Tusidharau kauli yote tunamwachia Mungu

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
6,180
13,592
Watu waliwadhihaki sana waliokuwa wanaonewa kwa kusema YOTE TUNAMWACHIA MUNGU.

Nakuwatukana eti watanzania ni wajinga na kamwe hawatakombolewa kwa kusema yote tunamwachia Mungu.

Vilio vingi sana vilisikika watu walipobomolewa nyumba zao na kusema YOTE TUNAMWACHIA MUNGU.

Waliobambikiziwa kesi walilia kwa uchungu waliposema YOTE TUNAMWACHIA MUNGU . Wapinzani kwenye uchaguzi walisema yote tunamwachia Mungu Wakachekwa.

Waliopoteza ndugu zao kwa kuuwawa, waliotekwa, walioporwa hela na mali zao walisikika sana wakisema YOTE TUNAMWACHIA MUNGU.

Hata Mo alisema YOTE ANAMWACHIA MUNGU. Na walipokuwa wakitaamka haya YOTE TUNAMWACHIA MUNGU walichekwa na kudhihakiwa na kuitwa wajinga.

Mtu ana dola mamlaka na hazina anakuonea na kajawa na kiburi hutakiwi kushindana naye. Wewe inamisha kichwa tu chini na kusema YOTE NAMWACHIA MUNGU.

Tumeona yaliotokea kwa kusema YOTE TUNAMWACHIA MUNGU.

Tusidharau huu msemo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom