Tuseme ukweli daima, kimya na kuficha kutatumaliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuseme ukweli daima, kimya na kuficha kutatumaliza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchapakazi, Sep 18, 2009.

 1. M

  Mchapakazi Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu Watanzania wenzangu,

  Sijawahi kuchangia wala kuandika hoja katika uwanja huu mbali ya kuwa mwanachama kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kilichonivuta leo kuandika hapa ni upotoshaji wa hali ya juu ambao jamii ya Watanzania imekuwa inafanya jambo ambalo laweza kumaliza hiki kizazi.

  Jambo hili kubwa linalonikera ni vitendo vya kuficha kwa makusudi tu sababu ya vifo vya hao waheshimiwa. Ni ukweli ulio wazi "data ninazo" kuwa Amina chifupa kafa kwa UKIMWI na mumewe Mpakanjia kamfuata kwa UKIMWI huo huo less than two years later. Lakini utakachosikia alikuwa na Pneumonia. Kwa nini mdanganye? Semeni basi kafa kwa ugonjwa ambao hatutaki kuusema..tuelewe kimoja.

  Hii tabia ya kuficha ficha na kusingizia kulogwa, pneumonia, malaria na kuendelea haiisaidii jamii ya kitanzania na mapambano dhidi ya UKIMWI.

  Au mnasemaje wadau?

  Naomba kusahihishwa ila hoja ndo hiyo aliyesikia na asikie ataeona nina wivu ni haki yake kuona hiyo.

  Nawakilisha
   
 2. Madikizela

  Madikizela JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2009
  Messages: 320
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na mtoa mada, lakini hata kimataifa health status ya mtu ni siri, sijui wewe una ushahidi gani kuhusu hayo, ninasema nina kubaliana kwa sababu ni ukweli na uwazi pekee ndiyo tiba kubwa ya kuzuia maambukizi zaidi, lakini bado sheria zetu na kanuni haziruhusu "kumnyanyapaa" mtu. Tuanze kupiga vita kanuni kama hizo ili kuondoa janga hili. Tatizo kubwa katika hili ni UNAFIKI wa bin adamu hawapendi mtu ajue kuwa ngono inafanyika na hioi diyo chanzo cha UNAFIKI!!. Hakuna maradhi yanayo ua kama Malaria! lakini hakuna unyanyapaa katika hilo!!

  Hatuna budi sisi kama Taifa tukubaliane kuwe na uwazi
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Bwana mdogo una ushaidi wa unalolisema?. Wewe ni daktari aliyewahudumia marehemu hao?. Acha uzushi usio miguu wala mikono.
   
Loading...