Tusiiangalie pesa kwa tarakimu zake bali kwa PURCHASING POWER yake – Money Redefined! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiiangalie pesa kwa tarakimu zake bali kwa PURCHASING POWER yake – Money Redefined!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Revolutionary, Feb 20, 2011.

 1. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  PART 1

  Kuna msemo usemao pesa uliyonayo mkononi leo ina thamani zaidi ya pesa utakayokuwa nayo mkononi kesho. Pia kutoka katika nadharia ya Gordon (1959) kuna msemo mwingine usemao ndege aliyeko mkononi kwako sasa ni bora kuliko ndege wawili walioko msituni!

  Hii yote ni misemo inayojaribu kutukumbusha thamani ya pesa kufuatana na wakati na mazingira husika.
  Kwa muwekezaji ni heri apokee pesa sasa kuliko kupokea kiasi hicho cha pesa isiyokuwa na uhakika baadae kutokana na ‘RISK’ na changamoto nyingi za kiuchumi zisizotabilika.

  Wengi tunaitazama pesa kwa namna na maana mbali mbali lakini leo hebu tuizungumzie pesa kutokana na uwezo wake wa kufanya manunuzi (Purchasing Power) katika wakati na mazingira husika.

  Mfumuko wa Bei na riba. Inflation and Interest rates
  Mfumuko wa bei au ‘Inflation’ kwa lugha rahisi ya kiuchumi ni kupanda kwa thamani ya bidhaa mbalimbali. Sasa nataka tuitizame picha hiyohiyoya kupanda kwa bei ya bidhaa kwa mtazamo mwingine, kwa mtazamo kwamba inflation pia kwa uhalisia mwingine ni kushuka kwa thamani ya fedha husika.

  Kwa mfano bidhaa au huduma uliyoweza kununua jana kwa shilingi 1,000 leo ikipanda bei na kuuzwa TZS 1,500 hutaweza kuinunua kwa Shilingi 1,000 ya jana. Hapo inamaanisha kwamba shilingi 1,000 sasa zimeshindwa kununua bidhaa au huduma hiyo. Yaani Purchasing Power ya pesa hii imeshuka na kimsingi sasa yakupasa kutoa shilingi 1,500 na kwamba kilichobadilika sio kupanda kwa bei ya bidhaa au huduma hii bali ni kushuka kwa Uwezo wa fedha hii na kufanya isiweze kukidhi kununua bidhaa hiyo.

  Kimsingi kuna sababu nyingi sana zinazopelekea kushuka kwa thamani ya fedha au kwa lugha nyingine kuoengezeka kwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali kama vile kuongezeka kwa gharama zitokanazo na kufanikisha uuzaji na ununuaji wa bidhaa au huduma husika. Mfano kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, usafirishaji na gharama mbalimbali ambazo hubadilika kwa kadri ya wakati na kwa kadri ya ubadilikaji wa bei za bidhaa nyeti zinazoendesha uchumi wa dunia kama vile mafuta na nyinginezo.

  Llengo langu leo sio kuyazungumzia hayo, kwani nitayazungumzia wakati mwingine inshalah! Leo nataka tuizungumzie pesa kwa mtazamo wa Purchasing Power yake.

  Wataalamu wa mambo ya kifedha wanawanajua namna mbalimbali za kuweza kucheza na fedha kiasi cha kufanya kwao pesa siku zote iwe na thamani na Purchasing Power kubwa kulingana naWAKATI na MAZINGIRA ya wakati huo.

  Udadisi wangu katika mambo fedha ndio ulionifanya nivutiwe na kutaka kujifunza zaidi ili kubobea katika masuala haya ya kifedha kwani hakika If you are smart enough when it comes to money, Money will always be knocking at your door while always escaping from other peoples wallets. Naahidi sitaacha kuwamegea kile kidogo ninachojifunza ili muweze kuelewa na kuweza kufanya maamuzi sahihi kuhusu fedha ili siku zote ziwafaidishe katika maisha yenu.

  ITAENDELEA!.........
   
 2. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2011
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu vp mbona somo haliendelei au?
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  somo limefikia wapi mkuu?
   
 4. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Napenda kuwashukuru wote kwa comments zenu! ninapost part 2 ya post hii soon ili tuendelee kujuzana ili tuwekane huru!
   
Loading...