Turudi kwenye misingi, ndoa zidumu na watoto wapate malezi bora

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Habari wadau,

Ni matumaini yangu mko poa. Leo ningependa tuangalie misingi ile ya zamani iliyofanya ndoa nyingi zikadumu na hata mabinti walikuwa wakiolewa wakiwa na bikira tofauti na leo.

Wakati huo kwanza mwanamke na watoto walikuwa wanahesabika katika orodha ya mali za mwanaume na hata kulala kitanda kimoja ilikuwa wakati wa tendo la ndoa tu. Tena mwanamke alipaswa alale nyumba moja na mbuzi, kondoo, ng'ombe, kuku, n.k lakini mwanaume hujenga nyumba yake mbali kidogo na hiyo yenye mali zake.

Ukweli ni kwamba ndoa hizi ndizo zilidumu muda mrefu na hata watoto walikuwa katika maadili mazuri. Huu utaratibu wa sasa wa mwanaume kulala kitanda kimoja na mali zake hadi watoto wanalala chini hadi wanaona ama wanasikia kinachofanywa na baba na mama usiku wa manane, vimechangia kurudisha sana maadili nyuma na hata kuchangia kwa kiasi kikubwa ndoa kuvunjika.

Turudi kwenye misingi ya kumtambua mwanamke kama sehemu ya mali za mwanaume, huu mtindo wa kusingizia kuwa ni mfumo dume, umeharibu na utazidi kuharibu ndoa nyingi na maadili ya watoto.
 
Well said mkuu...pia kuongezea wanaume tujifunze kutulia na wake zetu,wanawake watulie na waume zao..kuingia Kanisani au Msikitini kuwekeana nadhiri mbele za Mungu kisha mmoja wenu au wote kuvunja nadhiri hiyo ni mikosi ndani ya nyumba na familia yenu napia Mungu anawageuzia kisogo,uzinzi ni dhambi kubwa..pia kabla ya ndoa kila mmoja amuombe Mungu anaemwamini ampe mtu sahihi wa kuendana na mapungufu yake na makamilifu yake sio mnakutana facebook huko miez mitatu mnatangaza ndoa,no kaeni at least miaka miwili ndo mfanye uamuzi wa ndoa.kuvumiliana ni muhimu maana wote mnakutana ukubwani kila mtu alikuwa na malezi yake na ana tabia zake tukiyatekeleza haya tutakuwa na family zilizo bora na zenye furaha.
 
Una point, ila hapo kwny mwanamke kulala na mbuzi cjui kuku plsss ht km tunaishi Kijijini Mungu hapendi
 
Habari wadau,
Ni matumaini yangu mko poa. Leo ningependa tuangalie misingi ile ya zamani iliyofanya ndoa nyingi zikadumu na hata mabinti walikuwa wakiolewa wakiwa na bikira tofauti na leo.

Wakati huo kwanza mwanamke na watoto walikuwa wanahesabika katika orodha ya mali za mwanaume na hata kulala kitanda kimoja ilikuwa wakati wa tendo la ndoa tu. Tena mwanmke alipaswa alale nyumba moja na mbuzi, kondoo, ng'ombe, kuku, n.k lakini mwanaume hujenga nyumba yake mbali kidogo na hiyo yenye mali zake.

Ukweli ni kwamba ndoa hizi ndizo zilidumu muda mrefu na hata watoto walikuwa katika maadili mazuri. Huu utaratibu wa sasa wa mwanaume kulala kitanda kimoja na mali zake hadi watoto wanalala chini hadi wanaona ama wanasikia kinachofanywa na baba na mama usiku wa manane, vimechangia kurudisha sana maadili nyuma na hata kuchangia kwa kiasi kikubwa ndoa kuvunjika.

Turudi kwenye misingi ya kumtambua mwanamke kama sehemu ya mali za mwnaume, huu mtindo wa kusingizia kuwa ni mfumo dume, umeharibu na utazidi kuharibu ndoa nyingi na maadili ya watoto.
sirluta ulimwengu umebadilika mno kurudi huko ni vigumu labda tu tujitahidi kwenda na huu wakati kwa hekima na tahadhari kuu
 
Back
Top Bottom