Tusilaumu madaktari tu...

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,307
4,585
Watu wengi tumekuwa na tabia za kulaumu sana watumishi wa afya kwa kuwapa kila aina ya sifa mbaya. Ni kweli kwamba sifa nyingi wanazistahili.
Lakini mtu huyohuyo anayelaumu sana, ukimkuta eneo lake la kazi, utasema bora nikutane na daktari maana atanipa hata kitanda nipumzike.
Hakimu anashinda kuahirisha kesi, afisa ardhi anauza kiwanja chako kwa tajiri, polisi anakubambikia kesi, afisa utumishi hataki kujaza fomu zako za likizo n.k.
Kila mtu asipofanya kazi yake inavyostahili kuna mtu anaumia. Tofauti ni moja tu, watumishi wa afya wakikosea wanaweza sababisha kifo, lakini kada nyingine pia huleta madhara mengine mengi.
Sote tukubali, kazi zote ni wito, na si kwa madaktari, polisi na walimu tu. Wote wanapaswa kufanya kazi kwa wito. Haiwezekani baadhi ya viungo vya mwili viwe na wito zaidi ya vingine, kwani vinafanya kazi kwa kutegemeana.
Sote tupunguze madhara na malalamiko maeneo yetu ya kazi kwa kuchapa kazi ili wateja wanapoondoka, watoke wakiwa na tabasamu.
 
Back
Top Bottom