Tusifanye maigizo kwenye kumbukizi ya Hayati Nyerere

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Na Elius Ndabila
0768239284


Kati ya watu wagumu kuwajadili hapa duniani ni Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ni kwa sababu ya wingi na ukubwa wa mambo makubwa aliyoyashughulikia kabla ya urais wake na baada ya urais, uliodumu zaidi kidogo ya miongo miwili .Wakati Nyerere anafariki dunia kutokana na kansa ya damu akiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Tomaso mjini London, Oktoba 14, 1999, alikuwa amedumu katika siasa kwa takriban miaka 45. Huu ni muda mrefu na ulikuwa na mengi – iwe mafanikio au mitikisiko. Alifariki akiwa na umri wa miaka 77.

Nimekuwa ninajaribu kufuatilia midahalo mingi inayomhusu hayati Mwalimu Julius K Nyerere katika mienendo yake, misimamo yake na falsafa yake katika hatima ya Tanzania na Afrika kwa ujumla. Ni wazi kuwa watu wengi wakiwepo viongozi wastaafu na viongozi mbalimbali waliopo madarakani wamekuwa wanamzungumza Nyerere kama ndiye mtu pekee ambaye mawazo yake yanaweza kulisaidia Taifa. Si hivyo tu bali wapo wanaoona fahari sana kumtaja kila mahali Mwalimu Nyerere wanapotaka mambo yao kupita. Wanaozungumza wapo katika njia sahihi ya kueleza hayo huku wakihusishanisha na kipindi Mwalimu Nyerere yupo madarakani. Nikiwa ninafikiria hotuba mbali mbali za viongozi ndipo nikagundua kunaweza kuwa na njia sahihi lakini kusiwe na wakati sahihi. Ifahamike pia kuwa mimi ni sehemu ya Watanzania wengi ambao tulikuwa hatumfahamu Mwalimu, lakini kupitia vitabu mbalimbali na hotuba zake zilizoko youtube basi imekuwa rahisi wengi kujua Mwalimu ni nani? Kwa ufupi Mwalimu alikuwa krunzi.

Inawezekana mpaka kufikia kwenye hitimisho langu nikatofautiana na watu wengi wakiwepo madaktari na Maprofesa na Watanzania wengine wengi, lakini hayo yabaki kuwa maoni na mtazamo wangu katika kusherehekea miaka 20 bila Mwalimu Nyerere. Tunasherehekea kwa kuwa bado kila tunaposimama na kufanya jambo, basi mawazo ya Hayati Baba wa Taifa yamekuwa kama ibara kwenye katiba. Kwani maneno na misimamo yake huwa inatupa uelekeo wa namna ya kutenda na kutokutenda. Kwa kifupi maneno yake ni dira.

Aliheshimika Duniani kote ndiyo maana aliweza kupa tuzo mbali mbali. Kwa mfano Nchini Marekani kuna vyuo vikuu vitatu vilivyowahi kumtunukia Nyerere shahada za heshima ya udaktari wa falsafa ambavyo ni Duquesne, Howard na Lincoln.Si hivyo tu, bali chini Uingereza Chuo Kikuu cha Edinburgh alichosomea kilifanya hivyo pia, na hali kadhalika Chuo Kikuu cha Toronto nchini Kanada.. Barani Asia, Nyerere alipewa heshima hiyo ya udaktari wa falsafa na Chuo Kikuu cha Ufilipino pamoja na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru cha India. Huko Amerika ya Kati, nchini Kuba, Chuo Kikuu cha Havana hakikubaki nyuma kwenye kumtunuku Nyerere shahada hiyo ambayo msingi wake mkuu ni kuheshimika kwa utendaji, akili na uadilifu.

Barani Afrika ndiko alikopata shahada nyingi zaidi za heshima za udaktari wa falsafa ukianzia na Chuo Kikuu cha Cairo nchini Misri, Chuo Kikuu cha Nigeria, Chuo Kikuu cha Ibadan nchini Nigeria pia, Chuo Kikuu cha Liberia, Chuo Kikuu cha Taifa cha Lesotho, na Chuo Kikuu cha Fort Hare cha Afrika Kusini. Nchini Tanzania Nyerere amewahi kutunukiwa heshima hiyo na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

. Mbali ya shahada hizi, itakumbukwa pia Januari 26, 1996 Nyerere alikuwa mtu wa kwanza kupewa Tuzo ya Kimataifa ya Amani ya Mahatma Gandhi ya mwaka 1995 iliyotolewa na Serikali ya India. Nyerere aliwashangaza viongozi wa India siku hiyo aliposema kwamba hakustahili kupewa Tuzo ya Gandhi kwa sababu yeye alishiriki kwenye mapambano ya bunduki ya kuwang’oa wakoloni barani Afrika.


