Hbr ya Asubuhi wana jf ktk jamvi hili la MMU...
Leo ni jumapili tulivu sana ikiwa na shamrashamra za kumbukizi za Yesu kristu kukishinda kifo takribani miaka 2000 iliyopita.
Shamrashamra za siku ya Leo huwa za aina yake kwa makundi ya rika tofauti ktk jamii zetu.
Kwa vijana wengi siku hii ni kama nafasi adhimu kwani hupewa fursa ya kwenda kutembelea maeneo tofauti tofauti mbali na nyumbani ilimradi tuu wafurahi
Wengi wa vijana ( teen age) hufurika nyumba za wageni KUGEGEDANA, jambo ambalo sio kumchukiza Mungu tuu bali huweza pelekea maambukizi mapya ya VVU, mimba zisizotarajiwa na hata kuharibu uhusiano mwema na ndugu, jamaa au marafiki.
Wito wangu kwa wenye tabia hizo ni kuwa wabadilike kuanzia pasaka hii na kuendeleza mema daima. Kuchepuka pia iwe mwisho.
Nawatakia pasaka njema wote wenye kuamini.