Tusidanganyane: CHADEMA haina nguvu ya kushinda jimbo la Kinondoni

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,183
3,547
Katika kosa ambalo CHADEMA wamefanya na litawagharimu ni kusimamisha mgombea wa ubunge katika jimbo la Kinondoni huku wakitambua CUF wamesimamisha mgombea.

Katika jimbo la Kinondoni kuna maeneo ambayo CHADEMA inakubalika na kuna maeneo ambayo CUF inakubalika.

Maeneo ambayo CUF ina nguvu na inakubalika muda mrefu ni ;

1.Maeneo ya Tandale

2.Maeneo ya Magomeni suna

3.Maeneo ya Magomeni Kagera

3.Maeneo ya Magomeni Mzimuni

4.Maeneo ya Mwananyamala karibia yote .

5.Maeneo ya Kigogo yote

Haya ni maeneo ambayo CUF ina nguvu muda mrefu.

CHADEMA inakubalika sana maeneo ya Kinondoni na Kijitonyama .

Ukirudi katika uchaguzi wa ubunge CHADEMA kaweka mgombea na CUF kaweka mgombea na katika uchaguzi huu obvious CUF na CHADEMA watagawana kura.

Lakini pia CHADEMA ina wakati mgumu sana kukubalika maeneo ya Kigogo, Mwananyamala, Magomeni na Tandale kutokana na maeneo haya CUF inakubalika na ipo muda mrefu sana tangu 1995 chama kimejijenga sana.

Hivyo wanaoamini CHADEMA itashinda wanajisumbua bure lakini pia CUF pia haiwezi kushinda Kinondoni kwa sababu ya kata za Kinondoni na Kijitonyama CHADEMA inakubalika.

Hivyo wanaoneza propaganda CHADEMA itashinda wanajidanganya na CUF kama itashinda wanajidanganya pia

CCM ameshashinda mapema
 
Kwani watu huwa wanasimamisha wagombea wakiwa na uhakika wa asilimia mia watashinda? Ndo maana ya uchaguzi unasubiri matokeo. Huu uhakika wa kupata ushindi hata kabla ya kura Ndo unawafanyaga wengine wanasusa. Uchaguzi wa nn kama mshindi tayari anajulikana? Wamtangaze tu. Hata kwenye mpira Kuna wakati yanga inafungwa na mbao Fc. Lolote linawezekana. Tusubiri matokeo na yaheshimiwe.
 
Tatizo ndilo hilo, pamoja na maelezo yako Mimi napingana na we we mtoa post, kwa sababu watu kwa sasa wanamchagua mtu/mgombea aliye bora, labda kama ni jimbo la vijijini kwa kiasi Fulani ningekubaliana na wewe.

Lakini pia upande wa pili tunaangalia nani kasimamishwa, kikubwa hapa ni kusubiri jalamba lipigwe ajulikane nani anakubalika kwa wananchi, vinginevyo utabiri wako hauna tija.
 
Hoja yako itakua na mashiko ramda cuf kama watamshimamisha mgombea tena cuf Malimu sefu sio cuf Lipumba coz magomeni mapipa ilikua ngome ya ccm lakini hakuna tena ubishi watu wamagomeni ccm hawaitaki tena mim mwenyewe na kaa magomeni mapipa mulize Chambuso anajua nini kilimpata ambae alikua mgombea udiwani kata ya mzimuni mbona kazi ipo usichukulie poa huyo Mtulia tumempa kura hata kampeni zake watu walikua hawamsikilizi coz watu walikua wameichoka ccm na alipata kura nyingi sana ujue sasa atarajia kuachia jimbo ramda mkimbie na masanduku ya kura na kutumia nguvu za dola lakini ngoma ikiweka hazarani ccm kinondoni msichukulie poa hata kidogo
 
Tatizo ndilo hilo, pamoja na maelezo yako Mimi napingana na we we mtoa post, kwa sababu watu kwa sasa wanamchagua mtu/mgombea aliye bora, labda kama ni jimbo la vijijini kwa kiasi Fulani ningekubaliana na wewe.

Lakini pia upande wa pili tunaangalia nani kasimamishwa, kikubwa hapa ni kusubiri jalamba lipigwe ajulikane nani anakubalika kwa wananchi, vinginevyo utabiri wako hauna tija.
Mkuu siasa za kinondoni zimegawanyika katika itikadi

Kuna maeneo ambayo CUF HAIWEZI KUPATA KURA BILA SUPPORT YA CHADEMA.

kuna maeneo CHADEMA haiwezi kupata KURA bila support ya CUF
 
Back
Top Bottom