Tusaidiane Kuhusu 'Device is Write Protected'

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
31,918
63,920
Nimekutana na flash na memory card nyingi, mwanzo inakua nzima ila ghafla siku inafika unataka kuweka vitu inakukatalia halafu inakwambia 'Device is Write Protected' kama umechomeka memory card kwenye adaptor utajua tu ni adaptor kale kaswitch kametrip, utakarudisha.

Au kama flash yenyewe ina switch unairudisha na kazi itaendelea. Moto hua pale switch hakuna na memory card ndiyo inatoa onyo na siyo adaptor.

Mtandaoni wameorodhesha suluhisho la hili swala na hua wanashauri utumie Command Prompt au Registry Editor njia ambazo nimeshatumia na hazijawahi kunisaidia kutatua tatizo la write protection.

Suluhisho la kweli hua ni kuiformat hiyo flash kwa mtindo wa Low Level Format, na kuna tools kabisa za kufanyia hiyo kazi. Watu wengi ni wachoyo hua hawataji majina ya tools, nilienda Machinga Complex jamaa akanitolea nje nikaenda Mbagala bado nikatolewa nje.
Baada ya kuzunguka sana mtandaoni nikakutana na tool moja hivi ambayo ikanisaidia kutatua hilo tatizo kwa flash zote nilizokua nazo isipokua SanDisk cruzer blade haiwi detected na ile tool na mtandaoni hakuna tool specified for SanDisk.

Naomba member yeyote anayejua tool au namna ya kuiformat write protected SanDisk Flash anitajie hapa.

Natanguliza shukrani.

Pia tool ambayo ninatumia mimi kwa flash zingine inaitwa OnBelay. Icheki online.
 
Na wewe kama sio mchoyo tuwekee hapa hiyo tool ili na sisi itusaidie
Yaani nimekutajia jina ni wewe tu kudownload bado hutosheki? Mi mwenyewe hapa nauliza jina tu wala sijataka nigewe tool.
 
Atakayenisaidia nampa flash 4GB

IMG_20181107_154022.jpg
 
Na wewe umeupiga ukimya hujataja unategemea na me nikutajie ndugu... piga ukimya na sisi tunapiga ukimya..

Wenzako hadi link ya kudownload wanaweka hapa.. wewe maneno mengi kama mwanasiasa
 
Na wewe umeupiga ukimya hujataja unategemea na me nikutajie ndugu... piga ukimya na sisi tunapiga ukimya..

Wenzako hadi link ya kudownload wanaweka hapa.. wewe maneno mengi kama mwanasiasa
Boss mimi nimeomba jina la tool na mimi nikataja jina la tool ninayoitumia so kwa anayeitaka aidownload hata mi nikitajiwa jina nitaitafuta.
 
As you asked turnes out I had it: a "low level formatting tool"
Home Version
YCLY-6XLH-MHT8-3Q2J
Z2VG-D399-9KS3-T5CF
Commerical version
ZAXL-DPVZ-PD49-ATQ5
J6AA-QULA-9NMF-WYV6
 

Attachments

  • HDDLLFsetup.4.40.zip
    735 KB · Views: 27
As you asked turnes out I had it: a "low level formatting tool"
Home Version
YCLY-6XLH-MHT8-3Q2J
Z2VG-D399-9KS3-T5CF
Commerical version
ZAXL-DPVZ-PD49-ATQ5
J6AA-QULA-9NMF-WYV6
Chief nashukuru, ila hii haikunifanyia kazi niliwahi kuijaribu.
 
Leme help you!! Tafuta CD ya windows inayoboot, chomeka flash yako na ujue herufi yake, zima komputa, Fanya kama unapiga windows, ukifika sehemu ya kufomat hDD format hiyo flash yako kwisha habari yake
 
Leme help you!! Tafuta CD ya windows inayoboot, chomeka flash yako na ujue herufi yake, zima komputa, Fanya kama unapiga windows, ukifika sehemu ya kufomat hDD format hiyo flash yako kwisha habari yake
Shukrani wakuu.

Nitajaribu njia yako, nitaleta update kesho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom