Sanda Matuta
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 949
- 134
Kwa mnaoijua Uturuki, ni fursa gani za kibiashara zinapatikana huko?
mkuu mimi nilipata bahati ya kutembelea Uturuki na kufanya mikutano kadhaa ya kibishara kwenye maaneo yangu of interest.
Kwa kusema za ukweli ukiachana na watu wengi hapa wanongea mambo ya sio ya msingi na kuendeleza malalamiko kwenye thread hii,sisi tuna-nafasi kubwa ya ku-benefit na ushirikiano huu ila yatupasa kujituma na kuwa na nia za ukweli ilikufikia malengo.
Kuna wafanya biashara wengi sana wakubwa na wadogo wa kitanzania wanao jazana huko Uchina na nchi nyingi za Asia kufata bidhaanyingi zilizo chini ya kiwango,lakini kama wafanya biashara hao watahamishia mitaji yao kwa nchi kama hii ya Uturuki bila ya shaka ule msamiati ya ZA-KICHINA utafutika kabisa.kwani hao jamaa wanatengeneza bidhaa zilizo na ubora wa hali ya juu sana hasa bidhaa za viwandani kwenye nyanja zote.
Pili,haswa swala hili la kilimo ndio kabisa tunaweza kufaidika sana,kwani,kutokana na kilimo cha muda mrefu huko Uturuki toka enzi zakale ardhi yao imekosa au imeisha rutuba hivyo kufanya kilimo kuwa kigumu na kuwafanya wategemee sana ku-IMPORT mazao ya kilimo kwa kiasi kikubwa.Na hapa nadhani ndio sisi kama Watanzania ndio tunaweza kufaidika kwa kiasi kikubwa kwa kijiongezea pato kwa kupeleka huko mazao yeu.Tukifata na kuutekeleza mpango wa kilimo kwanza ni lazima tutafaidika tu na nchi hii.mimi binafsi nilipata order nyingi za mazao ya kutengeneza mafuta ingwa bado sijaingia kwenye nyanja hiyo.
Ni mambo mengi sana tunaweza kufaidika kutokea nchi hiyo,katika nyanja viwanda,biashara hasa ya vipuri vya magari,maeneo ya madini wao wanalo soko kubwa sana la madini pale Istanbul linakaribia lile la Ujerumani,mambo ya telecommication na tower building ili mladi kila sehemu za kiuchumi