Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Ndugu wana JF
Mimi binafsi si mwanachama wa chama cha CUF, lakini nimekuwa nafarijika sana jinsi chama hicho kilivyoibana CCM visiwani Zanzibar mpaka kufikia hatua ya kugawana madaraka. Tukubali au tukatae, ukweli unabaki kuwa CUF kimejenga historia katika visiwa hivyo.
Kwangu mimi, adui namba 1, 2 na 3 wa Tanzania kwa sasa ni CCM. Mgawanyiko wa CUF ni furaha zaidi kwa CCM; ikiwezekana, CCM kiko tayari kufadhili mgawanyiko huo. Nguvu ya CUF Zanzibar imekuwa ni kero kwa CCM; kama nguvu ya CHADEMA inavyoanza kuwa kero kwa CCM huku bara. Mgawanyiko unaoendelea CUF baadhi yetu tunaufurahia kana kwamba utaishia CUF tu. Ni mkakati thabiti. Umepangwa. Baada ya CUF kufa au kupungua nguvu Zanzibar, nani atafuata?
Kila mpenda maendeleo na demokrasia, asifurahie kifo cha CUF, hasa Zanzibar, na zaidi Pemba.
Mimi nasema ukweli, sipendi CUF ikose nguvu Zanzibar.