Tusaidiane ushauri juu ya mahusiano haya

Tusaidiane ushauri juu ya mahusiano haya

amu

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2012
Posts
16,171
Reaction score
31,357
Jamani nipo na mdada mmoja tupo sote kwenye program moja hivi huku vijijini actually ni office mate wangu na tupo karibu sana.
Sasa ngoja mnisaidie gt's wa mmu tokea jana binti hana raha kula hali kulia yeye sababu ni hii.

Ana mchumba wake mwaka na zaidi sasa na walipanga waoane mwaka huu kwa maelezo yake na niliyoshuhudia kweli jamaa anampenda jamani maana chrismass alifunga safari toka kusini mwa tanzania kuja kaskazini ya Tanzania kuspend nae holiday tatizo toka wajuane mwaka huu na zaidi hawajawahi kuwa na amani wao kila wakikutana haijalishi wapi kugombana,kufokeana kususiana yaani vururu vururu.

Imagine upo na mpenzi wako umemmiss then mkionana dakika chache mnagombana maelezi ya bi dada kuwa mwanaume hana kifua yeye kitu kidogo ataongea weeeee afu bi dada anaamini mwanaume hutakiwi uongee sana mtu hata kama mtu amekuudhi sana hiyo yashusha manhood.

Kingine mwanaume hajui kujiongeza yaani kila kitu yeye anamuuliza mwanamke hata vile vinavyoonekana wazi lazima aulize hapo ndo bi dada anapokasirika na kumjibu"wewe ndo utakuwa kichwa cha familia hata hili nalo la kuuliza?dogo hivi?kama hujui la kufanya usiniulize "hapo automatically ugomvi unazuka.

Mwanaume wake mbishi sana afu hajui kwamba yeye ni mbishi anabisha baada ya mda ugomvi ukitulia anakubali kosa.
Kila analotaka mwanaume/au kulifanya lazima amlazimishe mwanamke alifanye.

The guy he is not smart anaweza akatoka kusafiri mda mrefu safari ndefu kabla hata hajaoga kuondoa vijiharufu anataka kumparamia ndo hapo bi dada anapokataa na ugomvi unaanzia,harufu ya kikwapa hatari hata bodyspray hajui inauzwa sh ngapi.

Ila bi dada nae kiboko ana hasira balaa mimi namjua anaweza kukupa jibu moja ukawaza kwa nini kanipa hilo hilo jibu siku nzima afu mwenzako hana huo mda keshakupa lake huyo yake yanaendelea.

Sasa mwanaume tokea jana kamwambia kuwa mahusiano yaishie hapo sababu toka amfahamu hajawahi kuinjoi kuwa na yeye pia afya yake inatetereka kutokana na kuwaza sana hayo mahusiano jinsi ya kuyaokoa.

Maelezo ya bidada kuwa anampenda sana sababu zinazomkwaza ni hizo na anamweleza ajirekebishe mwanaume mbishi harekebishiki na hataki waachane mwanaume he seems to be serious japo anakeep on replying her msgs and receiving calls but he insist to end up relationship wawe to marafiki.

Hii issue ni nzito mie imenshinda kwa kweli naileta kwenu wanajukwaa tusaidiane.
Huyu bi dada amrudishe mpenzi wake.
 
Mimi bwana naona waachane tu haiwezekani uwe na mpenzi kika mkionana mgombane no enjoyment ila kumwambia bi dada ndo ngumu jamani japo namuonea huruma anavyohangaika kumrudisha mpenzi wake.
Na nyie wanaume mjifunze jamani vikwapa vinaturn off yaani mzuka wote unaisha na mapenzi siku zote kama unaweza kufanya kitu fulani.si lazima na mwenza wako.akifanye au umlazimishe akifanye hapo lazima mkosee.
Afu natamani kumuuliza shost uwezo wa bwana shem kitandani ila nashindwa maana nahisi atakuwa zero angekuwa anaperform vizuri bibie angekuwa mpole 😛 😛 dawa ya majeuri kama bi dada mgegedo wa haja.
 
Me what i believe if something wasnt meant to be it wont happen.
Dada apige moyo konde nae ampotezee wapeane space kama kweli wameumbwa kuwa wote watarudiana tuu hata iweje,
asiforce mambo.. Aende na flow ya huyo mkaka. Otherwise ataishia kuumia. Amwombe sorry kwa kumjibu vibaya ila asiforce mambo.
 
Hamna kitu hapo. Wanadhani wanapendana ila wajaribu kupeana space ndo atagundua kuwa walikua wanapotezeana muda tu. Ile chemistry haipo hapo. Eti kikwapa kikwapa kitu gani? Mi hata niwe nimetoka kulima yule mama huniparamia hata kabla sijafunga mlango vizuri, tena ndo niwe nimetoka safari?? Ohoooo hata choo cha stendi tunaweza kwenda kwakuona nyumbani mbali. It wasnt meant to be kama alivyoseema mdau hapo juu wanalazimisha naona. Kama mnapendana you will find a way to sync tu iwe isiwe. Halafu hilo la KIWANGO lina uwezekano mkubwa sana kuwa jamaa ni amateur....
 
