Tusijisahau binadamu wote ni sawa

Tusijisahau binadamu wote ni sawa

majoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
2,706
Reaction score
5,111
Tukumbushane wandugu.

Kumekuwa na matukio ya watu kujisahau na kujiona wao ni bora kuliko binadamu wengine. Kumbuka wewe ni udongo na mavumbini utarudi, wewe ulizaliwa na utakufa tu hata uwe na elimu au mali kiasi gani. Hebu tuache kubaguana na kujiona sisi ni zaidi ya wengine!

Nimeamua kuandika hili hasa kipindi hiki cha Corona ambapo wenye pesa na vyeo vyao wanajiona bora na kwamba wanahitaji kuishi zaidi ya wasio na kitu.

Unauza barakoa bei kubwa ili wasionacho washindwe kununua kwa kukosa pesa. Ni vema tungehakikisha kila binadamu anapata barakoa na anaitumia ipasavyo. Hakuna anayejali akiona wengine hawajavaa anajiona yeye ana pesa na ana akili kwa kuwa amejilinda bila kusahau hao ambao hawajajilinda ndio watakaokuambukiza. Nilikuwa sokoni, kuna waliovaa na wasiovaa. Waliovaa wanawakodi wasiovaa wawabebee mizigo yao! hapo umejilinda nini?

Kujilinda kwako kutakuwa na maana kama utahakikisha kila unayekutana naye amevaa barakoa na amenawa mikono mara kwa mara. Piga kelele bei za barakoa zipungue ili wote wavae pia hamasisha wanaojiweza wajitolee kuwanunulia wasiojiweza na kuwapa elimu na jinsi ya kujilinda! Kundi hili la wasiojiweza likiwa salama ndipo kutakuwa na usalama kwa wanaojiweza.

Maofisi mengine mabosi ndio wanathamani na wanajaliwa na kupewa sanitaizer na kumsahau mlinda mlango, mhudumu na mtu wa chini ofisini. Usipowalinda hawa unaowaona wa hali ya chini, hawana elimu, wafanya kazi za hovyo bado hutakuwa salama.

Kuna wengine ni uelewa mdogo unawafanya wasijali kunawa na kuvaa barakoa. Waelimishe. Hakuna taasisi itakayofanya kazi hii zaidi ya mimi na wewe. Tujilinde sote kwa faida ya wote!

Tukumbushane, toa wazo lako unafikiri tufanye nini ili kujilinda zaidi.
 
Back
Top Bottom