Mtanisamehe watu wa tusiime, wamiliki na walimu ila ukweli ni.....
nilikuwa na mtoto wangu anasoma pale nursery nimemuhamisha kisa...? administartion wameshindwa kudhibiti idadi ya watoto darasani, ukienda pale watakupokea na watakwambia lipia ada mtoto wako asome ukifika wanakwambia peleka mtoto wako dara sa fulani hata darasa hujui likwapi unafanya kuulizia ukifika darasani ticha anakwambia siwezi mkumpokea mtoto kwa sababu darasa limejaa nitashindwa kuwacontrol watoto na kucheki hivi darasa lina watoto 40 lol na wakwangu anakuwa wa 41 na wengine nyuma yangu wako 8 heeeh!! ntafanyaje sasa na ada hawarudishi daah!
akili kumkichwa ada yako isiende bure...
ikabidi nilonge na mwalimu kiingereza ili akuone wewe ni mzazi wa msomi wa kileo na fweza ipo coz kihaya sikijui na mie siyo mhaya, nikamnong'oneza ticha, mpokee mtoto wangu tutakuwa na mawasiliano mazuri palepale nikadondosha wekundu ticha akamkumbatia my son na nikamwacha hapo ila nilipotoka hapo nilianza kupiga simu kutafuta shule nyingine. Mwaka mzima ikawa ni kumrushia vocha ya simu ticha na kumpelekea vizawadi kama matunda, saa, pochi coz ni mwanamke na ili mtoto afundishwe na aende na wakati coz darasani wako wengi ikabidi ticha aniambie itabidi tumpe mtoto extra classes wakati wenzie wanacheza yeye anakuwa nae bennet kusoma na kweli performance alichange ila money needed for extra classes. Daah i payed the tuition fee cash kwa ticha hii ya kwake sio ya shule yaani baada ya mwaka hawakuniona tena nilimsepesha kid wangu now yuko shule ambayo iko poa wanafunzi wachache na maendeleo mazuri.
Tusiime ilikuwa shule nzuri imeharibiwa na hao wahaya wenyewe kutodhibiti idadi ya wanafunzi darasani na pamoja na kulipa ada kubwa why ulipe tuition tena? inamaana ada unayolipa ni ya kula lunch na usafiri tuu, kusoma ndo iwe tuition? kwa kweli management yao inatakiwa ijipange upya vinginevyo itakuwa kama ilikuwa kama ilivokuwa st marry's ya mama rwakatare ilikuwa nzuri kipindi inaanza now days imebaki school bus tu!! lol!
si bora umpeleke mtoto shule hizi za kata then ulipie tuition kuliko ulipe academy na bado upeleke tuition. Kwani tuition kazi yake ni nini? labda mie sielewi ila hii ya Tusiime sio fair hata.
nawakilisha tuu
ever remaining,
Sakapal