Chanaiti
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 208
- 93
Habari wakuu?
Katika kuishi kwangu, nimeona mara kwa mara ndugu upande wa mume haswa kaka na dada wa mume kutoelewana na wifi/shemeji yao.Binafsi naelewana nao vizuri mno na najihisi furaha.Lakini kwa watu wengi ni tatizo, Mfano mpaka nimelileta hapa limenigusa. Mdogoangu ameolewa mwaka jana lakini anayoyapitia na kwa umri wake na ukizingatia ndoa ni changa ni magumu. Maneno yanatoka kila kona na hawa ndugu wote ni tegemezi kwa maana ya kuwa Kaka yao amekua msaada kwao kwa kila kitu kwani yeye pekee ndiye msomi na mwenye maisha bora.
Ikumbukwe kuwa wakati wa uchumba aliwahi kwenda kwenye msiba wa ndugu za huyu shemeji na akawa anatambulishwa ila haikua habari njema. Kwani mdogoangu alisikia wakiongea kwa lugha akamuomba mtu amuelezee na kilichosemwa kilikua" Ooh anaoa mpare basi sahauni misaada"Kwa kifupi ameyasikia mengi ila tulimtia moyo mpaka akaolewa kwa kuwa mumewe anampenda mno.
Sasa nimekua nikijuliza tatizo ni njaa kwamba huyu amekuja kutupokonya tulichokua tunapata au ni tabia tu?
Maana hata mimi nimeolewa kwa with waliokulia middle-class lakini tunaelewana vizuri
Je unafikiri tatizo ni nini?