Maisha ndo yalivyo wagombanao ndio wapendanao. Hao ndio wanatakiwa kuoana maana kila mtu anajua hasira za mwenzie na makucha ya mwenzake. Usiombe akutane na yule ambaye anajibu ndio kwa kila kitu akisha olewa na kuzalishwa taaabu tupu itaingia.
 
amuuuuuuuuuuuuu..........hapa sidhani kama utapata msaada sana. Hiyo ngoma waachie wenyewe tu. We mpe kampani tu, mambo ya kumrudisha au kuachana hayakuhusu. Kaa mbali kabisa.
 
Washachokana hao......kila mmoja aangalie ustaarabu wake!!!!!!
 
Ebwana mi yangu machache tu:
No one is perfect in this world: Mnapoingia kwenye mahusiano ni lazima mmoja wenu awe mpole ilikuweza kudumu nakufikia malengo ya ndoa nakuishi mda mrefu, pia kwa upande wa wanawamke mbadilike kuwa waropokaji, unapoliona jambo linakukera sio kujifanya wewe ndio msafi kuliko mwenzi wako just tumia usitarabu na hekima kumuelimisha nakufikisha japo kiasi ambacho na yeye aone ni kosa akae nakutafakari nakuliacha taratibu but sio kurupuka nakutaka kili unasema akafuata haraka hatuendi hivyooo.... kumbuka wote mmelelewa na kukulia mazingira tofauti. ni hayo tu.
mfikishia huu ujumbe huu mwambie kama kweli anampenda abadilike na sio kumtangaza kwani na yeye anakasoro ambazo Jamaa nae zinamkera sema haropoki kwa watu kama yeye.
 
Huyo mwanaume ni pasua kichwa nahisi hawaendani yani interest zao tofauti hili nalo ni tatizo katika mahusiano! Siamini kama mtu mmemisiana then muda mfupi mgombane,kuna tatizo hapo, bidada aache kulialia atapata wa kuendana naye!
 
Mi nafikiri huyo dada naye anakosea kashamwambia jamaa kuhusu kikwapa na mambo ya usafi kabla ya kugegedana jamaa haelewi. Yeye si angejichukulia uamuzi wa kumnunulia body spray kama zawadi, na akija kumtembelea akitaka mambo anamtreat kimahaba na kumpeleka kwanza bafuni amuogeshe na mambo mengine yaendelee bila kupigizana kelele.

Labda kama kuna mambo mengine zaidi ya hayo. Wanasema mtu akipenda chongo huita kengeza.
 
jamaa keshasema "ITS OVER" anachotaka bdada nin tena wakat kero za hlo penzi anazjua? Au bado maumivu, harufu ya kwapa, kuulizwa maswali asiyostahili havijamtosha??
 
'''wewe ndo kichwa cha familia,hata hili ni la kuuliza?''
hii kauli ukimwambia mwanaume lazima aone unamdharau

na hizo spray na deodorant angemfundisha kuzipaka

ampe muda..atulie kwanza..
 
J
Ila bi dada nae kiboko ana hasira balaa mimi namjua anaweza kukupa jibu moja ukawaza kwa nini kanipa hilo hilo jibu siku nzima afu mwenzako hana huo mda keshakupa lake huyo yake yanaendelea.
.
229748_v0_220x145.gif
 
Jamani eeeee nipo na mdada mmoja tupo sote kwenye program moja hivi huku vijijini actually ni office mate wangu na tupo karibu sana.
Sasa ngoja mnisaidie gt's wa mmu tokea jana binti hana raha kula hali kulia yeye sababu ni hii.
Ana mchumba wake mwaka na zaidi sasa na walipanga waoane mwaka huu kwa maelezo yake na niliyoshuhudia kweli jamaa anampenda jamani maana chrismass alifunga safari toka kusini mwa tanzania kuja kaskazini ya Tanzania kuspend nae holiday tatizo toka wajuane mwaka huu na zaidi hawajawahi kuwa na amani wao kila wakikutana haijalishi wapi kugombana,kufokeana kususiana yaani vururu vururu.
Imagine upo na mpenzi wako umemmiss then mkionana dakika chache mnagombana maelezi ya bi dada kuwa mwanaume hana kifua yeye kitu kidogo ataongea weeeee afu bi dada anaamini mwanaume hutakiwi uongee sana mtu hata kama mtu amekuudhi sana hiyo yashusha manhood.
Kingine mwanaume hajui kujiongeza yaani kila kitu yeye anamuuliza mwanamke hata vile vinavyoonekana wazi lazima aulize hapo ndo bi dada anapokasirika na kumjibu"wewe ndo utakuwa kichwa cha familia hata hili nalo la kuuliza?dogo hivi??kama hujui la kufanya usiniulize "hapo automatically ugomvi unazuka.
Mwanaume wake mbishi sana afu hajui kwamba yeye ni mbishi anabisha baada ya mda ugomvi ukitulia anakubali kosa.
Kila analotaka mwanaume/au kulifanya lazima amlazimishe mwanamke alifanye.

The guy he is not smart anaweza akatoka kusafiri mda mrefu safari ndefu kabla hata hajaoga kuondoa vijiharufu anataka kumparamia ndo hapo bi dada anapokataa na ugomvi unaanzia,harufu ya kikwapa hatari hata bodyspray hajui inauzwa sh ngapi.
Ila bi dada nae kiboko ana hasira balaa mimi namjua anaweza kukupa jibu moja ukawaza kwa nini kanipa hilo hilo jibu siku nzima afu mwenzako hana huo mda keshakupa lake huyo yake yanaendelea.
Sasa mwanaume tokea jana kamwambia kuwa mahusiano yaishie hapo sababu toka amfahamu hajawahi kuinjoi kuwa na yeye pia afya yake inatetereka kutokana na kuwaza sana hayo mahusiano jinsi ya kuyaokoa.
Maelezo ya bidada kuwa anampenda sana sababu zinazomkwaza ni hizo na anamweleza ajirekebishe mwanaume mbishi harekebishiki na hataki waachane mwanaume he seems to be serious japo anakeep on replying her msgs and receiving calls but he insist to end up relationship wawe to marafiki.
Hii issue ni nzito mie imenshinda kwa kweli naileta kwenu wanajukwaa tusaidiane.
Huyu bi dada amrudishe mpenzi wake.

hapo kwenye rangi kama vile pamepishana...............

hao wote pasua kichwa tu na hakuna anayemfaa mwenzake............

ni rahisi kwa sisi kusema piga chini kwenye mapenzi , ila wenye maamuzi ya mwisho ni wao wenyewe............

ishu ya usmart hapo hata huyo bidada inaonekana amechangia , km hana spray si ampe zawadi ya spray .............

hlf mambo mengine mbona yanazungumzika.
 
jamaa keshasema "ITS OVER" anachotaka bdada nin tena wakat kero za hlo penzi anazjua? Au bado maumivu, harufu ya kwapa, kuulizwa maswali asiyostahili havijamtosha??

mapenzi bana ni temporaly madness,yaani unajifanya huoni kabisa, unajikuta unavumilia mambo ya ajabu tu, hadi baadae ukiwa kwenye akili zako timamu unajishangaaa,
 
'''wewe ndo kichwa cha familia,hata hili ni la kuuliza?''
hii kauli ukimwambia mwanaume lazima aone unamdharau

na hizo spray na deodorant angemfundisha kuzipaka

ampe muda..atulie kwanza..
Well said,mwanamke hana kauli nzuri mdomoni japo mtoa maada amejaribu kumkandia jamaa na kumtetea mwanamke mwenzake na siku zote mtu anapoleta mashitaka huwa anajitetea kwa upande wake ili aonekane mwema na hana kosa,sasa hapa la kujiuliza ni hili kama kweli dada kagundua na kayaona madhaifu ya mpenzi wake yanakera kiasi hicho na jamaa ameamua kujitoa iweje mwanamke ashindwe kula? hapo nadhani ndo angepumua maana naona alikuwa anahisi jamaa hawezi kuwa kichwa cha nyumba sasa analia nini?
 
Mimi bwana naona waachane tu haiwezekani uwe na mpenzi kika mkionana mgombane no enjoyment ila kumwambia bi dada ndo ngumu jamani japo namuonea huruma anavyohangaika kumrudisha mpenzi wake.
Na nyie wanaume mjifunze jamani vikwapa vinaturn off yaani mzuka wote unaisha na mapenzi siku zote kama unaweza kufanya kitu fulani.si lazima na mwenza wako.akifanye au umlazimishe akifanye hapo lazima mkosee.
Afu natamani kumuuliza shost uwezo wa bwana shem kitandani ila nashindwa maana nahisi atakuwa zero angekuwa anaperform vizuri bibie angekuwa mpole 😛 😛 dawa ya majeuri kama bi dada mgegedo wa haja.
Swali la kwanza mwanamke analia nini? kama kweli yote hayo uliyozungumza ndo yako hivyo hakuna mwanamke anayependa kuwa na mwanaume wa hivyo sasa anaposhindwa kula na kuwa na mawazohapo ninaamini mwanaume hayuko hivyo,huyo shost wako amekudanganya amemkandia jamaa halafu anamlilia wakati jamaa mwenyewe kasema yaishe mimi nilifikiri angefurahi tu!
 
Aaaaaa jamani yote mnayosema na mie musimamo wangu huo huo dada asonge mbele ila bi dada haamini kwa hilo ye anaona sijui mda umeenda mpaka ampate mwingine waanze upya tena.
Si unajua sie wadada tena
 
Labda kuna mengi nyuma ya panzia...ukute bidada ana makosa ila kwasababu umesikiliza upande mmoja unaweza kuamini mwanaume ana makosa..

Nachoamini mimi mapungufu ya mwenzako ukiyachukulia negative yatakusumbua sana...ila kama mapungufu hayo ukayabeba wew in positive way basi kama maugovi yatakuwepo hayatakuwa hayo yanayotokana na mapungufu ya mwenzi wako....

Kwahiyo hapo bidada akirudiana na huyo mkaka akubali kuyabeba yote...ila kama anaona hawezi basi waachane..aanze maisha mapya
 
Back
Top Bottom