Tusikwepe wajibu wetu katika jamii yetu

APA CHICAGO

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
259
293
Kuna watu wengi wanakwepa majukumu yao katika jamii yetu kwa kisingizio kuwa haya au hayo ni mambo ya kisiasa.

Binafisi huwa ninawaza watu hawa uelewa wao wa mambo ni mdogo sana au wameamua kwa makusudi wawe vipofu?

Tuelewane kidogo iko hivi siasa ndiyo inaendesha kila kitu katika maisha yetu takribani asilimia tisini (90%) ya mambo mbalimbali yanaongozwa kisiasa.

Nitataja mambo machache kadhaa ili kuonyesha kuwa siasa inagusa kila pembe ya maisha yetu.

1. Ujenzi wa miundo mbinu kama vile barabara, madarasa, majengo ya hospitali n.k. yote haya yanatekelezwa kwa nguvu za kisiasa.

2. Ajira mbalimbali katika serikali hasa utumishi wa umma na sekta binafisi zinategemea siasa.

3. Mishahara na marupurupu ya wafanya kazi hasa watumishi wa umma vinategemea siasa.
Wapo watakao bisha au kukataa ukweli huu lakini ieleweke kuwa maisha yetu yanaathiliwa sana na maamuzi ya wanasisa hii ndiyo kusema siasa ni elimu yetu, siasa ni barabara zetu na siasa ndiyo bei ya sukari dukani na pia ndiyo bei ya kila kitu dukani.

Hivyo basi ukimuona mtu anasema mimi siwezi kujihusisha na mambo ya siasa mtu huyo ni wa kumhurumia tu maana hajui alitendalo na alinenalo.

Ushauri wangu ni kuwa tushiriki katika siasa kwa lugha za staha, bila unafiki, chuki na uzandiki.

Tusikwepe kutimiza wajibu wetu katika jamii kwa kisingizio kuwa hayo au haya mambo ni ya kisiasa kwani kila kitu kinachofanyika katika jamii yetu ni matokeo ya michakato ya kisiasa. Niko tayari kukosolewa mtazamo wangu.
 
Back
Top Bottom