Pia ifahamike kwamba pamoja na mambo mengi ambayo Mwalimu aliyachukia na kuyakemea kwa nguvu zote lakini pia Mwalimu alikemea rushwa, wizi, kujilimbikizia mali ambazo chanzo chake hakipo wazi, unyonyaji, matumizi mabaya ya madaraka, mataba, kutokuwa wazalendo n.k Haya ni sehemu tu ya yale ambayo yalikemewa kwa nguvu zote katika uhai wake wote. Ninaikumbuka hata hotuba yake ya mwezi june wakati Watanzania wanataka kujua msimamo wake juu ya hatima ya Tanzania baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi alikemea sana juu ya mataba na alikataa kumzungumzia Mh Mrema kama mtu tishio kwenye siasa za wakati huo kama alivyokuwa ameombwa kufanya hivyo.

Mimi ninapata mashaka tunapokuwa tunamuenzi Nyerere kama maigizo. Watu wanamuenzi kama maigizo kwa kuwa matendo na maneno yanakinzana. Ni wazi kuwa sijamuona mtu yeyote akimpinga Nyerere hadharani, nilishawahi kumshuhudia Mh Lisu tu ijapo naye baada ya kauli yake ile alipingwa na Watanzania wengi ndani ya Bunge na nje ya Bunge. Unapojaribu kusoma hapa uwe na mtu wako kichwani na unamfikiria kuwa je, anayosema kuhusu Nyerere yeye anayafuata?Hii ni kwa kuwa wapo wanaotuelekeza juu ya sifa za hayati, lakini wao wakiwa na madoa madoa mengi.

Kila nikiangalia vyombo vya habari, nikitazama wanaomzungumzia Nyerere huku wakimpamba kwa wino wa kila aina huwa ninapata maswali mengi. Moja ninajiuliza, hivi kipindi cha maisha yao hata kipindi cha uongozi wao je haya walitimiza? Hawakuwa wezi? Hawakuwa wabinafsi? Hawakuwa wanajilimbikizia mali? Walikuwa wazalendo? Hawakuwa watu wa matabaka? Kama hawakuwa hivyo na walikuwa wakifuata misingi ya Mwalimu kwa nini maendeleo ya nchi hayafanani na umri wa Taifa? Inaniskitisha kwa kuwa wapo waliofanya kazi ndani ya vyama vyetu na ndani ya serikali yetu ambao wakipata nafasi ya kumzungumzia Mwalimu wanamzungumzia vizuri kweli, lakini wanasahau kutwambia je wao walifanya kama ilivyokuwa Mwalimu? Mwalimu mzuri ni Yule anayefundisha kwa vitendo, Mwalimu ambaye wanafunzi hawawezi kuwa na mashaka na mafundisho yake. Lakini ukiona Mwalimu unafundisha huku wanafunzi wanalala ujue wanamashaka na mafundisho yako.

Ninadhani tunapomunzi Mwalimu usiwe muda wa kueleza tu kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa hivi na hivi bali ninatamani sasa mtu ukipewa podium wambie Watanzania sifa za Mwalimu lakini pia wambie mimi katika nafasi au maisha yangu hili na hili lilinishinda ninaomba WATANZANIA MNISAMEHE. Unaweza ukawa ulikuwa na nafasi yoyote, njoo hadharani kuwa hapa mimi nilikosea katika utumishi wangu. Tumuenzi Mwalimu kwa vitendo na si kwa maigizo.

Yapo ambayo kwa leo ni ngumu kuyatekeleza na ambayo mwalimu aliyamini hii ni kwa kuwa muda na wakati umebadirika. Kwa mfano kipindi cha Mwalimu tuliamini katika ujamaa na kujitegemea leo hii Dunia imebadirika na tueshaingia kwenye ubepari bila kupenda. Katiba yetu bado naamini ktk ujamaa lakini fikra na mawazo yetu yanaishi katika Ubepari. Lakini je huu ubepari na mali tulizonazo tumezipata katika misingi ya haki na usawa kama ambavyo Mwalimu aliamini? Kuna watu waliwahi kuwa maDC, maDED, Mawaziri, Watumishi serikalini n.k walianza utumishi wakiwa hoi, lakini muda mfupi wakawa a mali nyingi, mali ambazo hazifanani na mapato yao.

