu nitakusimulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina kipaji cha ushawishi..niko vizuri sana katika ushawishi aseee

Naweza nikaongea na mtu mfano yuko na hasira ama hataki kufanya jambo fulani akatuliza hasira na akalifanya hilo jambo,mwanzo sikuwa najua niko na hiko kipaji lakini kadri navyozidi kwenda mbele ndivyo navyozidi kupata hizi compliments kutoka kwa watu tofauti tofauti

Nina uwezo wa kuzoeana na mtu wa rika lolote ndani ya muda mfupi kama nikitaka
 
Safi sana Joanah. Watu wa aina yako ni muhimu kila sehemu. Unafanya kazi inayoendana na hicho kipaji chako?
 
Japo sijapata nafasi ya kukitumia ila nina uwezo mkubwa wa kushawishi watu wakubali nilichopanga mm wakikubali (convincing power), hapa naona nafit kuwa marketing officer japokua sijasomea hii fani. Niligundua hili nilipokua advance na pia Watu kadhaa wameniambia. Nadhani muda utafika uwezo huu utaanza kuniingizia pesa.
 
Sio rahisi kihivyo mkuu.
Unapokwenda kufanya kazi ya marketing mitaani unakutana na mengi.
Utakutana na wavuta bangi,waliovurugwa na maisha,vichaa,wenye njaa.
Hao wote unatakiwa uende nao sawa na kuwashawishi ili wanunue bidhaa zako.
Na pia kumbuka unapewa target ya sales volume kwa mwezi,kwa mfano kama ni soda unawezz ukaambiwa kwa mwezi uuze kreti 9000.
Hapo lazima upate stress sana ndio ulipwe hela
 
Asante kwa ushauri. Ndio maana nikasema bado sijapata chance ya kutumia ila ngoja nianze na hii kitu huenda ikanitoa kimasomaso.
 
Nina kipaji cha ushawishi..niko vizuri sana katika ushawishi aseee

Naweza nikaongea na mtu mfano yuko na hasira ama hataki kufanya jambo fulani akatuliza hasira na akalifanya hilo jambo,mwanzo sikuwa najua niko na hiko kipaji lakini kadri navyozidi kwenda mbele ndivyo navyozidi kupata hizi compliments kutoka kwa watu tofauti tofauti

Nina uwezo wa kuzoeana na mtu wa rika lolote ndani ya muda mfupi kama nikitaka
Unakipaji kama changu Approaching power
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom