Habarini wanajamii forum!
Tuingie kwenye mada moja kwa moja..
Mimi ni kijana aged 24 years,katika kipindi fulani cha maisha nikiwa shule ya msingi nilipoteza uwezo wa kusikia (deafness) nasikia lakini si kwa ufanisi so i need special care while talking!
Mwaka uliopita nimehitimu mafunzo ya ualimu Grade A,kufika kitaa kusaka vibarua hapa na pale coz life ni tight mno! Kupata vibarua ikawa msala coz ya hili tatizo unaambiwa tu wewe husikii huwez fanya hii kazi!
Eeh! Unabaki umezubaa tu unajiask sasa kutosikia kwangu na hii kazi kuna uhusiano gani? Mbona kazi haihitaji too much communication?
Anyway unaenda tu kusaka mahala pengine wanakuangaliaaaaa mwisho wanasema sijui tukusaidiaje! Unabaki frustrated mbna me nahitaji ajira instead naulizwa nisaidiwajwe!!!
Baada ya kusota bila mafanikio nikaona life is toi short acha nitumie kataaluma kangu kabla sijafa so nikafind shule binafsi nijitolee majibu yao unaweza tamani ufe! Ardhi ikumeze upotee hii dunia!! Ila unaambiwa uvumilivu ni mafanikio!
Sasa leo nimeenda private moja ya mwisho hapa town nkaandaa barua yangu ya kuomba kujitolea nikapeleka bwana nikatolewa mkuu na kibarua changu tena na sister ambaye ndo msimamizi wa hiyo shule!
Hata kutembea nilishindwa maana ni maumivu tu kosa langu ni nini? Tumeshaambiwa tusihoji maamuzi ya muumba wetu hivyo sina la kumlaumu ila MENGINE HAYA YANAUMIZA SANA!
jaman msiwe mnafanya hivi maana hata sisi tuna mioyo sio chuma sema tu hatuna wa kumlilia!