Elections 2010 Tusiishie hapa.

IsayaMwita

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
1,127
140
Kila mpenda MABADILIKO afanye kwa sehemu yake, wale tutakao weza tuhakikishe tunasimama kama mawakala wa CHADEMA, na wale tuliopata nafasi ya usimamizi naomba tukalinde kura za Slaa, Ushindi ni lazima.

Wengine wenu tumepotea hapa jamvini na si kwamba tunapenda ila vita iliyoko mbele yetu, najua wangine wenu mko nyuma yetu.

Ndugu zangu ni wazi sasa CCM wamekosa mshiko sasa wana mkakati wa kuwapotosha Watanzania waamini kuwa Kura ZITAPIGWA kiudini na hii si kweli, hoja ya msingi ilikuwa ni vita dhidi ya Ufisadi ambao Mweshimiwa KIKWETE ameshindwa kuufanyia kazi, Mikataba ya Madini haikufanyiwa chochote.

Ndg zangu nawaombeni sana tuwe mabalozi wa kutoa elimu sahihi kwa Watanzania waliowengi ambao CCM inaweza kufanya lobying kwa hizi siku chache zilizobaki.

Ni wazi sasa Tanzania ya kesho itakombolewa na wewe Mwana JF Simama kwa zamu yako.

Na mwisho jihoji moyoni mwako utaifanyia nini Tanzania hii 31/10/2010 na kama si kuchagua kiongozi atakae mkomboa shangazi yako mama yako, ?
 
Ila nawaomba wahusika wa chadema hasa watakaoenda kusimamia kura kuweni makini nao wapo mamluki wa ccm angalizo natoa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom