Tusigwajimaise? Au tusihoji?

Tusigwajimaise? Au tusihoji?

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
445
Reaction score
553
Hivi karibuni, Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa CCM, alisema kile ambacho wengi wamekuwa wakiongea chini kwa chini:

“Vipi kama mtoto wa Rais ndiye angetekwa? Tungesema nini?”

Alizungumzia utekaji, mauaji, na hali ya sintofahamu nchini kwa lugha ya hoja, si matusi. Alitoa mapendekezo na akaonesha uchungu wa taifa.

Lakini kilichofuata?
🎭 Si majibu.
🎭 Si maelezo.
🎭 Si uthibitisho wa usalama.

Kilichokuja ni matusi, kejeli, na press conference za vijana wa UVCCM zikimtukana badala ya kujibu hoja.
Halafu TCRA wakaenda mbali zaidi – wakaandikia vyombo vya habari vifute press yake kwa sababu "haikuwa balanced".
Kwani press za kisiasa huwa balanced? 😅

Swali Dogo la Kiintelijensia:
Kama hoja za Gwajima hazikuwa na msingi – kwa nini zimeumiza mioyo hadi ngazi ya TCRA na vikao vya chama?

Kwa nini Rais mwenyewe kwenye mkutano mkuu wa CCM akasema:
“Tusigwajimaize chama chetu. Magwajima tuyaache nje.”

Je, kumuacha Gwajima nje maana yake ni kumuacha nje yeyote anayehoji?
Au chama hakitaki kujigwajima yaani kusikia ukweli mchungu?

Tusisahau:
Kusema ukweli ni sehemu ya kujenga nchi.

Kuhoji si usaliti – ni uzalendo.
Mbunge kusema “tunashindwa kulinda maisha ya watu” si uasi – ni wito wa mabadiliko.
“Demokrasia haijengwi kwa kushangilia tu. Inajengwa kwa kuuliza maswali magumu hata kama yanatoa jasho.”

Tusifunge mdomo wa aliye ndani ya nyumba kwa sababu anasema kuna moshi.
Labda moto upo kweli.

📌 #TuhojiKwaAmani
📌 #TusigwajimaizeDemokrasia
📌 #HojaSiMatusi
📌 #TanzaniaYetunayoitaka
 
Attachments

  • 20250120_091154.jpg
    20250120_091154.jpg
    344.2 KB · Views: 14
This time around..hata kama unahoja ya kujenga njia pekee ambayo ni nzuri ni shut up your mouth.. nakuhakikisha familia yako inapata mahitaji yote..unalala salama na kuamka salama amani tele ukijipendekeza kwa wananchi kimekula kwako..ndomaana tunachotakiwa kukipata sasa ni kutokuwa na vyama vya siasa nchini au kubaki na chama kimoja tu..binafsi ukiniuliza swali..Kuna umuhimu gani wa kuwa na vyama vingi nchini? ntakujibu, "hakuna umuhimu zaidi ya kuleta hasara kwa nchi yetu".
 
🤝🤝🤝
 
Back
Top Bottom