JPM anajaribu kurudisha misingi, lakini anarudisha misingi kwenye Taifa ambalo kama ni chuma kimejikunja sana. Chuma kinahitaji moto mkali utakao msaidia Sonara kukinyosha. Juzi akiwa Katavi amesema anataka alinyoshe Taifa na mimi ninamuombea alinyoshe. Ili chuma kinyoshwe lazima kiunguzwe sana kwenye moto, na hizi kelele ndogo zilizopo mtani ni dalili kuwa chuma kimepata moto na kinanyooka. Ni muombee JPM aendelee kutunyosha, asiwasikilize wanaombeza. Mifano hii imtie moyo kuwa ni kawaida ya Watanzania. Nyerere akiwa madarakani alibezwa na kusimangwa lakini alipoondoka alikumbukwa hadi leo anakumbukwa. Mzee mwinyi alitukanwa kila aina ya matusi akiwa Rais kitu klichosababisha kutokea hata kundi la akina Kasaka na wenzake na mwaka 1994 kama siyo 1993 Mrema aliasi baraza la mawaziri kwenye swala la MWEKEZAJI CHAVUDA. Lakini bada ya Mwinyi kustaafu alianza kukumbukwa na Watanzania hwa hawa kuwa Mkapa ameficha pesa bora mzee ruksa. Hii haikutosha mwaka 2005-2015 JK alitukanwa matusi yote, hawa walio kuwa wakimtukana Mkapa ndio walianza kumtukana JK na kumsifu Mkapa. Walisema bora MKAPA nchi ilikuwa inaenda(Siwataji majina). Baada yaw ewe kuingia, wale waliosema Kikwete hafai na ni dhaifu ndio wale ambao leo wanasema hatakuja kutokea Rais kama JK. Hii naonyesha wazi watanzania ni wachache wanaompenda mtu aliwa madarakani, ila akitoka. Hata wewe utakumbukwa mno kwani siku ukistafu meli zote ulizonunua huta peleka Chato, Ndege ulizonunua hautapeleka Chato, barabara unazotengeneza hautapeleka chato, makao makuu kuyapeleka Dodoma hautapelk Chato, Mashule na Hospitali unazojenga hautazihamishia Chato na mambo mengine yote, bali ukistafu vitaendelea kutumika na Watanzania wote. Endelea kumuenzi mwalimu kwa vitendo.

Kwa muda mfupi umeandika historia kubwa, umefanya mambo ambayo yataendelea kuishi hata bila uwepo wako. Wewe ni shuja na ni mtu hodari kwa kuwa ueamua kufanya yale uliyotamani kuyaona tangu ukiwa waziri. Umeamua kuziba masikio kwani najua Watanzania ni hodari wa kupiga kelele zinazowezakukupoteza kwenye uelekeo. Hata Nyerere wakati anadai uhuru aliziba masikio kwani Watanzania walijua anawapeleka kwenye vita ya tatu ya dunia au vita ya majimaji. Walianza kumuelewa bada ya kupata uhuru, ijapo akina Tunteeke Sanga bado hawakumuelewa hadi alipokuja kung’atuka.

Ukisikiliza hotubaza mwalimu na kusoma badhi ya vitabu vyake basi utakutana na maneno haya; "Uhuru na kazi", "Hakuna taifa lenye haki ya kufanya maamuzi juu ya taifa lingine; wala hakuna mtu mwenye haki ya kumfanyia maamuzi mtu mwengine’’, "Umoja hautatufanya tuwe matajiri, lakini itaifanya vigumu kwa Afrika na Waafrika kupuuzwa na kufadhaishwa","Elimu sio njia ya kuepukana na umaskini, ni nia ya kuapambana nao", "Ili kupata maendeleo ya kweli, watu lazima wahusishwe."
 
Kuelekea 2020 tutaona makala nyingi sana za kujipendekeza ili mpate majimbo. Lengo mnataka sote tuimbe sifa tu kwa jiwe.
 
Nilipo ona namba ya simu umeiweka juu nilipata jibu ya nia yako haya umeshinda tusubiri uteuzi baada RC kumwagwa
 
Maelezo mengi! Kumbe lengo lako kuu ni moja tu , kumuimbia mapambio ya kumsifu na kumtukuza malaika wako mkuu. Mada zenu hazina tofauti na zile za wale matapeli wa "tuma hiyo pesa kwenye namba hii"

Mnachokifanya ni kubadili tu maudhui. Hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom