Tusemeje hii

kande kavu

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
234
86
Waungwana maajabu ya watanzania /Viongozi wetu yanaendelea.

Jioni hii wakati natoka kizigoni, mbele yangu kulikuwa na Prado jeupe lenye kibao kilichoandikwa W UL pale sehemu ya namba yagari. Nikawa nashangaa huyu kaacha wapi V 8 lake. Punde nikapata wasaa wakuwa ubavu kwa ubavu na gari hilo. Hamadi! mbele kulikuwa na dereva tu na viti vya nyuma Chinese/Japanese wawili wameketi raha mustarehe.

Je hii ni sawa kwa hizo namba za magari ya wanene wetu kutumika hata kama wao hawayatumii magari haya? Nini maana yake? Na kwa kuwa wanene wengi wa kada hiyo na manaibu wao wanatumia V 8, hiyo pleti ilifikaje kwenye Prado kama si kimkakati? Na kama ni kimkakati, nani anafaidika hapo? Aaah kweli watanzania tu wakarimu!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom