Tusemezane Jumapili: Muujiza wa LANCIANO

Tusemezane Jumapili: Muujiza wa LANCIANO

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
20,212
Reaction score
35,865
Tumsifu Yesu Kristo,

Muujiza huu ulifanyika mwanzoni mwa karne ya saba, wakati mtawa wa Basilia alipokuwa akisoma Misa. Baada ya kubariki mkate na divai, alianza kuona mashaka kama kweli katika kalisi ile na mkate ule ni kweli ni Mwili na Damu ya Kristu. Wakati huo huo , wakiwepo mashahidi wengi, ghafula aliona hostia ile ikibadilika kuwa sehemu ya mwili hai, na divai kuwa damu halisi, iliyoganda katika matone saba ya ukubwa tofauti.

Katika muujiza huu, kitu kingine hakikuelezwa, kilitokea tarehe 17 February 1547, mbele ya Askofu Mkuu Rodriquez na umati wa watu. Walipopima kila tone la damu ile, ambapo matone yalikuwa na ukubwa tofauti, kila tone likawa na uzito wa matone matano pamoja.

Muujiza huu wa Nyama na Damu ulifanyiwa majaribio kwa muda mrefu. Mwili huo na Damu huheshimiwa hata leo, Kanisa la Mt. Francis.

Mtawa mdigo katika konventi, aliyepewa uangalizi wa Kanisa, muujiza ulimtokea, alitaka kuthibitisha muujiza huo. Kwa idhini ya Roma, kililetwa kikundi cha wataalamu kuupima Mwili na Damu ile iliyoganda. Kati ya November 1970 na mapema machi 1971, ulifanyika uchunguzi mkali wa maabara uliofanywa na maprofesa Linoli na Bertoli kutoka Chuo Kikuu cha Sienna.

Tume ya madawa ya U.N.E.S.C.O ilithibitisha matokeo ya uchunguzi wao kwa majaribio 500 yaliyochukua miezi 15.

Ufuatao ni uamuzi baada ya majaribio yaliyoenezwa dunia nzima;

1) Ile ni damu kweli na mwili kweli
2) Damu ile na Mwili ule vinatoka kwenye mwili wa binadamu
3) Nyama (mwili) ile ni ya tishu za moyo (Myocardium)
4) Mwili ule na damu ile vina damu ya aina moja AB
5) Picha ya damu hii inalingana na damu ya binadamu iliyochukuliwa kwenye mwili wa binadamu siku ile ile
6) Mwili na Damu ile ni vya binadamu wa kweli
7) Hakuna alama za kujipenyeza dawa ya kutunza visioze
8) Jinsi nyama hii ilivyokatwa kutoka kwenye moyo, inahitaji ujuzi wa pekee kabisa wa mtaalamu wa madawa
9) Hakuna dalili zilizoonekana hata za kuanzaanza kuoza Mwili ule na Damu, ingawa vimekuwepo karne nyingi.

Muujiza huu ukakuimarishe imani yako unapopokea Ekaristi Takatifu ili upate uzima wa milele.

Source; kitabu cha MAWARIDI ya SALA.

Pia karibuni Emaus Centre karibia na stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo katika kambi ya uponyaji.
IMG-20190215-WA0000.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom