Mayombya Jr
Member
- Oct 24, 2022
- 25
- 30
Habari,
Nimesoma bandiko la Thadei Ole Mushi kuhusu "Mshahara wa Mwalimu unavyotafunwa CWT" la Dec 2022.
Lakini pia nimepitia uzi wa Mpwayungu Village kuhusu Tuungane kwa pamoja kuwasemea walimu, hakika nimetafakari kwa kina jambo fulani.
Sekta hii ya ualimu ni sekta nyeti sana nchini, lakini walimu wetu hawajitambui kwakweli, walimu wamekuwa ni chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya mtoto wa kike katika jamii yetu.
Naomba mniwie radhi ili mimi nimsaidie Mwl Mpwayungu Village, kuwasemea na kuonyesha upande wao wa pili ulivyo katika jamii, pengine serikali hawajui haya.
Kuna shida kubwa sana kwa walimu hasa katika upande wa maslahi hatukatai hilo, bali pia kuna shida ya hawa walimu kushiriki katika tabia chafu inayorudisha nyuma maendeleo yetu, na hii utokana na maslahi madogo ambayo hayakidhi mahitaji ya mwalimu kwa mwezi.
Kuna mtu alileta uzi humu jamvini, kuhusu 80% ya wanawake na waschana ni omba omba, ni kweli sikatai hilo lakini kuomba omba kwao, sisi wanaume tusiyojitambua wakiwemo walimu ndiyo tumewatengenezea.
Tumekuwa mstari wa mbele kuwaharibia jinsia ya kike future yao, hatutaki kusaidia serikali kuhakikisha mtoto wa kike anapata Elimu itakayomsaidia katika maisha yake ya baadaye.
Baadala yake tunawabebesha mimba tunawaharibia maisha yao alafu tunakuja humu jamvini kuwasimanga, mfano, viongozi wanao husishwa na kurudisha nyuma maendeleo ya mtoto wa kike kupata Elimu, kule Kata ya Ikunguigazi Wilayani Mbogwe-Geita tunaomba wachunguzwe jamii tumechoka, tunaomba kujua serikali imechukua hatua kule Ikunguigazi.
Tumechoka na vitendo vya rushwa vinavyo rudisha nyuma maendeleo yetu, kama viongozi waliotajwa wamehusika kwa namna moja ama nyingine kupindisha sheria usichukue mkondo wake ili haki isipatikane kule Ikunguigazi Wilayani Mbogwe-Geita wawajibishwe.
Tunaanda taifa la aina gani, taifa la omba omba, wakati sheria zipo ila rushwa inaonekana ina nguvu kuliko sheria zenyewe, hii haikubaliki katika jamii na taifa kwa ujumla.
Mwl Mpwayungu village, tunawapenda na tunaheshimu kazi yenu kubwa mnayoifanya walimu katika jamii, nitaleta mada humu hapa kuomba serikali iingilie kati kuokoa mtoto wa kike, kutoka kwenye mikono na walimu na watu wasio wema.
Haiwezekani binti abebeshwe mimba na mwalimu wake, amfiche mwaka mzima alafu amtelekeze na mtoto, alafu atumie pesa zake kuzuia hatua isichukuliwe dhidi yake, niombe serikali hizi siri/uovu zinapo ibuliwa katika jamii wawe wepesi kufuatilia na kuchukua hatua.