Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,915
Ni hulka ya binadamu kukinai au kukichoka kitu fulani pale anapokuwa nacho au kukitumia kwa muda mrefu na hivyo hutaka kubadili/kukibadili kwani anakuwa amekichoka /amekikinai.
Mifano michache:
Binadamu akila chakula cha aina moja kwa muda mrefu au akila chakula cha aina moja mfululizo humfanya akikinai na kutaka kubadili aina ya chakula.
Binadamu huyu huyu akisikiliza aina fulani ya muziki mfululizo kwenye CD,n.k humchosha na kutamani kusikia nyimbo nyingine tofauti kabisa na hiyo.
Vile vile wimbo ukivuma sana baada ya muda fulani watu huuchoka(tunasema umechuja) hata kama wimbo huo ulikuwa unapendwa kiasi gani.
Binadamu huyu hata akikaa sehemu moja kwa muda mrefu utamsikia anaanza kulalamika hapa mahala pamenichosha jamani ngoja nibadili mazingira au nifanye utaratibu wa kuhama.
Watu pia habadili style na mitindo ya maisha kwasababu wamekuwa nayo kwa muda mrefu na hivyo style na mitindo hiyo inakuwa imewachosha.Mfano kina Dada na mitindo ya usukaji nywele,n.k.
Kali kuliko zote.Binadamu huyu humchoka hata binadamu mwenzake(mpenzi) na kuamu kumtosa na kutafuta mwingine.
Sasa kama tunaweza kukinai karibu kila kitu mpaka binadamu wenzetu, inakuwaje baadhi ya wenzetu "CCM" haiwachoshi?
Hivi vitu vingine binadamu tunavikinai automatically tu,sasa inakuwaje CCM hii na makandokando yake yote mtu bado haikuchoshi?
Sijui tumelogwa?!
Kwakweli sipati majibu wacha tu niishie hapa maana kichwa kimeanza kuuma na bahati mbaya hata hela ya panadol sina kutokana na hali ngumu ya uchumi mifukoni mwangu.
Mwalimu Nyerere,mwaasisi wa chama hikii, aliwahi sema CCM si mama yangu na kwamba siku kikikiuka misingi ya kuanzishwa kwake atajitoa.
Sasa kama Nyerere alitamka hayo,nyie wenzangu na mimi mnasubiri nini huko CCM wakati wamesema wazi kuwa hawawezi kufukua makuburi?