Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,599
Ndugu wana MMU na wadau wengine wote wa jukwaa letu tukufu,
Toka tulipoanza mwaka huu wa 2012, niliahidi kwamba nitajaribu kila ninapopata nafasi kutoa maoni na ushauri wangu wa jinsi ya kuimarisha ndoa zetu kwa wale ambao tuko ndani ya game; na pia ushauri kwa wale ambao wanatarajia/wanatamani kuungana nasi katika hii taasisi muhimu.
Hivi karibuni, nilikuwa naongea na mjukuu wangu mmoja ambaye yuko njia panda. Yeye anataka kuoa mke yeyote atakayempenda ila ndugu na jamaa wanaomzunguka wamemshikia bango kwamba lazima atafute mchumba wa kabila lake. Yeye anapingana na ushauri huo ila bado anajiona kama vile anakosa ujasiri wa kuwakatalia ndugu zake.
Baada ya mjadala mrefu kidogo, nilimweleza kuwa katika maandalizi ya kuingia kwenye ndoa, kuna vitu vingi ambavyo ni muhimu sana kuvipa kipaumbele cha aina yake. Miongoni mwa vitu hivyo ni mapenzi/upendo na maslahi (uzuri, elimu, kiwango cha ustaarabu, utanashati, urembo na sifa nyingine za ndani na nje ambazo mhusika anazo). Hata hivyo alishangaa nilipomueleza kuwa, watu wa enzi zetu huwa tunachukulia kuwa sifa hizo zinazoangukia kwenye kundi la maslahi ni muhimu sana kwani ndizo zinazoweza kuifanya ndoa idumu au isambaratike haraka. Nilimwambia kuwa, sie tuliamini na tunaendelea kuamini kwamba, mapenzi/upendo katika ndoa yanakuwa ya msimu ila vigezo vya maslahi (vilivyo vingi) ni vya kudumu.
Huyu mjukuu alionekana kunishangaa pamoja na kumweleza kuwa hii imani yetu ina backing from natural theories za biology kwani kila kiumbe kinaangalia sifa ambazo zinatakiwezesha kuacha mbegu zake duniani; tena katika hali ya kushinda ushindani katika mazingira yake.
Kutokana na jinsi huyu mjuu wangu alivyobaki mdomo wazi, nimeonelea nilete hili jambo hapa ili kama wapo wanaoshangaa kama huyu mjuu wangu watoe maoni yao. Pia sitashangaa kama kutakuwa na wale ambao watanishangaa mimi pia.
Nawapenda sana na nawatakia week end njema!!
Babu DC!!