Kwali shule hiyo ni ghali. Kwani shule hiyo ipo wapi?
Serikali yetu ina vituko!
Nilishawahi kushauri iundwe Regulatory Authority kama ilivyo SUMATRA,EWURA,TACRA nk ili kusimamia elimu na kiwe chombo huru. Hakuna nchi hata moja hapa duniani ukiachia za kiafrika ambazo zinachia sekta nyeti kama elimu iendeshwe kama biashara ya wamachinga!!
Najua fika shule nyingi za serikali sio shule bali ni mabanda ya kufugia kuku lakini wao wanayaita shule. Kama akiwepo Regulator nyingi zitafungwa kwani hazifikii kiwango.
Sitaki kudumaza mawazo yenu lakini kumwambia mtu anyelalamikia ulanguzi wa karibu Milioni moja na ushee ili mtoto apate elimu ya msingi kwenye hiyo shule japo siifahamu lakini kwa hilo jina linafanana kama kuna asili ya Kiganda kama nakosea kunisahihisha ruksa.
Panahitajika kuwepo na Regulator vinginevyo elimu Tanzania inaelekea kuzimu tuache kuganga njaa the same applies kwenye sekta ya Afya!
Huu mzaha na CCM hautufikishi mbali kuna siku mtanikumbuka!!
Hapana shule ni ya Mhaya hana ubia na mganda mwenye shule anakwambia alianzia ahule ya chekechea sebuleni kwake mpaka hapo alipo!!na alikataza hiyo nyumba yake aliyokuwa anaishi na akaanzisha chekeche ibaki kama makumbusho!!..........Kimsingi zina bei kubwa sana mfano ni kama shule ya St Anne Marie wao wana mihula minne(4) bei ni 385,000/-+Transport sasa fikiria hapo!!na kwa nini kuwepo na mihula minne(4)?? Nadhani nitakuwa nimekujibu vema ndugu Magezishule ni wahaya na waganda
Wahaya watu wabaya sana!
Shule ina mihula mitatu. Kila mhula shilingi 325,000 sio bweni, usafiri 70,000 kwa mhula computer studies 30,000. Huyo ni mwanafunzi wa msingi. Gharama hizi ziko juu sana. Hiyo bodi ya shule sijui kama wanaelewa mateso wanayopata wazazi. Tunaomba zipitiwe upya ikibidi na mamlaka zinazohusika. Wazazi wanaumia sana hawana pa kusemea tu. Kama elimu ni biashara, basi hawa jamaa wafungwe gavana. Itakuwaje mwanafunzi wa msingi alipe sawa na mwanafunzi wa sheria chuo kikuu? Huku ni kukomoana. Nawasilisha